Elimu ya kuchora panzi...
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ni kweli tunahitaji mageuzi katika mfumo wa elimu.
Mapungufu yake ni kwamba hayamuelekezi huyu aliyefeli aende wapi ?
Si kweli kumchora panzi hakuna manufaa katika elimu, hapana manufaa yapo.
Ila manufaa yake utayaona utakapoenda taasisi za elimu ya juu
Mfano kiumbe yeyote yule katika tafiti za kisayansi anaweza kuwa kiumbe mwenye kuwabeba viumbe wanaofanyiwa tafiti walio wadogo kuliko yeye (host organism) atakayetumika katika kuwakuza viumbe chini ya utafiti.
Kujua sehemu zao na tabia zake na hormoni zao ni kujua mahala ni wapi viumbe walioko katika utafiti waingizwe (injected)
Nimeongelea eneo moja tu juu ya kwa nini ni muhimu kuwafahamu viumbe hawa.
Nitatoa mfano kidogo tafiti nyingi za kiafya kwenye masuala ya kinga na tiba yalianzia kwa wanyama mfano;-
Nguruwe - hormone ya insulin
Bacteria - tafiti za virusi na chanjo.
Shida siyo nini faida ya kumchora panzi tatizo ya elimu ya tanzania ni kwamba;-
1. Huko chini inatoa basic general knowldge ambayo huwezi kujua unvyovisoma vina faida ipi kwa wakati huo ila mpaka ukifika mwisho.
2. Elimu hii inaamini kila mtu atafaulu hakuna atakaye feli. Hivyo ukifika juu utajua zaidi faida ya unayoyasoma
3. Haijamuandalia huyu anayefeli pa kwenda.
Haijui hata kama kafeli kwamba anaweza akawa trained kushikilia kazi za mikono mfano
1. kuunda vyungu
2. Kufuga kuku
3. Kulima bustani
4. Kuchakata ngozi za wanyama na kutengeneza viatu.
5. Kuunda makampuni ya kutoa huduma za kijamii mfano mapambo harusini, kutengeneza mapambo, mataji
N.k
Ili wavifanye kwa viwango vikubwa ili kuleta tija na kujikidhi kimaisha.
Hawa waliofeli mitihani wanayaweza haya.
Mchango wangu wizara ya elimu iweke muongozo kwa anayefeli akapate elimu hizi za ujasilia mali na kujikimu
Sent using
Jamii Forums mobile app