Kuelekea uchaguzi wa wabunge nchini Burundi

Kuelekea uchaguzi wa wabunge nchini Burundi

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,481
Reaction score
1,450
Kesho tarehe 6 Juni, 2025, ni siku ambayo nchi ya Burundi itakuwa na uchaguzi wa wabunge nchi nzima.

Burundi, mojawapo wa nchi za jumuia ya Africa Mashariki, kwa miaka mingi, ilikumbwa na ghasia ya vita vya ukabila, ambapo wahutu na watutsi, haziivi mpaka sasa.

Makabila haya, mwanzo hayakuwa hivi, yalichochewa na ukoloni, sawa na nchini Rwanda.

Mpaka sasa, chama tawala cha CNDD-FDD chini ya rais Mhe Evariste Ndayishimiye, kimekuwa na tuhuma nyingi za kuwabana wapinzani, na huku chama cha CNL kikiondolewa katika mchakato huo. CNL chini ya Agathon Rwasa, ndo chama pekee kilichokuwa kikioneka kuwa na nguvu inayoweza kutikisa chama tawala.

Kupitia kundi la vijana wa chama tawala wajulikanao kama IMBONERAKURE,ambao kazi yao ni kutekeleza maagizo ya viongozi wa chama, wamevuruga amani kwa kiasi kikubwa, ikiwemo kuwapiga na kuwapoteza wafuasi wa vyama pinzani. Zimekuwepo kesi nyingi tena zikiongezwa za ubakaji.

Raia wengine hawakuweza kuvumilia hali hiyo, sehemu zingine waliwaumiza na kuwaua baashi ya vijana hao.
Chama tawala, ni cha kihutu, hali inayopelekea watutsi kuwa na wakati mgumu.

Katika utoaji wa orodha ya wagombea, yameonekana majina yaliyoleta utata; ambapo wahutu waliwekwa kwenye list za watutsi, kuonyesha serikali kutenda haki sawa kwa wote.

Pamoja na vitendo volivyowakera watu, ni michango ya lazima kwa chama tawala.
Pia, chama tawala, kutumia magari na mafuta vya serikali, kiliweza kufika maeneo yote nchi nzima yaliyoandaliwa kwa wanachama kunadi sera zao.

Hali ikiwa tofauti kwa vyama pinzani na wagombea binafsi, kutokana na ukosefu wa mafuta, hali inayoendelea nchi nzima kwa muda wa miaka mitatu (3) sasa.

Chama tawala pia kimepingwa vikali na badhi ya wananchi, kwa kusitishiwa huduma kwa muda mrefu ili wakakusanyike viwanja vya wagombea. Shule nyingi pia zilifungwa kwa muda, huku watoto wakitumika kufanya maonyesho ya maandalizi ya chama hicho, kinachosema mtoto yeyote kuanzia miaka 9 hadi 17, anatakiwa kuwa manachama wa CNDD-FDD.

Zoezi la uboreahaji wa taarifa za wapiga kura na lenyewe liliingia dosari: mpaka sasa, watu wengi waliojiandikisha kupiga kula, walikosa kadi zao.

Kadi nyingine, zililipotiwa kuharibiwa na Imbonerakure katika vituo mbali mbali nchini, jambo linalowapa wasiwasi walio wengi kuhusu utekelezaji wa uchaguzi huru na wa haki.

Ikumbukwe, katibu mkuu wa chama tawala, Revelien Ndikuriyo, siku za nyuma alitangaza kwamba, haitakaa itokee chama chake kikabidhi madaraka vyama vingine, kwa madai ya kwamba vilipopata nafasi hiyo miaka ya nyuma, vilinyanyasa raia wengi(wahutu).

Burundi pia imekuwa ikivifungia cyombo vingi vya habari ambavyo havipo katika mfumo wa chama tawala, huku waandishi wengi wakitekwa na kupotezwa, wengine wakikabiliwa na kesi za uvunjifu wa amani na kutaka kuhimiza raia kujiondoa kwenye mfumo wa chama. Jambo linalowaweka kwenye kundi la wasaliti wa serikali.

Raia wa Burundi waliopo Ubelgiji na Ufaransa wapatao elfu 30, wao wanalalamikia kutofikia na kupewa nafasi ya kushiliki uchaguzi.

Mpaka hapo kesho, tutajua mchakato mzima unaendeleaje.
 
Burundi kaiga kwa kaka yake mkubwa Tanzania
 
kwa WAtumishi tu wa kawaida ndani ya wizara.
Bongo wizara zenye mishahara minono ni zipi bwashee ukitoa wizara ya tamisemi, wizara ya TRA na Wizara ya Ulinzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom