Kufukuzwa wanafunzi 2000 mlimani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufukuzwa wanafunzi 2000 mlimani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpambanaji K, Jan 10, 2009.

 1. M

  Mpambanaji K Member

  #1
  Jan 10, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania wenzangu,

  ninaandika hoja yangu huku nikiwa na majonzi tele kuhusu hatima ya elimu yetu Tanzania.

  Inaonekana wazi kuwa viongozi wa chuo na serikali imeamua kwa makusudi watoto wa masikini wasisome Tanzania?nyie mwaonaje?


  Naomba kuuliza wandungu wangu, hivi hatima ya Tanzania inaelekea wapi? ninamaanisha? serikali kutelekeza jukumu lake la kutoa elimu kwa wanannchi wake ni nini?
   
 2. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  You cannot manage students and then you want to manage a country; and the number is only 2000 students; this is alarming; tumerudi wakati ule wa mzee ruksa! give a pill to this problem!
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwandishi alikuwa uchwara hakuna mwanafunzi aliyefukuzwa bali hao wanafunzi 2000 hawajakamilisha mashariti ikiwa ni pamoja na form zao kutofika UDSM. Hata hivyo chuo kimewapa muda hadi Thursday next week. Kwa hiyo wanaowashwa wasubiri hiyo siku.

  Hivyo hadi sasa hakuna tatizo la ku-escalate kuja huku kijiweni... ni mambo ya ndani ya chuo tu bado.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  na pia tujiulize, ni nini jukumu la wazazi/walezi kuwapatia watoto wao elimu?
   
 5. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Ndiyo haya tulikuwa tunaongelea kule kwenye polygamy; wazazi wengi nchi hii wanajua kuzaa na serikali itunze; ni kweli kuwa serikali ni wazembe kiasi kikubwa; lakini wazazi wa Tanzania hata wale wanafunzi (walengwa) hutegemea serikali mno! This issue must be managed otherwise sioni kama tutaendelea hivi kuwa na serikali ambayo inashindwa kusaidia wanafunzi wake; na wazazi wengi ambao hupenda kuzaa na kuto-invest kwa watoto wao.
   
 6. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Interested Observer umekosea kidogo unapo sema wazazi wengine kazi yao ni kuzaa tu wakingojea serikali iwasomeshee. Serikali ni nani?? Inasomeshea pesa za nani??? Ni kodi zetu sote watanzania (direct taxes and inderect taxes). Wao wamepewa jukumu la kukusanya na kupanga matumizi na kusimamia utekelezaji wa matumizi hayo.

  It's our monies full stop.

  Je, serikali isomeshe watoto wa walala hoi, so ifanyie nini hizo pesa???? Iwalipe akina Wakili mkono??? inunulie magari ya kifahari??? Watanulie mawaziri na maofisa wengine wa serikali??? Watajirikie viongozi na maofisa wengine wa serikali ambao baada ya miaka michache ya kazi ya kiutumishi au kisiasa wawe matajiri wa majumba mengi ya kifahari, magari mengi ya kifahari, na mipesa mingi wakaifije akaunti za kigeni kama akina Chenge????

  Pesa yote iliyokwenda Meremeta, Deep green, n.k. isinge wezesha kusomesha watoto kwa kiasi kikubwa????

  Ni kweli kuzaa bila mpango haitatusaidia. Lakini pia hata nchi nyingi zilizo endelea hawajawaachia wazazi tu suala la elimu. Fanya utafiti na utaelewa.
   
 7. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Tukubaliane kweli kabisa serikali yetu ni corrupt, hilo halifichiki; wameshindwa kupanga na kutatua matatizo ya wanafunzi; sawa kabisa. Hata hivyo hayo ni matatizo 50% ya watoto wetu. Another percent ambayo ni 50% vile vile ni ya wazazi at least ku-contribute at least kwenye investment ya watoto wao. Compare na nchi nyingine utaona kuwa at least 80% ya earning za familia zinaenda kwenye investment ya future za watoto wao. Wewe kama umepanga kuzaa watoto watano na unaweza kuwatunza watoto wawili je utegemee nani akutunzie hao watatu?
   
 8. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Nyerere wakati anawasomesha watanzania bure wakati ule zile pesa alikuwa anazitoa wapi?
  Nsololi umeeleza vizuri kabisa na nakubaliana nawe.Kama elimu ingekuwa priority ya serikali yetu basi hakuna mwanafunzi angeachwa.Pesa ipo isipokuwa inatumika katika vipaumbele hasi.
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mtarajiwa ;

  Ifuatayo ni jibu la swali lako!

  1. Inawezekana sana kusomesha watu hadi University bure... ingawa bure yenyewe inategemea unaangalia kutoka engo gani?
  *Vijana waliovijiweni wakifanya kazi wote au at least 75% na kuzalishia taifa, alafu wakajisikia wazalendo na wakalipa kodi ​
  *Wenye majumba ya kukodisha wakilipa kodi​
  *Wenye biashara wakalipa kodi kwa kiwango kile kile ambacho mfanyakazi analipa​
  *Wafanyakazi wa serikalini wakaondoa marurupu yasiokatwa kodi, badala yake yawekwe kwenye mishahara na kukatwa kodi​
  *Kwa ujumla wetu tukibalika tukaona fahari kulipa kodi sio sasa asiyelipa kodi ndiye shujaa​
  Tutaweza kufanya mengi.

  2. Namna ya pili kodi zisilipwe kama ilivyo sasa na kila mtu abebe mzigowake mwenyewe. rejea msemo wa . C.D. Msuya. yaani mkusanye kodi kidogo, hivyo hamuwezi kutoa huduma za kijamii... ati ukipiga mkwara record za ukusanyaji zinapanda... ukitulia ukasanyaji kodi unakuwa wa chini... taifa gani hili?

  Nyerere alitumia ya njia ya 1.... kumbuka kulikuwa na kodi ya maendeleo pia na wananchi walikuwa wakilipa... Mashirika na viwanda vilikuwa vikilipa kodi

  Siku hizi kuna mtu hajui kodi ni nini? ati kuna wanasamehewa 100%..kisa mishahara yao ni chini ya 100,000/-. that is wrong! kodi inatakiwa akatwe kila mtu hata kama itakuwa kama token tu... inabidi aelewe kwamba kuna kitu kinaitwa kodi.


  Sisi tunatumia hiyo njia ya 2.
   
 10. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kasheshe japo maelezo yako ni mazuri lakini bado sikupati mkuu.Una maana Nyerere alikuwa anakusanya kodi vizuri au kipindi cha Nyerere watanzania walikuwa wanalipa vizuri kodi kuliko sasa ndiyo maana Nyerere aliweza kuwasomesha bure?Lakini mbona kuna hotuba moja ya Nyerere niliona anahimiza serikali(ya Mkapa) nadhani kuacha kuogopa kukopa kwani hata mataifa makubwa yanakopa.Akasema lengo la kukopa ni kuwaondolea wananchi umaskini siyo kwa kuwagawia zile pesa za mkopo bali kuwasomeshea watoto zao.Akasema hata yeye kipindi chake alikopa sana ndiyo maana aliwasomesha kina Mkapa hao.
  Sasa mkuu,maswali yangu ni je-ina maana sasa hivi serikali yetu haikopi huko WB sijui IMF?Kama inakopa hizo pesa inafanyia nini?Ina maana serikali yetu sasa haipati tena misaada kutoka kwa wahisani?Kama inapata hizo pesa inafanyia nini?Ina maana sasa serikali yetu haikusanyi kodi,ni masikini kabisa haina pesa?Kama haina zile pesa za kununulia ule utitiri wa mashangingi zinatoka wapi?Zile pesa za Pinda za kubailout TRA sijui zinatoka wapi?Siyo kwamba pesa ipo lakini inatumika ndivyo sivyo mkuu?
   
  Last edited: Jan 12, 2009
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Jan 12, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nilichokiona juu ya wanafunzi hao 2000 ni wenyewe kuamua ama kwa kutaka au kwa bahati mbaya kutoendelea na chuo.Walitangaza mtu ambaye hatajaza form atakuwa amejiondolea haki ya kusoma pale. hawa hawakujaza so wameamua kutoendelea na chuo. Waliopewa musa mpaka alhamisi ni waliojaza lakini hawakulipa ada yote wanayodaiwa. still inaonyesha nchi yetu elimu ni kwa walionacho.
   
 12. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Msisahau uchangiaji wa elimu, afya,nk. ni moja ya sera zilizolazimishwa na IMF na WB. Lengo ni baki kubwa ya mapato ya serikali yaelekezwe kwenye ulipaji wa madeni ya nje na kulipia miradi inayowanufaisha *wawekezaji* kama TICTS, Richmond, na mengine. Bila uchangiaji hawa wateule hawawezi kulipwa. Ndiyo wanaopewa kipaumbele cha kwanza.

  Kwa kweli uchangaiji ni double taxation. Hizo pesa za serikali ni kodi yetu. Hata kama serikali itakopa bado ni sisi hatimaye tutakaolipa hiyo mikopo. Huwezi kulinganisha uchangiaji wa mzazi wa Kimarekani au Mwingereza na huu wa Kitanzania. Hizi ni dunia mbili tofauti zanazohitaji mbinu tofauti. Wazazi wa Kitanzania siyo wazembe. Wengine hata mtoto mmoja hawawezi kummudu.
   
 13. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuseme kuwa Serikali hii imeshindwa majukumu; haijui inachokifanya;na kilichopo inafanya uhuni na ulaghai dhidi ya WATZ; ni barabara zipi zimejengwa mpaka wanachuo wasisome; afya je hamna kitu ahadi tu;ni madarasa yapi (kama sio michango ya wananchi tena), ni maisha bora yapi yamepatikana mpaka wanachuo wasisome; ni mtandao upi wa maji umepatikana mpaka wanachuo wasisome; ni matrekta yapi yamenunuliwa mpaka leo hii useme wanafunzi wasisome; ni nyumba zipi zimejengwa mpaka useme sasa serikali imemaliza hela; ni nini kimefanywa sasa tuseme basi kweli serikali isamehewe kwa wanafunzi wa chuo? Wizi mtupu; wananchi hawajui pia walifanyalo; kwa nin hawaulizi kodi zao zinaenda wapi? kwa nini hawaulizi maongezeko ya kodi yanasaidia nini; bila wafadhili kwa sababu ya ufisadi hamna mradi unaweza kuendelea; magari ya kifahari na ufisadi kibao unafanywa kwa nini tusiombe mabadiliko; what is Bill 17 kwa wanafunzi kama mnaweza kununuaa generator ya Bill kibao ( Richmonduli); Wizi mtupu; lazima wananchi wajitolee mhanga la sivyo ipo siku taifa letu litaangamia maana watu wameweweseka ingawa barabarani ukimkuta anasema mambo safi; what is mambo safi wakati huna uhakika na week mbili zijazo kama utaishi? why? kwa nini; najua ahadi ni wakati wa uchaguzi na uchaguzi ukiisha yanakuwa matendo why this
   
 14. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MMHH analyse and get fact before you say this serious thing; wamekuambia ujaze ukiwa na list ya laki nne; kama ukikosa laki nne utajaza form ya nini; na usipojza je ndio umejiondooa au masharti ndio y amekuondoa; kumbuka walichokigomea ndio bado hakijapatiwa majibu na zaidi wanakiongezea ukali; mie nalipa hela ya mkopo wa chuo na nimesomeshwa full payment; sioni tatizo lakini kwa nini hela yangu isisaidie hawa wadogo zangu; Je serikali ikikosa hicho kiasi kidogo cha hela bado tuiite serikali au tuotafutie jina- Mtanzania halisi lazima aguswe na udhalimu ni hasira za walala hoi wasioweza kupiga kelele kwa shida zao
   
 15. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tatizo letu ni kuwa kila kitu kinachofanywa na serikali tunailaumu bila kujali au kungalia sababu za msingi za kufanya kitu cha aina hiyo. kama waliambiwa wajaze form na hawakujaza then nani alaumiwe serikali au wao kwa kuescarate mgogoro usiokuwa na msingi.
  sera sio kitu cha kuchange siku moja it need a deep analysis before making a decision, keki ya taifa ni ndogo ukiamua kumpa mmoja wapo inabidi unyanganye mwingine, put aside mambo ya ufisadi kwani yanaitaji muda kufanyiwa kazi je immediate measure ni nini ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao bila mgomo.
  hatuhitaji malaika kutoka mbiguni kuja kuiongoza tanzania, tutoe malalamiko yetu na kuacha serikali iyafanyie kazi kwa taratibu zilizowekwa na sio kuamua kuilazimisha kwa migomo na vitu vingine ambavyo costs yake kwa mtoto wa masikini ni kubwa sana.
  pesa waliyotumia kukaa guest wakati wamefukuzwa au kwa ndugu au nauri za kurudi kwao wangeweza kupunguza madai ya chuo na kuomba nao wapewe muda zaidi kumalizia wakati viongozi wao wakiwa wanalishughulikia kwa ustaarabu.
   
 16. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wandugu Suala la kodi kwa kweli linahitaji wanauchumi waliokomaa. Tanzania inakusanya kodi kwa wanyonge tu, kule kijijini balozi na mgambo shina wanakamata mbuzi, bata na kuku kisa mwananchi ameshindwa kulipa cash. Muulize huyo kiongozi washina hao wanyama wanakwenda WAPI? ni kitoweo chake na mafisadi wenzake. Ninachotaka kuchangia hapa ni kwamba; Watanzania wanalipa kodi katika ngazi tofauti tofauti. Kodi hizo zinaishia mikononi mwa mafisadi. Tunao mafisadi wa kila level. Wakumhurumia ni huyo mwananchi wa chini ambaye kuku wake amekamatwa na kiongozi wa shina kisa hana Cash. Leo unamwambia alipie mtoto wake chuo inawezekanaje??? Tanzania haikujiandaa kuwandaa wananchi wake kujilipia gharama za shule. Ukimfukuza chuo huyo kijana/binti sasa, serikali haiondokani na tatizo inazidi kukuza tatizo. Wezi wataongezeka ambao wanalihujumu taifa hata kwa ufisadi. Watoto wa wazazi wasio na elimu na watoto wa mitaani wataongezeka. The feedback will go back to the Government of Tanzania na wananchi wote. Je Tanzania imejiandaa kupambana na ufisadi utakaoletwa na hilo kundi litakalofukuzwa chuo na vizazi vyake?? Yangu hayo tu.
   
 17. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Cutting off your nose to spite your face!
   
 19. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Date::1/14/2009
  Daruso yafutwa, sheria mpya UDSM zatangazwa
  Latifa Karugila na Hussein Kauli

  CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeweka masharti magumu ya kudhibiti usajili wa wanafunzi waliodahiliwa upya kuingia chuoni hapo kuanzia Januari 19, mwaka huu.

  Vile vile, kimetangaza rasmi kufutwa kwa sheria za chuo zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Daruso).

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Makamu Mkuu wa chuo (Taaluma), Profesa Makenya Maboko, ilionyesha kuwa wanafunzi wote watakaotimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo, watapewa vitambulisho vipya pamoja na taratibu za namna ya kuishi chuoni hapo.

  Profesa Maboko alieleza kwenye taarifa hiyo kuwa, mwanafunzi atakayekutwa ndani ya chuo bila ya kuvaa kitambulisho atakuwa amesababisha uvunjifu wa amani na utulivu, hivyo atachukuliwa hatua za kisheria juu ya kitendo hicho.

  "Wanafunzi watakaokuwa wamevaa vitambulisho hivyo ndio watakaoruhusiwa kuingia darasani," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

  Ili kutekeleza masharti hayo, Profesa Maboko alisisitiza kuwa kila mwanafunzi atakayekamilisha taratibu za usajili atapaswa kupatiwa kitambulisho kipya, vinginevyo hatatambuliwa kama mwanafunzi aliyetimiza vigezo vya kujiunga tena na chuo.

  Akizungumzia kuhusu Serikali ya Wanafunzi wa UDSM (Daruso), Profesa Maboko alisema taasisi zote za wanafunzi zilizokuwa zikitambuliwa na sheria ya chuo ya mwaka 2007, kabla ya kusimamishwa kwao, hazitatambuliwa tena.

  Alisema taasisi hizo zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho.

  "Taasisi mpya za wanafunzi zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho," aliongeza Profesa Maboko.

  Wanafunzi waliosajiliwa upya watatakiwa kuripoti chuoni hapo kuanzia Januari 19 hadi 22, mwaka huu, kwa utaratibu maalumu uliotolewa na chuo.

  Source: Mwananchi
   
 20. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2009
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nashukuru sana kwa kutupatia fursa hii tuweze kutoa mchango wetu kuhusiana na hili. Mimi ninadhani hawa viongozi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wachunguzwe uraia wao. Mimi nina wasi wasi na uraia wao kwa sababu kwa mtazamo wa kawaida haiwezekani adhabu iwakumbe vijana wengi kiasi hicho. Hii ina maanisha hawakuwa makini katika kubaini chanzo halisi cha migomo. Kwa hakika ni mbinu ya kuiangamiza Tanzania kielimu. Tungependa wadau mbali mbali waingilie kati suala hili maana si jema kwa Tanzania hii ya sasa.

  Adhabu waliyopewa vijana hawa ilitosha tu kule kusimama masomo kwa kipindi chote hiki lakini kwa idadi hii kulipuliwa hivi ni sawa na maangamizi wanayofanyiwa Wapalestina kule Ukanda wa Gaza.

  Tungependa vyama mbali mbali vya siasa kulipigia kelele suala hili tuweze kujua vyama hivi viko makini katika kuliandaa taifa la baadaye lenye wasomi watakao iendesha Tanzania hapo baadaye katika ushindani huu wa soko huria. This issue is not POLITICAL is about NATIONAL STRATEGY for the FUTURE. VYAMA VYOTE UNGANENI KUPINGA HILI. Haliko katika ilani ya chama chochote kwanini nyie vyama msikemee???

  We can not imagine such professors beeing agents of killing their fellow Tanzanians. I doubt the level of education they have and the decision they use to make.
   
  Last edited: Jan 15, 2009
Loading...