Hivi unajua mwalimu wa Serikali wanavyonyanyaswa kupata haki zake,? Hivi unategemea darasani atafundisha akiwa na saikolojikale nzuri? Nyumbani kuko hivyo,Anaidai serikali haitaki kumlipa, Madaraja haimpandishi kwa wakati na wakati mwingine yanapandishwa kwa upendeleo, Mfano ninao ushahidi wa waalimu watatu shule ya kijijini waliajiliwa 2011 Hadi sasa hawajawahi kupanda daraja, Hawana kesi yoyote na wanafanya kazi izuri lakini hawathaminiwi,Sasa unamtaka Mkuu wa shule awasimamie nini? Waliopo halmashauri kutwa nzima wapo kwenye vikao visivyoisha tena vyenye kulipana posho, Je ni lini waalimu wamefanya vikao shuleni kwao wakajilipa posho? Polisi kila tarehe 15 Anapewa Ration ya chakula, 400000, Mwalimu kila tar 15 Anapewa nini? Acha kuropoka, Funga mdomo kama hujui chanzo cha tatizo