Kufanyia Mikutano kila mara IKULU kuna faida au hasara gani ya Kiusalama?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Sasa ni muda mrefu nimekuwa nikiona Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli akifanya Vikao vyake au Mikutano yake mingi tena ile mizito na ya Serikali kutokea IKULU na naona sasa imeshazoeleka na si ajabu hata ambao huwa wanaalikwa kuhudhuria huko tayari wameshajua kona zote za IKULU na si ajabu wameshazoeana pia na hata wale Ndege wazuri Tausi na Watu wengineo pale.

Naomba kuwaulizeni Wajuvi / Wabobezi ( Pundits ) wa masuala haya ya Ulinzi na Usalama je huku kuendelea kwa Rais kufanya Mikutano / Vikao vyake pale IKULU kuna faida gani au hasara gani hasa ya Kiusalama?

Naomba kuwasilisha na nitashukuru nikielimishwa nanyi Wataalam mliotukuka.
 
Haina tatizo bali ni salama zaidi kwa sababu kule kuna ulinzi wa hali juu, pia inaokoa pesa ambazo zingelipwa hotelini kama ingefanyika huko.
 
Haina tatizo

Kuna waliobarikiwa na kuwa na macho ya Kijasusi ambayo yakiangalia tu sehemu mara moja basi huweza kujua taswira nzima ya eneo zima hivyo ikawa si salama kwa eneo husika. Hivi wote wanaoalikwa pale tunawajua vizuri au tuna uhakika nao hasa ya Kiuzalendo kwa nchi yetu hii hasa ukizingatia kwamba karibia 75% ya Watanzania wengi Kihistoria siyo Raia kamili na pengine labda wanaweza kutumika bila Mamlaka kujua?

Ni mtazamo wangu tu lakini ila binafsi nikiulizwa kama hili jambo la Mkuu wa nchi kupendelea kufanya Mikutano yake pale IKULU ni jema nitapingana nalo kwani sidhani kama IKULU kunapashwa kuzoeleka hivyo kwa Watu kila mara kuja na kuondoka na ninavyosikia Wabobezi wenyewe wa haya Masuala wanasema kuwa moja ya Principle yao kubwa ni kutomuamini yoyote yule sasa hawa Wageni wanaoingia pale katika Vikao / Mikutano wanawaamini vipi?
 
Kupunguza matumizi yasiyo yalazima

Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuwapa Watu fursa ya kuzidi kuzoea maeneo ya IKULU ambayo naamini ndiyo sehemu NYETI namba moja nchini ipi ina afadhali au faida Mkuu?
 
Ingekuwa kuna tatizo wataalam wa masuala ya usalama wangeona tangu mwanzo na ukumbi wa mikutano usingejengwa ikulu.
 
Kuna waliobarikiwa na kuwa na macho ya Kijasusi ambayo yakiangalia tu sehemu mara moja basi huweza kujua taswira nzima ya eneo zima hivyo ikawa si salama kwa eneo husika. Hivi wote wanaoalikwa pale tunawajua vizuri au tuna uhakika nao hasa ya Kiuzalendo kwa nchi yetu hii hasa ukizingatia kwamba karibia 75% ya Watanzania wengi Kihistoria siyo Raia kamili na pengine labda wanaweza kutumika bila Mamlaka kujua?

Ni mtazamo wangu tu lakini ila binafsi nikiulizwa kama hili jambo la Mkuu wa nchi kupendelea kufanya Mikutano yake pale IKULU ni jema nitapingana nalo kwani sidhani kama IKULU kunapashwa kuzoeleka hivyo kwa Watu kila mara kuja na kuondoka na ninavyosikia Wabobezi wenyewe wa haya Masuala wanasema kuwa moja ya Principle yao kubwa ni kutomuamini yoyote yule sasa hawa Wageni wanaoingia pale katika Vikao / Mikutano wanawaamini vipi?
Watu wengine mmebarikiwa,umechambuavizuri sana,lakini kuna manyang'au hawataelewa kabisa ulichokusudia.
 
Ingekuwa kuna tatizo wataalam wa masuala ya usalama wangeona tangu mwanzo na ukumbi wa mikutano usingejengwa ikulu.

Mbona nchi za Wenzetu ambazo ni kubwa, tajiri na zina kila aina ya Uimara wa Kiusalama lakini Viongozi wao Wakuu wa hizo nchi zao hawafanyi hivi kama hapa Kwetu Tanzania lakini hili jambo mbona halikuwepo katika awamu zingine nne ( 4 ) zilizotangulia? Je hao waliopita hapo hawakuona huo umuhimu ambao umeonekana sasa?

Mimi siliafiki kabisa tena kwa 100%.
 
Kuna waliobarikiwa na kuwa na macho ya Kijasusi ambayo yakiangalia tu sehemu mara moja basi huweza kujua taswira nzima ya eneo zima hivyo ikawa si salama kwa eneo husika. Hivi wote wanaoalikwa pale tunawajua vizuri au tuna uhakika nao hasa ya Kiuzalendo kwa nchi yetu hii hasa ukizingatia kwamba karibia 75% ya Watanzania wengi Kihistoria siyo Raia kamili na pengine labda wanaweza kutumika bila Mamlaka kujua?

