Kuendesha Gari Barabara Kuu Sasa ni Kero: Alama za 50km/hr Zinapaswa Kupitiwa Upya

Unadhibiti gari je ajali ikitokea inaua gunia au mtu.endelea kuringa na speed zako ila tambua speed kills.reasoning yako inaonyesha jinsi ulivyo

Sasa nimejua kwa uhakika kabisa muda wote huu nilikuwa nampigia mbuzi gitaa!
 
Wiki iliyopita nilikuwa nikisafri toka Moshi kuja Dar nikiwa na Landcruiser V8. Baada ya kuvuka mto Wami nilisimamishwa na askari wa Usalama Barabarani nikaambiwa niliteremka bonde la mto Wami kwa spidi ya 70km/hr badala ya 50km/hr.

Nilimuuliza kiongozi wa wale askari pale kama alidhani ni busara kutegemea gari kama Landcruiser V8 kuwekewa kiwango cha spidi cha 50km/hr sawa na semitrailer iliyobeba mzigo wa tani 20, ukizingatia kwamba lengo la kiwango cha spidi kuelekea mto Wami ni kudhibiti gari na sio kuhatarisha uhai wa watu, kwa kuwa lile sio eneo la mji. Kama kawaida ya polisi hakuelewa nilichosema zaidi ya kung'ang'ania nilipe faini ili awafurahishe wakuu wake wa kazi kwa mapato.

Naunga mkono kabisa suala la spidi ya 50km/hr maeneo ya watu, lakini kuna walakini iwapo vibao vyote vya 50km/hr vimewekwa sehemu zinazostahili au viko reasonable kwa gari za mizigo na ndogo kufuata hiyo spidi limit.

Nimeshakutana na maeneo mengi yenye utata sana kuhusiana na hizi spidi za 50km/hr. Kuna sehemu nyingine haieleweki kwa nini hata kibao kiliwekwa. Kuna sehemu nyingine utakuta 50km/hr ni amri yenye umbali usiozidi mita 100. Kuna sehemu kuelekea eneo la mji hivi vibao vimewekwa tangu aneo la mbali sana bila sababu za msingi - mfano kuingia Same ukitokea Moshi. Kuna sehemu nyingine umbali wa kutumia 50km/hr ni mkubwa sana na hata unapita sana nje ya eneo la mji.

Kuna sehemu nyingine zenye maudhi utakuta kibao kukuonyesha mwisho wa 50km/hr kiliondolewa, labda kwa ajali, bila kurudishiwa. Kuna sehemu nyingine, kama hilo la bonde la Wami au mteremko wa Kiwira kule Mbeya (Uwanja wa Ndege), haileti maana kwamba gari ndogo na malori yote yanatakiwa kutumia 50km/hr ikiwa suala ni kumwezesha dereva adhibiti gari yake kutokana na kuwa ni eneo la hatari. Kuna sehemu nyingine hivi vibao vinaonekana ghafla sana bila dereva kuviona mapema ili kupunguza spidi - na hivi hupendwa sana na traffic kuweka mitego yao.

Ningependa kutoa wito kwa TANROAD na Polisi Usalama wa barabarani kupitia upya hivi vibao kama kweli lengo lao ni kudhibiti usalama na sio kuvifanya vyanzo vya mapato kwa serikali. Tulio na safari za mara kwa mara tumeanza kuamua kusafiri usiku ili kukwepa tochi, jambo ambalo nina uhakika kabisa sio salama sana.
Mi mpaka huwa nadhani kna makosa ya vipimo hivi vya Metric.
 
Nilipita Arusha majuzi kutokea mjini kuja Dar nafika sanawari mpaka tengeru ni 40km/hr na barabara iko kwenye matengenezo lakini trafik wako barabarani na tochi hii sasa inakuwa ni kama kuwakomoa madereva na mkumbuke sio kila anayeendesha gari ni mmiliki wagari au kila anapoendesha gari ana pesa mfukoni,huu sio utaratibu mzuri kweli kikosi cha usalama barabarani agalieni hili swala mnatufanya wananchi tuichukie serikali yetu iliyoko madarakani bure kwa kitu mnachoweza kurekebisha

Na sio muda wote kuna Men at Work wakitengeneza hicho kipande cha barabara
 
Majuto ni mjukuu Bwana V8 Masifa Masifa, punguza mwendo, tii sheria. Kwenye hizo mbio zako, akikatiza tu mnyama pori barabarani wewe ni mhanga.

Fahari ya binadamu ni kuwa hai, sio kufia ndani ya V8. Jali maisha yako na ya wengine.

Usinikasirikie mie. Mie sio kisababishi cha wewe kutoweza kununua gari hadi leo. Ningekuwa masifa ningeteremka Wami na 70km/hr? Na nani amekuambia sikufuata 50km/hr huko nyuma? Una hasira na wenye magari hadi unashindwa kuelewa thread inasema nini. Mwenye kuhemuka hapa nani sasa? Na V8 utazisikia tu redioni na kuzisoma namba.
 
Juz natoka mbeya narud dsm akanisimamisha trafik maeneo ya nyololo..kweli nilikuwa spid 156..akaninyesha nikamwambia ni kweli tena hii nimepunguxa nlipokuona ila huko nyuma nilikuwa na 175..akasema spid ni kubwa mno unaenda wapi?nikajib dsm..lipa fine..nikasema sina hela bali maji ya barid haya hapa..nikawapa chupa moja ..nikaondoka..
 
Usinikasirikie mie. Mie sio kisababishi cha wewe kutoweza kununua gari hadi leo. Ningekuwa masifa ningeteremka Wami na 70km/hr? Na nani amekuambia sikufuata 50km/hr huko nyuma? Una hasira na wenye magari hadi unashindwa kuelewa thread inasema nini. Mwenye kuhemuka hapa nani sasa? Na V8 utazisikia tu redioni na kuzisoma namba.
Sikukasirikii, nakusikitikia. Mimi nina magari ya biashara na pikipiki ya kutembelea. Sina V8 kweli...kwenye hayo tuishie hapo.

Kuhusu usalama barabarani, ACHA UJUAJI. Ukiwa Wami, endesha kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa. Kuna watu wana fahamu zaidi yako, ndio walioweka zile alama baada ya kuzingatia mambo kadhaa.
 
Una magari ya biashara unatembelea pikipiki? Huna kitu wewe, acha kututambia bure. Mtu mwenye magari ya biashara hawezi kutembelea pikipiki kwa kuogopa kugongwa na magari na kufa na kuacha watu warithi magari yake. Empty bragging!

Na kwa nini usiwe na self confidence kwa kudhani kila lililofanywa limefanywa na watu wanaofahamu zaidi yako? Wao ni malaika wasiokosea? Hata mainjinia wakali wa kutengeneza ndege kuna wakati wanakosea. Hata raisi kuna wakati anakosea anastahili kukosolewa. Sembuse hawa vilaza walioweka alama za 50km/hr barabarani pamoja na sehemu zisizostahili? Au hujaona sehemu nyingi tu wameweka dotted au solid line (sijui kama unazijua) barabarani sehemu zisizostahili?
 
Hii speed ya 50km/hr tena porini hakuna makazi ya watu sielewi inatoka wapi.. na unakuta barabara imenyooka..

Sehemu korofi zimajulikana, eg karibu na mito, au kona kali, miteremko na milima, ila njia nyeupe kabisa au kijiji lina watu labda 50 unaweka sp. 50, ya nn..?

Speed safe na most acceptable kwa high way atleast 80km/hr.... hii inatosha kabisa hasa kwa magari ya abiria na mizigo.. na sehemu zilizo nyooka..!! ukiacha sehemu korofi..

But magari private, mm nadhani sehemu iliyonyooka hata akiwa 100km/hr ktk highway haina shida kwa Tz..

50km/hr kwa private cars ni ndogo sana sana highway za Tz.. speed ndogo sana hiyo.. alafu polisi walivyo wa ajabu, hata ukiwa 51km/hr eti wanakukamata..? Mambo ya ajabu haya.. sbb huwezi kuendesha constant 50km/hr.. sometimes inafika 55km/hr mara inashuka 45km/hr..

Polisi lazima wapewe speed limits.. sio exactly 50km/hr ktk makazi ya watu.. ili ukiwa hata 55km/hr is ok..

Hii biashara ya speed imekuwa ya KUTAFUTA KIPATO SANA KWA POLISI SIKU HIZI.. SHIDA NI HELA TU
 
Vibao vinafichwa makusudi ili trafiki wapate hela. Ukiwa barabara ya morogoro dar bango la kutoruhusu kukata kona limefichwa nyuma huku mbele trafiki anakusubiri ukate kona akulime. Mapato ya fine za trafik 59.3 bilion ziende kuweka miundombinu sahihi za barabara
 
Kwa hiyo wewe wakati unateremka hapo mto wami, uligeuka jiwe, yaani hukuwa mtu! Halafu mule bondeni si kuna majumba mle watu wanaishi!...Elimu zenu hizi za barabarani zitatupeleka kusiko! Ulitakiwa kulipa faini mara mbili kwa usumbufu kwa askari!
 
Tanzania nzima mwisho ni 80 km/saa, na kuna sababu za msingi kuamua hivyo, hapa maslahi ya Watanzania yamewekwa mbele na siyo baadhi ya watu wenye V8, hutaki hama nchi!
hivi unajua sheria ya 80km/hr ilitungwa mwaka gani na ni mazingira yepi yaliyofanya ikawa 80km/hr?
 
Una magari ya biashara unatembelea pikipiki? Huna kitu wewe, acha kututambia bure. Mtu mwenye magari ya biashara hawezi kutembelea pikipiki kwa kuogopa kugongwa na magari na kufa na kuacha watu warithi magari yake. Empty bragging!

Na kwa nini usiwe na self confidence kwa kudhani kila lililofanywa limefanywa na watu wanaofahamu zaidi yako? Wao ni malaika wasiokosea? Hata mainjinia wakali wa kutengeneza ndege kuna wakati wanakosea. Hata raisi kuna wakati anakosea anastahili kukosolewa. Sembuse hawa vilaza walioweka alama za 50km/hr barabarani pamoja na sehemu zisizostahili? Au hujaona sehemu nyingi tu wameweka dotted au solid line (sijui kama unazijua) barabarani sehemu zisizostahili?
Nawatambia wewe na nani? Be confident, am talking to you. Kuwa na magari ya biashara sikumaanisha mimi ni tajiri, nilimaanisha kuwa ninayo. Na ndio sehemu ya uchumi wangu. By the way, nimezaliwa mjini, sioni ajabu ya mtu kumiliki gari km unavyoona wewe.

Ningefurahi sana ungenipa ushahidi wa hizo sehemu zilizowekwa mistari au dash lines pasipo stahili.

Naomba mjadala wa mimi na wewe uelekee huku na sio kwenye namiliki nini? Twende kwenye mistari iliyokosewa
 
Hii speed ya 50km/hr tena porini hakuna makazi ya watu sielewi inatoka wapi.. na unakuta barabara imenyooka..

Speed 50 si kwa makazi ya watu tu, huko unakoita porini kuna udhibiti mwingine unaendelea. Eneo unalolifahamu wewe kama pori, kuna taasisi au mamlaka nyingine inalitambua kivingine. Mapito ya wanyama, vivuko vya mifugo na hata frequency ya matukio ya ajali za nyuma zinaweza kuwa sababu.

Sehemu korofi zimajulikana, eg karibu na mito, au kona kali, miteremko na milima, ila njia nyeupe kabisa au kijiji lina watu labda 50 unaweka sp. 50, ya nn..
Si kweli kwamba kila kwenye kijiji kuna katazo la mwendo kasi wa zaidi ya 50. Na sioni ni rahisi kwako kiasi gani kujua idadi ya watu kwa kupita na gari lako barabarani. Nyumba unazoziona karibu na njia sio ndio nyumba zote zilizopo eneo husika, kijiji hakikai pembeni mwa njia.

Speed safe na
most acceptable kwa high way atleast 80km/hr.... hii inatosha kabisa hasa kwa magari ya abiria na mizigo.. na sehemu zilizo nyooka..!! ukiacha sehemu korofi..

But magari private, mm nadhani sehemu iliyonyooka hata akiwa 100km/hr ktk highway haina shida kwa Tz..

50km/hr kwa private cars ni ndogo sana sana highway za Tz.. speed ndogo sana hiyo.. alafu polisi walivyo wa ajabu, hata ukiwa 51km/hr eti wanakukamata..? Mambo ya ajabu haya.. sbb huwezi kuendesha constant 50km/hr.. sometimes inafika 55km/hr mara inashuka 45km/hr..

Polisi lazima wapewe speed limits.. sio exactly 50km/hr ktk makazi ya watu.. ili ukiwa hata 55km/hr is ok..

Safe na most acceptable kwa mujibu wa utafiti upi ulioufanya? Wakati mamlaka zimefanya utafiti na kuweka viwango, tusiwe wepesi kuhoji kwa hisia. Barabara zina viwango na hadhi. Hata hivyo, Sheria ya Usalama Barabarani ya Tanzania haijaongea lolote kuhusu kikomo cha mwendo kwa magari yaliyo chini ya 3.5tons kwa maeneo yasiyo na katazo. Lakini kwa maeneo yenye katazo, mwendo unapaswa kuzingatiwa kwa vyombo vyote.

Hoja ya 51 na 55 hazina mashiko kwani hakuna atakayekukamata ukiendesha 45. Jifunze kutii sheria.

Hii biashara ya speed imekuwa ya KUTAFUTA KIPATO SANA KWA POLISI SIKU HIZI.. SHIDA NI HELA TU
Biashara huusisha muuzaji na mnunuzi. Amua kutofanya makosa ili wakose mteja. Dhana uliyoiweka kichwani mwako kuhusu askari wa usalama barabarani inarudisha nyuma harakati za kutokomeza ajali.
 
Vibao vinafichwa makusudi ili trafiki wapate hela. Ukiwa barabara ya morogoro dar bango la kutoruhusu kukata kona limefichwa nyuma huku mbele trafiki anakusubiri ukate kona akulime. Mapato ya fine za trafik 59.3 bilion ziende kuweka miundombinu sahihi za barabara
Kasumba ya kutotii sheria
Kasumba ya kunung'unika hata bila kuwa na ushahidi
Kasumba ya kukariri.

Kama bango limefichwa, mbona umeliona? Kwote duniani, kibao cha tahadhari, maelekezo na hata onyo hukaa mita kadhaa kabla ya sehemu yenyewe. Haiingii akilini bango likawekwe hapo hapo kwenye kona, sasa sijui saa ngapi utalisoma na saa ngapi utajipanga kutekeleza agizo.

Jiulize tu wewe mwenyewe kama alama ya kuonesha kuwa kuna tuta ingewekwa hapo hapo kwenye tuta, si kila mtu angekuwa anaruka mazima.
 
Hahaha! Mkuu, kuna sehemu zinastahili 50km/hr, lazima tukiri. Ila sasa ukiwa na gari ya maximum 260km/hr unatamani zile free way za Europe ambazo hazina kiwango cha spidi kanyaga mwenyewe utakavyo! Niliona Uturuki wao wana barabara mbili kati ya Ankara na Istanbul; kuna ile ya kanayaga utakavyo ambayo inalipiwa ushuru na ile ya spidi ya kawaida ya bure.
katika mji wa Asmara kule Elitrea speed ya mjini ni 30kph, ile nchi 70% ya watumishi wa umma ni wanajeshi na ukikamatwa unaweza pewa adhabu yeyote. Yaani hakuna jam wala msongamano wa magari.

Kule Mwanza kulikuwa na msongamano mkuwa wa magari kutokea eneo la mlango mmoja hadi natta, tangu magari yaamuriwe kutembea 50kph msongamano hakuna tena kwani magari yanaachiana nafasi ya kutosha. kwangu mie miji kama Dar Mwanza arusha speed ya mjini iwe 40kph wala hutasikia kelele za msongamano wa magari.
 
Tanzania nzima mwisho ni 80 km/saa, na kuna sababu za msingi kuamua hivyo, hapa maslahi ya Watanzania yamewekwa mbele na siyo baadhi ya watu wenye V8, hutaki hama nchi!

Maximum speed kwa magari Tanzania ni 100 kmh. Hiyo 80 ilikuwa zamani.
 
katika mji wa Asmara kule Elitrea speed ya mjini ni 30kph, ile nchi 70% ya watumishi wa umma ni wanajeshi na ukikamatwa unaweza pewa adhabu yeyote. Yaani hakuna jam wala msongamano wa magari.

Kule Mwanza kulikuwa na msongamano mkuwa wa magari kutokea eneo la mlango mmoja hadi natta, tangu magari yaamuriwe kutembea 50kph msongamano hakuna tena kwani magari yanaachiana nafasi ya kutosha. kwangu mie miji kama Dar Mwanza arusha speed ya mjini iwe 40kph wala hutasikia kelele za msongamano wa magari.

= Eritrea
 
Back
Top Bottom