Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,730
- 7,979
Nianze kwa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kwa uthubutu na hatimaye kuwaweka katika meza ya majadiliano Kampuni ya Barrick kujadiliana juu ya rasilimali zetu za madini. Hapana ubishi kwamba Makampuni haya ya kimataifa yamekuwa yakitumia udhaifu wetu katika kuvuna utajiri tulio nao. Na hili si jambo jipya. Ni la enzi na enzi tokea akina Carl Peters. Natumai spirit hii itandelezwa kwa Makampuni yote yanayochimba madini katika ardhi yetu na ikihusisha rasilimali nyingine ikiwemo Gas.
Hata hivyo wakati tukipongeza hatua hii, huenda hatua iliyo mbele yetu ndio ngumu na muhimu zaidi ili kufikia lengo lakunufaika na Rasilimali zetu. Tunahitaji timu ya majadiliano ambayo itaweza kusimama na hawa "watata" wazungu ambao wao kiukweli baadhi yao hawana huruma na maisha ya ndege tunayoishi huku wao wakiishi maisha ya kipepo katika dunia hii yetu. Tunahitaji ushirikishwaji wa wataalam wa kimataifa kuungana na Timu yetu ya ndani katika kujadiliana na Timu ya Barrick.
Nashauri tuwapate wataalam mfano Professor Paul Collier wa Chuo Kikuu cha Oxford na Profesa Joel Slemrod wa Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani. Professor Collier ana uelewa wa kutosha wa masuala ya natural resources na Africa kwa ujumla ilihali Profesa Slemrod ana uzoedu wa kutosha wa masuala ya Tax manipulations yanayofanywa na Multinational Companies. Sina maana kwamba nadharau wataalam wetu, hapana ilakuwachukua hawa kusaidia katika ushauri kunaweza kuleta matokeo mazuri zaidi.
Mungu Ibariki Nchi yetu.