Kuelekea Nyerere day; Mama Maria Nyerere akumbusha mshikamano

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
MARIA+NYERERE+PICHA.jpg

Dar es Salaam. Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere amesema wananchi wanatakiwa kushikamana ili kuleta maendeleo nchini.

Mama Maria alisema hayo nyumbani kwake Mikocheni jana wakati kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kinondoni ilipokwenda kufanya usafi wa mazingira eneo hilo ikiwa ni sehemu ya kumuenzi muasisi wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kamati hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wake, Ally Hapi ilifika eneo hilo saa moja asubuhi ikiwa na askari 417 kutoka idara mbalimbali likiwamo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Magereza pamoja na Jeshi la Polisi.

Mjane huyo ambaye alikuwa mke wa rais wa kwanza, aliipongeza kamati hiyo kwa kazi waliyoifanya kwa kuunganisha nguvu na kufanya kazi pamoja.

“Suala la kulinda na kutunza mazingira liwe kichwani. Ukibaki kusema mimi, mimi huwezi kufika mbali na ukitaka kurudi kuwa sisi inakuwa ngumu,” alisema.

“Watu wanapokutana kwa ajili ya usafi wanapata nafasi ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala yanayogusa maisha yao.”

Pia, alipongeza uongozi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kwa kuanza kusahihisha makosa yaliyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

“Lazima tukubali makosa na tujisahihishe. Mambo mengine yanauma sana lakini kujikosoa kutafanya tuendelee mbele,” alisema.

Hapi ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo alisema kupitia kufanya usafi wa makazi hayo ni njia mojawapo ya kumuenzi Baba wa Taifa kwa vitendo.

Hapi alisema Mwalimu Nyerere alipingana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini hivyo usafi ni sehemu ya kuunga mkono vita aliyoianzisha hasa kupinga maradhi yanayotokana na uchafu ya mazingira. Kumbukumbu ya Baba wa Taifa inafanyika nchini kesho.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu naye akapumzike, mshikamano wakati watu wanapigwa risasi. Kuolewa na nyerere (philosopher/ great thinker????) sio warrant kuwa na wewe n great thinker/ philosopher!
 
Hivi makazi ya Nyerere hayafanyiwi usafi hadi ifike Oct? Sio sawa!! Yafaa iwe wanapakumbuka japo wafungwa wawe wanaenda kusafisha kupaka rangi hata mara 1 tu kwa mwezi....sio hadi ifike Oct ......akumbukwe daima JKN....!! Ametutoa mbali amefanya mengi...acha mjane ahudumiwe makosa aliyoyafanya basi haina jinsi tumuache apumzike!!!
 
Huyu mama hana msaada wowote kwa taifa hili ajipumzikie tu hakuna mtu anayemsikiliza hayo maneno yake
 
Wafanye usafi wenyewe.. wachafu sana hawa watu wa hii familia
 
Huyu Bibi anyamaze. Mme wake kuwa Great thinker/Philosopher(???) siyo kuwa na yeye ni Great thinker/Philosopher. Amekemea maovu gani tangu utawala huu uingie madarakani. Anyamaze aendelee kuheshimiwa, asiwavuruge watu.
 
Huyu mama hana msaada wowote kwa taifa hili ajipumzikie tu hakuna mtu anayemsikiliza hayo maneno yake
Huyu inabidi aitwe rasmi mama wa taifa maana naona hawaanzi na maneno 'mama wa taifa'
 
Haya mama.

Mama ana roho ngumu huyu.

Miaka 17 baada kifo cha mumewe bado ana dunda tu.

Na ndipo ninapojiuliza:hivi ni kwanini wanaume tunakufa mapema kuliko wanawake?

Na ukichunguza ndoa nyingi hasa wanandoa wazee.

Kwa asilimia kubwa wanandoa wa kiume wanatangulia mapema kuliko wale wa kike.

Why?
 
Sote twapenda mshikamano lakini msjikamano hujengwa na sio kulazimishwa. Unapotaka kuongea wewe peke yako kweli pana mshikamano hapo? Tena unakwenda kupitisha sheria ili iwe hivyo. Mimi simo.
 
Huyu naye akapumzike, mshikamano wakati watu wanapigwa risasi. Kuolewa na nyerere (philosopher/ great thinker????) sio warrant kuwa na wewe n great thinker/ philosopher!
Mkuu una mawazo ya kibongo typical. Kosa lake yeye ni lipi kuwa mjane wa Mwalimu Nyerere?

Kafuatwa na waandishi wa habari kwa hiyo akae kimya?. Hizo hasira zenu mnaposhindwa kufanikisha mambo yenu muwe mnazimalizia ndani ya kaya zenu na sio kuzisambaza kwa ambao haziwahusu.
 
Mpuuzi wewe nshomile. siongei na nshomile majidai tu
 
Mpuuzi wewe nshomile. siongei na nshomile majidai tu
Acha chuki wewe. Hasira za nyumbani kwako usizihamishie kwa Mama Maria.

Mungu kampa uhai, sasa msitake kuanzisha aina ya ufikiriaji ambao umeficha dhihaka na kebeki kwa watu wenye umri mkubwa.

Uzee pia utakuja kukuhusu, acha kabisa mawazo ya vijana ambao vichwa vyao viliharibiwa na viroba.
 
Uzee is a natural phenomenon ambayo kila mmoja anaweza akaipitia/ au asiipitie. Sitaki unafiki . Watu wanapigwa risasi hakemei, wanapotea kwenye sandarusi hayaoni, hayakemei, hayasemei, leo eti mshikamano. harrasiment za wapinzani hazikemei..., Mshikamano hauji katika hali kama hii. Awe mkweli au anyamaze, tuendelee kumheshimu miaka yote. Asiwe kama Pengo. Umri mkubwa usipokuwa na busara tutakusema, bora unyamaze.
 
Sio kila mtu anatakiwa aongee kwa mujibu wa unavyoiona wewe nchi inaendeshwa.

Wala huna uhuru wa kumuamrisha mtu mwenye umri mkubwa kitu ambacho anapaswa kukiongea.

Kwa hiyo matukio ya watu kupigwa risasi yameanza leo duniani?. Huyo Mama hapungui miaka 85, aliyoyaona katika uhai wake ni mengi kuliko wewe unavyoifikiria Tanzania ya awamu ya tano.

Achana na kauli za dharau kwa watu wenye umri mkubwa, huku JF yupo brother Andrew, pengine kina Madaraka na Makongoro ni members pia. Sasa hizo hasira zako zisiwe ni sababu nyepesi za kuwakosea heshima.
 
Nasema ukiwa mzee ukautumia uzee kutoa comments za kutatanisha, tutahoji. Labda mnaoambiwa nini cha kusema/kuhoji. You just keep silence! Ukiwa public figure lazima watu wakukosoe , watoe maoni kwa sababu tamko lako lina nguvu katika jamii. Tutajadili tamko lako as we are doing now!
 
Back
Top Bottom