Kufunga ndoa na ujauzito ikoje kiimani?

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
17,167
26,143
Wadau,

Kuna hili swala huwa inatokea mtu anafunga ndoa mwanamke akiwa na ujauzito wake tayari, tena tumbo unakuta ni kubwa au kuzaa mtoto kwanza ndio ndoa inafungwa, hili swala kiimani limekaaje ni ruhusa au wachungaji/mashehe wanalazimisha?
 
Kama kwa Walutheri ndo imepitishwa kabisa haitakiwi hiyo kitu, Na kiimani kwa hali ya kawaida jamani uzinzi dhambi na chochote baada ya hapo ni uchafu au haramu wakati ndoa ni agano takatifu sasa iwaje ufanye uchafu halafu ukaweke agano takatifu na mbele za Mungu ni hadi toba ifanyike.
 
Kwa sisi wa vijijini enzi zetu tumeshuhudia baba,wajomba,kaka zetu wakiswaga ng'ombe kupeleka kwa wazazi wa wake zao.Baada ya kukabidhiana kilichofuata ni maisha ya ndoa ambayo wengi wetu tunaohangaika na ndoa za kisasa tumezaliwa huko.Kama unawekewa vikwazo sijui na mchungaji nani huko,kwa nini usifanye ya kimila? Maana inatambulika kisheria.Mungu nisamehe sipendi kuongozwa muda wote na akili za wachungaji.
 
Kufunga ndoa bila kuzaa?? Weeeee
Wanaoelewa mtoto wa nje ya ndoa ana status gani hawasubiri mpaka mdada ajifungue... Kuna rafiki yangu alifunga ndoa wakati mimba ina miezi nane... Walienda tu kwa mwenyekiti na gauni lake la kawaida wakafunga ndoa yao na kurudi kufanya kapati ka familia... Aligoma kabisa mtoto wake azaliwe nje ya ndoa
 
Wadau kuna hili swala huwa inatokea mtu anafunga ndoa mwanamke akiwa na ujauzito wake tayari,tena tumbo unakuta ni kubwa au kuzaa mtoto kwanza ndio ndoa inafungwa,hili swala kiimani limekaaje,ni rukhsa au wachungaji/mashehe wanalazimisha?
Yaani hapo unakuwa umeoa wake 2 yaani huyo mama na mtoto aliye ndani, kwa hyo akizaliwa mtoto anakuwa mke wa pili.
 
Wanaoelewa mtoto wa nje ya ndoa ana status gani hawasubiri mpaka mdada ajifungue... Kuna rafiki yangu alifunga ndoa wakati mimba ina miezi nane... Walienda tu kwa mwenyekiti na gauni lake la kawaida wakafunga ndoa yao na kurudi kufanya kapati ka familia... Aligoma kabisa mtoto wake azaliwe nje ya ndoa
Ahaaa kumbe...Lakini pia Mtoto wa nje ya ndoa nae mtoto pia..ijapokuwa kuna wanaowaita haramu na kuwaona hawafai
 
Wanaoelewa mtoto wa nje ya ndoa ana status gani hawasubiri mpaka mdada ajifungue... Kuna rafiki yangu alifunga ndoa wakati mimba ina miezi nane... Walienda tu kwa mwenyekiti na gauni lake la kawaida wakafunga ndoa yao na kurudi kufanya kapati ka familia... Aligoma kabisa mtoto wake azaliwe nje ya ndoa
Mimba inamiezi nane then unajiongopea kwa kufunga ndoa ili mtoto asiwe kazaliwa nje ya ndoa.....Mjini kweli kuzuri.

Hata mimba ikiwa na siku moja bila ndoa ni mtoto wa nje ya ndoa.
 
Imani zote zinakataza bali kwa sasa Imebidi iwe kawaida, watu wanaogopa kuuziwa mbuzi kwenye gunia
 
Hoja ingekuwa kutokula papuchi kabla ya ndoa. Suala la kufunga ndo na ujauzito sio issue maana wengine watoa mimba, wengine wanatumia njia za uzazi wa mpango na wengine wanatumia Tigo kukwepa mimba. Tubaki MABIKIRA HADI NDOA
 
Kwa sisi wa vijijini enzi zetu tumeshuhudia baba,wajomba,kaka zetu wakiswaga ng'ombe kupeleka kwa wazazi wa wake zao.Baada ya kukabidhiana kilichofuata ni maisha ya ndoa ambayo wengi wetu tunaohangaika na ndoa za kisasa tumezaliwa huko.Kama unawekewa vikwazo sijui na mchungaji nani huko,kwa nini usifanye ya kimila? Maana inatambulika kisheria.Mungu nisamehe sipendi kuongozwa muda wote na akili za wachungaji.
Mkuu, kuna watu walijitungia sheria duniani ili kuwa na mamlaka.
Ninachoamini, kuna sheria nyingi za kanisa zilitungwa na wanadamu Kwa maslahi yao.
Hii mambo ya kuambizana dhambi sijui nini na kutishiana ovyo ovyo sidhani Kama ni Mungu kaleta.
 
Back
Top Bottom