Kufeli shuleni sio kufeli maisha

Assalafiyyu

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
1,799
2,000
Kama haya ndio yanayosomwa...kwa sababu hayaakisi maisha halisi wala hayagusi changamoto zake na kuzitatua...

Sasa nimsome Panzi na kuweka kichwani parts zake zote ili iweje...

Hebu tuambieni mliomeza haya mavitu...yamewasaidia nini kujikwamua na hali mbaya ya Jiwe...

Hili lielimu letu liangalie mambo ya msingi ya kusoma...kuanzia ya msingi...mtu atoke na fani yake kabisa itakayomsaidia na kupambana na changamoto za kimazingira...

Wizara ya elimu...sijui hayo maprofesa ugali tu...vitambi vimewajaa tu bila kuwa na mawazo mbadala...

Lets change our mindset...

Leo mtoto aliyemaliza form four akafeli akarudi mtaani...hajui what to do kabisa...kwa ajili ya kuwamezesha utumbo utumbo kama huu...

UKIONA MWANAO AU NDUGU YAKO KAFELI FORM FOUR...BASI USIHUZUNIKE...NI KWA SABABU WANAMEZESHWA UTUMBO KAMA HUU...NA UUMPE PONGEZI KUWA AKILI YAKE IMEJUA KUNG'AMUA IKAONA SIO MUHIMU KUHIFADHI UTUMBO KAMA HUO...
IMG_20190310_074340.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
abdi ally

JF-Expert Member
Dec 4, 2018
1,568
2,000
Kama haya ndio yanayosomwa...kwa sababu hayaakisi maisha halisi wala hayagusi changamoto zake na kuzitatua...

Sasa nimsome Panzi na kuweka kichwani parts zake zote ili iweje...

Hebu tuambieni mliomeza haya mavitu...yamewasaidia nini kujikwamua na hali mbaya ya Jiwe...

Hili lielimu letu liangalie mambo ya msingi ya kusoma...kuanzia ya msingi...mtu atoke na fani yake kabisa itakayomsaidia na kupambana na changamoto za kimazingira...

Wizara ya elimu...sijui hayo maprofesa ugali tu...vitambi vimewajaa tu bila kuwa na mawazo mbadala...

Lets change our mindset...

Leo mtoto aliyemaliza form four akafeli akarudi mtaani...hajui what to do kabisa...kwa ajili ya kuwamezesha utumbo utumbo kama huu...

UKIONA MWANAO AU NDUGU YAKO KAFELI FORM FOUR...BASI USIHUZUNIKE...NI KWA SABABU WANAMEZESHWA UTUMBO KAMA HUU...NA UUMPE PONGEZI KUWA AKILI YAKE IMEJUA KUNG'AMUA IKAONA SIO MUHIMU KUHIFADHI UTUMBO KAMA HUO... View attachment 1042077

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hongera kuwa na wazo fikirishi japo wapumbavu watakupinga juu ya hilo
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,399
2,000
Changamoto za maisha sio changamoto za kiuchumi pekee! Mtu mwenye elimu anakuwa na upeo mkubwa zaidi wa kuchanganua mambo yanayomzunguka mwanadamu kwa usahihi...
 
Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
4,524
2,000
Wewe unayejitambua...umetambua nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimetambua kuwa hujielewi japo wew ni baba wa mke na watoto

Hivi mtoto kujua sehemu ya mwili wa binadamu na wadudu na jinsi zinazofanya kazi havimsaiidi

Hivi hesabu wanazosoma hazisaidii

Historia za mashujaa na marais waliyokuwa wanafanya nyuma kusoma madarasani hayawasaidii ,

Shuleni wanajifunza mambo mengi zaidi ujuavyo, wanaongeza knowledge na uwezo wa kufikili kuliko wew kiazi unavowazaa

Yaani huo utumbo umeoandika ufiche unajiaibisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,399
2,000
Elimu ya kuchora panzi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hicho ni kisehemu kidogo cha elimu. Piga picha elimu inaanzia shule ya msingi, miaka saba, sekondari ya kawaida miaka minne, sekondari ya juu miaka miwili. Jumla hadi hapo ni miaka 13. Ukienda chuo tena miaka mitatu, jumla ni miaka 16. Huwezi tu ukawa unachora panzi miaka yote 16. Kama ungekuwa umesoma, ungeelewa ni mambo gani yanayofundishwa huko shule. Kama hukupata bahati ya kusoma, pole sana. Ila hakiisha unawapeleka watoto wako shule. You never know, huenda elimu ikawatoa...
 
ArchAngel

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
4,461
2,000
Wanaotegemea mshahara kusurvive hawatakuelewa mleta mada.

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,193
2,000
Kweli hii elimu ya kipumbavu sana tunayopewa bongo,weee unanifundisha mambo ya banseni bana yanisaidie nini kwa nini usinifundishe namna ya kutengeneza kitanda,nakumbuka kipindi tunasoma kuna somo likiitwa sayansi kimu na mambo ya stadi za kazi yale masomo yalikua yanafunzishwa kwa practical jinsi ya kupika,kufua,kunyoosha,uchongaji,uchoraji yani kama ule mfumo ungeendelea hadi sasa watoto wengi wangekua wanamaliza primary tayari wana fani zao za kujiajiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nicklaus

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
322
500
Kama haya ndio yanayosomwa...kwa sababu hayaakisi maisha halisi wala hayagusi changamoto zake na kuzitatua...

