Kuelekea Uhuru wa Kweli Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea Uhuru wa Kweli Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjanga, Sep 9, 2012.

 1. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  kila mtanzania mwenye nia njema na nchi yake bila shaka anatamani kuona Tanzania yenye
  amani, utulivu, na haki! yote haya yanawezekana endapo kutakuwa na mabadiliko na mageuzi
  ya namna nchi inavyoendeshwa (Uongozi imara, thabiti na inayosimamia haki).

  kwa sasa kuna milolongo mingi sana ya vifo vya raia wasio na hatia wakifa mikononi mwa
  watu wanaostahili kulinda maisha yao (POLISI)(haijalishi kifo kimetokana na harakati za kisiasa au la),
  na wanaharakati na hata viongozi wa kisiasa wanatoa milolongo ya orodha ya matukio ya hivi vifo!
  wengine wakitoa mawazo yao juu ya nini kifanyike ili kupunguza haya mauaji, ilhali wengine waki
  tuhumu vyama vya kisiasa kama chanzo cha mauaji haya!

  Kinachonishangaza zaidi ni pale Viongozi wakubwa na wazoefu ndani ya vyama na serikali
  wanavyoonesha kutoshangazwa na haya mauaji yanayofanywa na Polisi!
  Nikianza na Mheshimiwa Msajili wa vyama vya siasa kutoa kauli kuwa "Chama chochote
  kitakachohusishwa na matukio ya vifo kufutwa.." sijui huyu mheshimiwa alichukua muda wa kutafakari
  hathari ya hii kauli. kama haitoshi, wakati anashiriki kipindi cha "KIPIMA JOTO" kinachorushwa na ITV Bwana
  Tendwa anaonesha wazi na kubariki mauaji ya raia yanayofanywa na polisi kwa kusema "Mauaji yanafanywa na polisi
  sehemu nyingi (nje na ndani ya nchi)..." hii inaonesha ni jinsi gani anataka kuwafanya waTanzania kuamini kuwa Polisi
  kuuwa raia ni jambo la kawaida sana!

  siku ya 8/9/2012 Mhishiwa Wasira akitumia chombo cha habari cha umma (TBC1) ameonyesha waziwazi
  kuiegemea serikali na chama chake huku akishutumu CDM kama chanzo cha mauaji! akaendelea kuwashutumu wana
  harakati na CDM kuitaka serikali kuunda Tume Huru kuchunguza mauaji ya huko Nyololo! Wasira ametoa milolongo ya
  mauaji yaliyofanywa na polisi! kinachonishangaza ni pale yeye na wizara yake pamoja na serikali wanposubiri
  shinikizo toka kwa vyama pinzani na wanaharakati ndipo uchunguzi wa haya mauaji yafanyike!! Wasira amejitahidi
  kujenga hoja dhaifu na kutaka kutuaminisha kuwa kazi ya polisi na serikali ni kuuwa raia...haya yanathibitika ndani
  ya kauli zake hasa anaposema polisi nao ni binadamu...! inawezekana ikawa hivo lakini tunaamini Jeshi la polisi wanamafunzo ya kuweza kukabiliana na ghasia zozte bila kutumia nguvu nyingi na silaha za moto hasa wanapopambana na raia wasio na silaha!

  kimsingi kwa kauli za viongozi kama hawa wenye mamlaka makubwa, Je Tanzania bado i salama??
  ikumbukwe kuwa hata mbwa mwoga akichoka kukimbizwa ugeuka mkali na wa hatari kuliko yule shujaa!
  Mungu Ibariki Tanzania!
   
Loading...