Kuendesha PlayStation (Playstation Management)

Kuendesha PlayStation (Playstation Management)

Mtuiz

New Member
Joined
Mar 17, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Habari gani👋🏾
Je kuna mtu yoyote ambae ana experience ya kuendesha Play station?🎮
Je unazijua changamoto?
Je zinatatuliwaje?
Zipi mbinu za kuvuta watu zaidi?
Games zipi ni pendwa zaidi?
Decorations za ndani zipi zinavutia zaidi?
Kwa sasa watu wanapenda Ps4 au Ps5?
Yapi maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kufungua play stations?
Maeneo yapi ni mazuri zaidi kufungua biashara hiyo?


Tupeane maarifa kwa ufupi leo tukijadili hili wadau🤌🏿
 
Maeneo mazuri ni changanyikeni usifungue mitaa ya ushuani maana wale wanazo kwenye majumba Yao.
Maswali mengine watajibu members wengine
 
Habari gani
Je kuna mtu yoyote ambae ana experience ya kuendesha Play station?
Je unazijua changamoto?
Je zinatatuliwaje?
Zipi mbinu za kuvuta watu zaidi?
Games zipi ni pendwa zaidi?
Decorations za ndani zipi zinavutia zaidi?
Kwa sasa watu wanapenda Ps4 au Ps5?
Yapi maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kufungua play stations?
Maeneo yapi ni mazuri zaidi kufungua biashara hiyo?


Tupeane maarifa kwa ufupi leo tukijadili hili wadau🤌
Ngoja nikupe maujanja..

Kama utafungua PS kitu cha msingi ni wateja... Wateja unawapataje?

Andaa shindano ambapo mshindi wa kwanza hadi wa tatu atapata posho... Mfano mshindi wa kwanza 50k, wa pili 30k wa tatu 20k...

Na usiweke kiingilio chochote kwa watu kushiriki mashindano hapo utakua umetumia sh. Laki Moja tu kufanya promo...

Nimechoka kutype bana nikipata muda ntakupa faida, changamoto na nini cha kufanya
 
Habari gani👋🏾
Je kuna mtu yoyote ambae ana experience ya kuendesha Play station?🎮
Nishawahi kufanya iyo biashara takribani miaka minne iliyopita
Je unazijua changamoto?
Changamoto zake
1. Controller kualibika mara kwa mara. Unatakiwa kununua controller imara, pia fuatilia wateja ambao wanazikandamiza controller wakati wa kucheza game waambie wacheze taratibu tu bila kutumia nguvu sana.
2. Watoto watolo shuleni kuifanya ofisi yako ndio chimbo. Usiruhusu wanafunzi muda wa shule especially wakiwa wamevaa uniform.
3. Malalamiko ya wazazi kwamba watoto wanaiba hela nyumbani kuja kucheza ps. Hapa unaweza kumwambia mzazi akuonyeshe mtoto wake ili uwe unamkata kuingia ofisini kwako
4. Mgogoro wa umeme wa wapangaji wenzako. Wapangaji wenzako watakua na fikra kwamba unatumia umeme mwingi sana. Kukabiliana na hii changamoto ni vyema ukawa na submeter ambayo inasoma matumizi yako ya umeme.
Zipi mbinu za kuvuta watu zaidi?
mbinu za kuvuta watu ni kuanzisha mashindano ya kimtaa au vijiwe, yaani mitaa au camps tofauti kila upande unatoa mzigo halafu anatafutwa nani bingwa wa ps. Mbinu zingine unaweza kujiongeza mwenyewe
Games zipi ni pendwa zaidi?
game ya mpira. Akikisha unayo ya msimu husika
Decorations za ndani zipi zinavutia zaidi?
Hii haina umuhimu sana. Kwa picha za ukutani unaweza kuweka tu za wachezaji wa mpira. Viti viwili au sofa moja ya kukaa watu wawili mbele ya tv kwa ajiri ya wanaocheza na sofa kubwa la watu watatu au wanne ambao ni watazamaji. Kwa joto la dar feni pia muhimu
Kwa sasa watu wanapenda Ps4 au Ps5?
HApa sipajui kidogo maana kwa kipindi hicho mimi nilikua na ps3 ila always watu lazima watapendeleo toleo la mwisho tu.
Yapi maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kufungua play stations?
Ukiwa na wazo la biashara usijiulize sana, wewe anza tu mengine yatajiset mbele kwa mbele.
Maeneo yapi ni mazuri zaidi kufungua biashara hiyo?
Maeneo ya uswazi kidogo au makazi ya watu wa hali ya kati. Usiweke ofisi yako karibu sana na shule ya msingi ili kuepuka lawama za wazazi, walimu na viongozi wa mtaa
Tupeane maarifa kwa ufupi leo tukijadili hili wadau🤌🏿
Nyongeza; zingatia suala la umeme. Kadiria matumizi yako kwa siku halafu unapoungua ofisi tu akikisha zipo unit za kutosha mpaka muda utakaofunga. akikisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom