Kufanya Biashara na Taasisi ni changamoto sana

Kufanya Biashara na Taasisi ni changamoto sana

kuna jamaa pale mapinga aliwauzia wachina matofali ya kutosha.
Anakwenda kudai hela wachina wamemaliza kazi wameondoka
Amefilisika mpaka leo
 
Tafuta wakili uishtaki serikali maana kinachoendelea sasa hivi ni full uhuni na upigaji.
 
kuna jamaa pale mapinga aliwauzia wachina matofali ya kutosha.
Anakwenda kudai hela wachina wamemaliza kazi wameondoka
Amefilisika mpaka leo
Hakuingia nao mkataba.
 
Pole sana Kapten, naona unapigwa speed governor upunguze kidogo vurugu na mama michepuko. Umeandika Kwa hisia na upole wa Hali ya juu kama sio wewe kidume Cha kusawazisha
 
na ukitaka kufa haraka shiriki biashara za kukopesha taasisi za serikali, hawalipiiiiiiiiiiiiii utalia na kusaga meno kuna usanii mwingi sana mara taratibu za manunuzi mara sijui nini upigani kibaaaao yaani mpaka kero
 
Mkuu kosa lako ulitoa Pro former bila kuwaandikia limit ya muda. Kuna pahala tulienda kuchukua list ya vifaa na wakakubali kutoa pro former ila wakatugea limit ya wiki moja tu.
Na chini wakaandika "ikipita wiki moja basi karatasi hii haitopokelewa hapa ofisini kwetu" [emoji23][emoji23][emoji23]
 
na ukitaka kufa haraka shiriki biashara za kukopesha taasisi za serikali, hawalipiiiiiiiiiiiiii utalia na kusaga meno kuna usanii mwingi sana mara taratibu za manunuzi mara sijui nini upigani kibaaaao yaani mpaka kero
Yaan Ni wasumbufu Sana mkuu
 
Mkuu kosa lako ulitoa Pro former bila kuwaandikia limit ya muda. Kuna pahala tulienda kuchukua list ya vifaa na wakakubali kutoa pro former ila wakatugea limit ya wiki moja tu.
Na chini wakaandika "ikipita wiki moja basi karatasi hii haitopokelewa hapa ofisini kwetu" [emoji23][emoji23][emoji23]
Umeniongezea kitu kichwani
 
Pole kaka si ungetafta mwanasheria akusaidie,na ulivopokea pesa kwenye account yako ya bank,ungeenda kwa manager wa bank kureport ili kujihami uwe salama , haki yako haiji kwa kuilalamikia bali kuipigania.usiwe mnyonge
 
Jitaidi kupata koneksheni ya watu wenye dawa mbaya usikubali kuonewa hovyo.
 
KESI YA PILI,
Wanakuja Watu wa taasisi wanakuja kwako wanataka material

Unawaambia
"Hapa bila cash hamna mzigo wakuu"

Wanakwambia pesa zipo na zishaingizwa kwenye force account.

Unasema "sawa tufanye KAZI"

Siku ya kwanza Wanachukua mzgo wanalipa cash. Siku inayofata wanachukua mzigo wanalipa cash.

Sasa Kama mjuavyo hasa kwenye mambo ya ujenzi, Kuna vitu kadha wa kadha vinasahaulika na vingine huibuka pale pale saiti kutokana na mahitaji ujenzi husika.

Mtu wa taasisi atakwambia,
"Kaka namtuma kirikuu, mpe Moja mbili tatu pesa nakuja nayo nikitoka saiti" . unasema "sawa"

Ikifika jion kimya,
Unamuacha mpk kesho yake
Ukimtafuta anakwambia
"Kaka Jana MDA ule benki washafunga, na leo sijaenda saiti tulikua na kikao, tuonane kesho"
Unasema "sawa"

Kesho yake ukimtafta Anakwambia,
"Kaka pesa yako imechelewa, Kuna signatory mmoja ametoka. Haya mambo ya taasis pesa hazitoki kwa sahii ya mtu mmoja. Tuko Kama watano kusiani ndo kuidhinisha malipo" . Unasema "sawa"

Wanakaa zaidi ya wiki ndo unalipwa pesa zako na ujenzi wao bado unaendelea, wakifika hatua ya kuanza kutindua kuta na kulaza mabomba ya umeme na maji watakutafuta Tena mkae mezani.

Utaletewa orodha kubwa ya vifaa vya maji na umeme uorodheshe Bei zao utakazowauzia.
Unawauliza
"Mnataka bei za cash cash au mkopo?"
Watakwambia,
"Kaka Mbona mzito kuelewa?"
"Hapa tuuziane cash cash, ushaambiwa Mzigo umewekwa kwenye force account, unalipwa cash cash"

Unasema
"Basi sawa, Bei ntawauzi hizi hapa"
Kisha unazijaza hiz Bei kwa Kila bidhaa kweye fomu zao na kuzisaini. Wanazichukua na kuondoka zao.

Wiki zinapita, hawaji kununua Mzigo
Miezi inapita, hawaji kununua mzigo
Mwaka unaisha, hawaji kununua mzigo.
Kumbe mradi umesimama, pesa hazijaja na hawakwambii.

Baada ya mwaka na kitu ndio wanaibuka, na Lile fomu lao la Bei za mwaka Jana ulizowaandikia.

Wanakuja na cash kabisa kabisa wanataka mzigo wao wakamalizie mradi. Unawaambia
"Wakuu, mmechukua Moja mbili tatu, jumla mzigo wote mnapaswa kulipia shilingi Fulani"

Wanastuka na kutizamana usoni,
"Wewe jamaa, sisi pesa tuliyopewa ni Hii Hapa. Usitake kutupandishia Bei.
Fomu yako Hii Hapa ulituandikia na kusaini mwenyewe"

Unawaambia,
"Ni kweli, ila mzigo wa kipindi kile sio sawa na mzigo nilonao wa Sasa.

Kwa Sasa bidhaa mnazotaka Bei zimepanda sana, na Hizi Bei nilioandikia mlisema mnanilipa cash cash siku ile afu mkapotea jumla.

"Inakuaje mnakuja mwaka huu mnataka niwauzie kwa Bei za mwaka Jana? Na Bei wenyewe hizi za Corona vitu vimepanda bei Zaid ya mara mbili"

Wanasema
"Hilo la Bei kupanda sisi halituhusu, kwahiyo Unatuuzia hutuuzii?"

Unawajibu,
"Kiukweli kwa Bei hizo mlizokuja nazo, siuzi mzigo bora uozee TU dukani. Mkamuungishe TU mwingine, haikua riziki yangu. Mtaa huu Maduka yako mengi wakuu"

Wanajibu, "sawa, tunaondoka"

Baada ya wiki wanarudi Tena,
"Aisee Kaka hebu tuuzie mzigo, Hii ishu Ni urgent. Huu mradi unatakiwa uzinduliwe na mweshimiwa na atakuja kuukagua. Mfumo tu unazingua, kesho kutwa pesa yako unaingiziwa"

Unawaambia,
"Kiukweli kwa ulipaji wenu, ni ngumu Sana kuwapa mzigo. Nyie nendeni mkakope mahali mje na cash niwape mzigo muende. Au chukueni mishahara yenu mjazie, pesa ya mradi ikiingia mtajirudishia pesa zenu. Kwangu hapana"

Watakwambia
"Unazingua, wewe dawa yako ndogo"

Unasema "POA wakuu"

Basi hujakaa sawa,
Unashangaa Kuna pesa inaingia kwenye account yako kimya kimya.

Unasubiri labda Kuna mteja atakupigia Simu kukufahamisha kua kakuingizia pesa,Anataka mzigo flani.Nako kimya.

Zaidi ya wiki imepita tangu uingiziwe pesaUnashangaa maaskali wamekuja kukukamata bila maelezo yoyote.

