Kufa au kupona- Kutoroka kwa Rahaf al-Qanun

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,049
Tibilisi, Georgia

Wafa mwenye umri wa miaka 25, na dada yake Maha mwenye umri wa miaka 28, waliwalaghai wanafamilia ya kwamba wanasafiri kwenda mji wa Ranyah, huko Saudi Arabia kumtembelea kaka yao.

Wakiwa katika mji mkuu wa Saudia, Riyadh, mabinti hawa walifanikiwa kupata passport na tiketi za ndege kuelekea mji mkuu wa Uturuki, Istanbul pasipo familia yao kufahamu jambo lolote. Tarehe 1, mwezi wa 4 mwaka 2019, waliwasili katika uwanja wa ndege wa Instanbul, Uturuki. Mabinti hawa walivunja sim card zao ili wasiweze kufuatiliwa. Pia walivua mavazi yao ya niqab, lengo likiwa wasije kushtukiwa kuwa wametoka kwenye familia zenye msimamo mkali na kuulizwa kwanini wanatembea wakiwa peke yao. Kisha walipiga selfie, na hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mabinti hawa kupanda ndege.

Lengo la mabinti hawa ilikuwa waweze kufika mpakani kati ya Uturuki na Georgia. Kutokana na fununu kwamba mambo ya ndani ya nchi ya Georgia hayajulikani kwa watu wa nje na pia raia wa Saudi Arabia hawahitaji visa kuingia Georgia, mabinti hawa waliona ni sehemu sahihi ya kujificha.

Kutokea Instanbul, mabinti hawa walichukua usafiri wa ndege na kuelekea katika mji wa Trabzon, huku wakiwa wanapiga sala ndege yao isichelewe. Ilikuwa ni muda kidogo tu ambapo kaka yao ataenda kuwapokea na asiwakute, jambo ambalo lingefanya familia ijue kuwa mabinti hawa wametoroka.

Walipowasili Trabzon, walikodi taxi na kusafiri umbali wa maili 113 mpaka kwenye mpaka wa Georgia. Walifika mji mdogo uliokaribu na Bahari Nyeusi (Black Sea) unaojulikana kama Batumi, wakaingia kwenye mgahawa mdogo ambapo walikuta kuna akina mama peke yao, wakaomba msaada. Mama mmoja raia ya Georgia alijitolea kuwa hifadhi kwake, na kisha siku iliyofuata aliwapeleka mji wa Tbilisi uliopo maili 230 kutoka Batumi.

Mabinti hawa walidai wanakimbia manyanyaso, na mateso na ukosefu wa uhuru kwasababu ya sheria za huko kwao Saudi Arabia. Walidai mwanamke anahitaji kuwa na ruhusa kutoka kwa ndugu yake mweye jinsia ya kiume kwa kila maamuzi ya msingi anayotaka kuchukua. Walitumia kwa siri akaunti ya baba yao ya application ijulikanayo kama Absher, hii ni application ya Saudi Arabia ambayo mzazi au mlezi hutumia kumwekea alama mwanamke kuwa kampa ruhusa ya kusafiri. Vyombo vya usalama uwa wanaitumia kuangalia mwanamke kama ana ruhusa iwapo watahitaji kufanya hivyo.

Lakini hawa siyo wanawake peke yao ambao wamejaribu kukimbia saudi Arabia. Wachache wamefanikiwa na wengi wameshindwa na kuishia kuuawa na familia zao au kuteswa.

Kisa cha Rahaf al-Qanun
rafa.jpg


Rahaf al-Qanun akiwa na umri wa miaka 18, alikuwa katika safari ya matembezi yeye na familia yake huko Kuwait wakiwa wametokea Saudi Arabia. Wakiwa Kuwait, binti huyo (wa katikati kwenye picha) aliwatoroka na kupanda ndege kuelekea Australia. Ndege hiyo ilikuwa inabidi ipite Bangkong ambapo ataunga ndege nyienge kwenda Australia kwakuwa alikuwa na Visa ya Australia.

Alipotua Bangkok, kumbe habari ya kutoroka kwake ilikuwa ishajulikana na taarifa ilikuwa ishatolewa kuwa akitua Bangkok ashikiliwe. Basi alipotua tu akanyanganywa passport na maafisa wa Ubarozi wa Saudia aliokutana nao wakati akiwa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi. Bila passport alikuwa hawezi kuendelea na safari. Basi walimweka kwenye chumba cha hoteli pale pale uwanja wa ndege wakisubiri familia yake ije kumchukua.

Rahaf al-Qanun alikuwa anaua kuwa akichukuliwa na kurudishwa kwao atauawa na kama hatouawa basi atateswa sana. Jambo moja ambalo watu hawakulijua ni kwamba, toka anaanza safari alikuwa anasaidiwa na mabinti wengine waliofanikiwa kutoroka kumbe walikuwa na kundi lao wanaelekezana nini cha kufanya na ni wapi pa kuelekea. Kosa la maafisa wa ubarozi walilofanya ni kutomnyanganya simu.

Rahaf al-Qanun hauwa tayari kurudi nyumbani, hivyo akajifungia kabisa kwenye chumba cha hoteli huku wenzake wakimshauri inabidi afanye jambo litakalo vuta mashirika ya kimataifa na nchi kujua nini kinaendelea juu yale. Kosa jingine alilokuwa kafanya ambalo kama angerudishwa kwao ni lazima angeuawa, alikuwa ka retadi (kajiondoa kwenye dini ya Uislam kwa kupost twitter).

Wenzake walimwambia kama anataka kuishi inabidi avue niqab, atengeneza video aipost mtandaoni watu wamuone sura yake wajue kuwa kweli anaye tweet hizo tweeets hatanii bali ni mtu kweli. Ikabidi afanye hivyo akaanza kujirekodi video na kuziposta akielezea hali yake na kuwa akirudishwa nyumbani atauawa. Kwa muda mfupi story yake ikawa kubwa watu wakaanza kuisambaza twitter, wakiwatag viongozi wa mashirika makubwa kama UNHCR, na asasi za haki za binadamu.

Wengine wakaanza wasilaina na mamlaka za Thailand kujua kwanini wamemshikilia bidada. Mamlaka za Thailand zikawa zinadai kuna tatizo la kifamilia ndiyo maana hawakumruhusu kuendelea na safari, huku wengine wakisema aliomba visa alitaka abake hapo wakamkatalia hivyo wanamrudisha kwao.

Rahaf al-Qanun bidada aliendelea kujifungia ndani pasipo kutoka hata walipogonga mlango hakufungua. Ikafika muda maafisa wa Thailand wakishirikiana na wa Ubarozi wa Saudia wakaja kugonga mlango wakijifanya kuwa ni maafisa wa UN ili afungue, bidada akawambia kama kweli wametoka UN wapitishe vitambulsiho vyao chini ya mlango aone. Mbinu zao zikagonga mwamba. Bahati nzuri kuna mwandishi wa habari wa Australia aliona tweets zake aksafiri mpaka Bangkok, na kwenda mpaka pale hotelini. Bidada akamfungulia mlango akaingia wakawa wote mle ndani.

Huyo mwandishi akaanza wasiliana na watu mbalimbali kujaribu kutafuta msaada. Ubarozi wa Australia ukakubali kuja kumchukua. Wakamchukua na kumpeleka Ubarozini ila wakawa hawajampa hifadhi akawa yupo ubarozini tu. Canada wakaingilia kati wakamchukua na kumpa hifadhi na kumpeleka Canada.

Bidada mpaka leo anaishi na kusoma Canada. Siku chache zilizopita kapost picha amevaa Bikini kalio wazi wazi, wananzengo wamemaindi kwamba yani alikuwa anatafuta uhuru wa kuanika kalio.

Mbaki Salama Salmin....
 
Hii stori inasikitisha sana. Nchi nyingine tofauti na Jehanamu ni ndogo sana.
 
Hahaha 😂 😂 watu wanataka uhuru ... Mtu unaishi katika nchi kama upo kuzimu khaaa!!
 
Back
Top Bottom