Ni mtazamo wangu tu lakini ila binafsi nikiulizwa kama hili jambo la Mkuu wa nchi kupendelea kufanya Mikutano yake pale IKULU ni jema nitapingana nalo kwani sidhani kama IKULU kunapashwa kuzoeleka hivyo kwa Watu kila mara kuja na kuondoka na ninavyosikia Wabobezi wenyewe wa haya Masuala wanasema kuwa moja ya Principle yao kubwa ni kutomuamini yoyote yule sasa hawa Wageni wanaoingia pale katika Vikao / Mikutano wanawaamini vipi?
Katika ulimwengu wa sasa hivi wa sayansi na Tekinolojia ukizingatia kuwa unanunua kila kitu kutoka nje, unawezaji kujilinda kwa kujifungia ndani na kuzuia watu kuona makazi yako, unaweza kukuta hata nguo, miwani, kiatu saa au kifungo cha nguo yako kinapiga picha na kukusanya maneno yote unayoongea na kuyatuma kwa mtu anayezihitaji.
 
Hilo swala ni nyeti sana , maana kiintelijensia hakuna kuaminiana sana .
Ila mimi ningeona ni vema kuwa na ikulu ndogo kama Marekani walivyo
na Ikulu yao ndogo almaalufu kama 'Camp David".
ili mambo kama hayo ya mikutano basi yafanyikie huko na sio white house yetu.
Camp David has been used extensively to host foreign dignitaries.
 
Ingekuwa kuna tatizo wataalam wa masuala ya usalama wangeona tangu mwanzo na ukumbi wa mikutano usingejengwa ikulu.
Kujengwa ukumbi wa mikutano ikulu ndo sababu ya kupafanya pale pawe kama Serena??

Kuna waliobarikiwa na kuwa na macho ya Kijasusi ambayo yakiangalia tu sehemu mara moja basi huweza kujua taswira nzima ya eneo zima hivyo ikawa si salama kwa eneo husika. Hivi wote wanaoalikwa pale tunawajua vizuri au tuna uhakika nao hasa ya Kiuzalendo kwa nchi yetu hii hasa ukizingatia kwamba karibia 75% ya Watanzania wengi Kihistoria siyo Raia kamili na pengine labda wanaweza kutumika bila Mamlaka kujua?

Ni mtazamo wangu tu lakini ila binafsi nikiulizwa kama hili jambo la Mkuu wa nchi kupendelea kufanya Mikutano yake pale IKULU ni jema nitapingana nalo kwani sidhani kama IKULU kunapashwa kuzoeleka hivyo kwa Watu kila mara kuja na kuondoka na ninavyosikia Wabobezi wenyewe wa haya Masuala wanasema kuwa moja ya Principle yao kubwa ni kutomuamini yoyote yule sasa hawa Wageni wanaoingia pale katika Vikao / Mikutano wanawaamini vipi?
 
Wageni wenyewe muda wowote wanategemea kutumbuliwa na hawakopesheki inamaanisha position zao sio dhamana tena, Rahisi sana kutumiwa na magaidi au majasusi
 
Mbona nchi za Wenzetu ambazo ni kubwa, tajiri na zina kila aina ya Uimara wa Kiusalama lakini Viongozi wao Wakuu wa hizo nchi zao hawafanyi hivi kama hapa Kwetu Tanzania lakini hili jambo mbona halikuwepo katika awamu zingine nne ( 4 ) zilizotangulia? Je hao waliopita hapo hawakuona huo umuhimu ambao umeonekana sasa?

Mimi siliafiki kabisa tena kwa 100%.
Serikali ya Washington huwa inafanya most of the press conferences ikulu yake...

By the way mkuu kama wapo watu/kikundi cha watu wenye nia ovu hara hawahitaji kuingia sana ikulu kufanya yao...huwa wanapandikiza mamluki wa kijasusi (anaweza hata akamwa mke au mtoto wa rais)
 
Mbona nchi za Wenzetu ambazo ni kubwa, tajiri na zina kila aina ya Uimara wa Kiusalama lakini Viongozi wao Wakuu wa hizo nchi zao hawafanyi hivi kama hapa Kwetu Tanzania lakini hili jambo mbona halikuwepo katika awamu zingine nne ( 4 ) zilizotangulia? Je hao waliopita hapo hawakuona huo umuhimu ambao umeonekana sasa?

Mimi siliafiki kabisa tena kwa 100%.

Mkuu tena huko nchi za wenzetu ndo kabisa. Whitehouse kwa Trump ndio mpaka kuna ofisi ya waandishi wa habari wako hapo 24/7 na bado kuna ile gallery ya briefing ya waandishi wa habari(Daily Briefing) za Spicer pia kuna tour kabisa za kutalii ikulu kwa wananchi wa kawaida,watoto/wanafunzi

Nadhani ushauri wako ni mzuri na pia nadhani kuna restricted areas ambazo watu hawafiki. Wazee wa njiwa kwenye tawi watakua wamepata ushauri wako kudhibiti watu wasiohusika kufika maeneo nyeti
 
hatari ni kubwa sana jana wasanii wengi waliingia ikulu as if wameenda studio kurekodi nyimbo
 
Back
Top Bottom