Ukifika kituoni unauliza shida Nini, unaambiwa Ni maelekezo ya kiongozi fulani kapewa mamlaka ya kukuweka ndani masaa 48 bila maelezo.

Unalala siku ya kwanza kituoni,
hamna maelezo ya kueleweka.
Siku ya pili unaambiwa
"unahujumu mradi makusudi, umegoma kutoa mzigo na pesa ushalipwa"

Unabaki mdomo wazi,
Unauliza "pesa gani hiyo nishalipwa?"

Wanakwambia
"ushahidi Ni huu Hapa"
(Unaonyeshwa Bank slip ya ile pesa iliyoingia kimya kimya kwenye account yako).

Wanaongezea
"Hii kesi huna dhamana utapelekwa mahakamani kwa kuhujumu na kuchelewesha mradi makusudi na pesa ushalipwa na ushahidi tunao"

Ukishasikia habari ya kesi tena
Roho inakuruka, unaomba mkae mezani myazunguze kumaliza utata.

Majamaa Wanataka figure za pesa zinazowaijia TU kichwani wanavojiskia.

Unajisemea "pesa zinatafutwa, Uhuru kwanza "Unawalipa unatolewa ndani.

Mpaka unaruhusiwa kutoka ndani,

Tayari Ushanyonyoka pesa kibao ambazo hata ungewauzia kwa Bei ile ya hasara zisingefikia kiasi hicho walichokupiga.

Ukirudi mtaani unakua Kama unaanza na Moja Tena, majuto na masononeko kibao.

Wakitoka hapo,
Watu hao hao wa taasisi Wanakuhama
Na Hawanunui Tena kwako.

Biashara na Taasisi Zina frustration sana,
Yamenikuta mwaka huu na najuta[emoji22]
Next time pesa ikiingia kwenye account yako bila taarifa report Police
 
Next time pesa ikiingia kwenye account yako bila taarifa report Police
Account yang inapokea nyingi Sana kutoka kwa Watu/sehemu tofauti tofauti Kila siku

Mwingine anakutumia pesa anajikusanya kuwezekeza material kidg kidg Kisha baada ya wiki au mwezi anakuletea slip zake zote, unaangalia kweli alikuingizia pesa unampa mzgo anaondoka zake.

Halikunipa shida hata kdg,
Nilijua TU Ni Kama ilivozoeleka
 
Kuna brother wangu anaidai halmashauri moja huku kusini zaidi ya Million 70+ huu mwaka wa pili... ana duka la vifaa vya Ujenzi,, ameyumba sana, ameuza magari yake mawili ya kutembelea kupambana na mikopo yake benk,, aise Aya Mambo acha kbsaa!!
Biashara si biashara hadi pesa inapoingia kwenye akaunti yako......
 
Kuna ndugu yangu somewhere waliwah kumfanyia mchezo kama huu... Nikamwambia naomba majina ya hao wapumbavu walikufanyia huo unyama... The rest is history, saa hizi wapo mtaani mwaka wa 4 huu hawana kazi familia zao hazina mbele wala nyuma, I hope watakufa kwa jinsi maisha yalivvyo wanyoosha... Hii dunia ukifanyiwa unyama lipiza unyama, kumuachia Mungu ni upuuzi kwasabab hata huko kwa Mungu huna uhakika wa kufika...
 
Kuna ndugu yangu somewhere waliwah kumfanyia mchezo kama huu... Nikamwambia naomba majina ya hao wapumbavu walikufanyia huo unyama... The rest is history, saa hizi wapo mtaani mwaka wa 4 huu hawana kazi familia zao hazina mbele wala nyuma, I hope watakufa kwa jinsi maisha yalivvyo wanyoosha... Hii dunia ukifanyiwa unyama lipiza unyama, kumuachia Mungu ni upuuzi kwasabab hata huko kwa Mungu huna uhakika wa kufika...
Hii ndo inatakiwa unyamaunyama2 hakuna kucheka na nyani
 
Back
Top Bottom