Sasa nimsome Panzi na kuweka kichwani parts zake zote ili iweje...

Hebu tuambieni mliomeza haya mavitu...yamewasaidia nini kujikwamua na hali mbaya ya Jiwe...

Hili lielimu letu liangalie mambo ya msingi ya kusoma...kuanzia ya msingi...mtu atoke na fani yake kabisa itakayomsaidia na kupambana na changamoto za kimazingira...

Wizara ya elimu...sijui hayo maprofesa ugali tu...vitambi vimewajaa tu bila kuwa na mawazo mbadala...

Lets change our mindset...

Leo mtoto aliyemaliza form four akafeli akarudi mtaani...hajui what to do kabisa...kwa ajili ya kuwamezesha utumbo utumbo kama huu...

UKIONA MWANAO AU NDUGU YAKO KAFELI FORM FOUR...BASI USIHUZUNIKE...NI KWA SABABU WANAMEZESHWA UTUMBO KAMA HUU...NA UUMPE PONGEZI KUWA AKILI YAKE IMEJUA KUNG'AMUA IKAONA SIO MUHIMU KUHIFADHI UTUMBO KAMA HUO... View attachment 1042077

Sent using Jamii Forums mobile app
Endelea kulaumu wakati wenzako walijitoa na kumeza huyu panzi saa hivi wanakula hela pasi na jasho kushndwa umeshindwa ww wengine wana enjoy tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
792
1,000
Kilimo ni Uti wa mgongo,cha kusikitisha hata vijijini wanapotegemea kilimo shule za kata hazifundishi somo la kilimo,Division four na Zero zimekuwa nyingi,kwa kufundisha masomo ya kilimo ingesaidia kundi hili kubwa la wanaoferi kuanzisha miradi ya kilimo na kujikomboa na maisha.Inasikitisha form four wa Bush hajui hata kupanda maharage au mahindi kisasa,hajui lolote kuhusu kilimo cha kisasa.
Serikali inayoelekea kwenye Viwanda/Uchumi wa kati ingepata malighafi nyingi kutoka kwa wanaoshindwa kuendelea na kidato cha tano n.k
Mitaala ibadilishwe,wizara imulike practical skills/vocational trainings kuanzia levo ya msingi,sekondari mpk vyuoni itolewe ili kutoa elimu mbadala ya kukabiliana na maisha,sio hii elimu inayotengeneza walalamikaji mitandaoni na wasubiria ajira...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CSF

Member
Sep 4, 2018
86
125
Umekuwa na mwendelezo wa kuleta maada kuhusu elimu na mfumo wa elimu kwa ujumla wake . kuna thread unasema advance haina faida ni upotezaji wa mda tuu ,hapa pia unalalamikia kuhusu panzi na vitu kama hivyo ,,,,unaonekana ni victim was mfumo huu japo haujalisema hili direct ,,,,mengine ambayo huyajui wewe hayaondoi maana katika jamii na panzi na mbu wataendelea kufundishwa tuu mpaka level ya chuo kama unataka kujua umuhimu wa kujua vitu bora uwe unauliza sio unaclash moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baijukya

Member
Jun 8, 2018
10
45
Ndugu tunakuomba usirudie kuleta thread kama hizi huku kama mpaka sasa haujatambua mchango wa madakitari mpaka sasa kwenye jamii pamoja na walimu bora utulie tu. Sayansi sio ya kuchezea hivyo ndugu aisee kwa mfano kupitia hao insects tunaweza kujua various methods of pest control (njia mbalimbali za kuzuia wadudu wasiathiri mazao yetu) ambayo ni maisha ya kila siku kukutana na hao wadudu mashambani kwetu. Pia kupitia hawa wadudu ndo tunapata asali ambapo pia inachangia kiuchumi so bila kusoma insects kwa ujumla ukabakia kuchora mchoro tu basi hautaelewa maana halisi nacho kuomba kama umemaliza form six bila kuongeza kozi yoyote nenda kamalizie kozi alafu ndo urudi huku aisee
Kama haya ndio yanayosomwa...kwa sababu hayaakisi maisha halisi wala hayagusi changamoto zake na kuzitatua...

Sasa nimsome Panzi na kuweka kichwani parts zake zote ili iweje...

Hebu tuambieni mliomeza haya mavitu...yamewasaidia nini kujikwamua na hali mbaya ya Jiwe...

Hili lielimu letu liangalie mambo ya msingi ya kusoma...kuanzia ya msingi...mtu atoke na fani yake kabisa itakayomsaidia na kupambana na changamoto za kimazingira...

Wizara ya elimu...sijui hayo maprofesa ugali tu...vitambi vimewajaa tu bila kuwa na mawazo mbadala...

Lets change our mindset...

Leo mtoto aliyemaliza form four akafeli akarudi mtaani...hajui what to do kabisa...kwa ajili ya kuwamezesha utumbo utumbo kama huu...

UKIONA MWANAO AU NDUGU YAKO KAFELI FORM FOUR...BASI USIHUZUNIKE...NI KWA SABABU WANAMEZESHWA UTUMBO KAMA HUU...NA UUMPE PONGEZI KUWA AKILI YAKE IMEJUA KUNG'AMUA IKAONA SIO MUHIMU KUHIFADHI UTUMBO KAMA HUO... View attachment 1042077

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom