Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa

DAT BOY SU

Member
Nov 15, 2017
29
30
Ni siku moja imepita tangu kuanza kwa uandikishaji wa wapiga wa Serikali za mitaa, kwa watu wote wenye sifa za kufanya hivyo nchi nzima.

Hii ndio sehemu pekee kwa watu wote ambao wanataka mabadiliko au maendeleo ya mtaa mpka nchi kwa ujumla,

Kwanza watu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wanaofaa

Pili vijana tujitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizi za Serikali za mitaa ili kufanya yale ambayo tumekuwa tukiyakemea na kuyataka toka kwa viongozi waliopo madarakani.

Kumekuwa na kasumba vijana wengi kutojiandikisha wala kuchukua fomu za kugombea katika mitaa yetu.

Sisi vijana tumekuwa wakwanza kukimbilia kukosoa na kusema mabaya tu au kuwaachia wazee wagombee sio kama wazee hawastahili kugombea hapna bali nataka tuwape changamoto,

Hatuendi kupiga kula kuchagua viongozi ila tumekuwa wa kwanza kutukana viongozi waliochaguliwa kihalali.

Mwisho kila mtu ajiulize kwanza yeye ataifanyia nini Tanzania na sio Tanzania itamfanyia nini yeye.

Twendeni tukatimize wajibu wetu kwa maendeleo yetu..
 
Niende kupanga foleni kumchagua mwenyekiti wa mtaa? Hawa wanaodhani jukumu lao kubwa ni kukusanya hela za takataka na zile za sungusungu? Oky sawa!
 
Niende kupanga foleni kumchagua mwenyekiti wa mtaa? Hawa wanaodhani jukumu lao kubwa ni kukusanya hela za takataka na zile za sungusungu? Oky sawa!
ndio uwezo wako wa kufikili umeishia hapo...kuwa uyaone kwanza bado u mdogo hujui hya mbambo
 
Back
Top Bottom