Kuelekea ng'ambo ya pili: Dereva amekiri kukata tamaa, akina nani bado wana hamu ya safari?

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
27,536
40,673
Waungwana salam,

Ni mara nyingine tena tukiwa na matarajio ya kuvuka ng'ambo ile basi ni vizuri huku tukitakiana heri tuulizane je akina nani bado wana hamu au matumaini ya safari?

Katika familia baba ambaye ndiye kiongozi wa nyumba siku zote huwa ni nadra sana kukiri kwa familia yake kuwa ameshindwa au anaona ugumu kuongoza familia. kusema hayo ni kukaribisha baba mwingine katika familia.
vivyo hivyo katika jeshi ni mwiko kamanda au kiongozi wa kikosi kukiri kushindwa!! kukiri kushindwa ni kusalimu amri vitani... maana yake ni kusema hakuna tumaini tena zaidi ya kuwekwa mateka....

Baada ya utangulizi huo naomba turudi katika duna yetu halisi... Dreva wa Gari letu ambaye awali alituaminisha na kututia moyo kuwa kazi ya kutuendesha kufika tunakotaka anaimudu... Dereva lionesha ari...moyo na nguvu weli kweli kiasi kwamba kila mtu aliamini atafika safari tena kabla y muda uliotarajiwa.....

Lakini kabla ya mambo kuchanganya dereva wetu alikiri wazi kuwa kazi aliyopewa ni ngumu kwake na anajuta!! ni vigumu sana dereva kukiri hadharani kuwa kazi ya kuendesha chombo inamshinda au ni ngumu.... angalau wa kwetu amekiri hadharani!!! kitendo cha dereva kukiri tena kwa kupiga simu kwa kiongozi mkuu wa kiroho kumwambia kuwa anajuta kukubali udereva na anatamani auache kunatoa ujumbe gani kwetu abiria? kwa wale alioshindwa kupata ujumbe tufuatane.....

1. UCHUMI; Dereva wetu eneo hili limeshamshinda.... hali ya uchumi kwa sasa ni mbaya na hakuna mwenye matumaini ni lini uchumi wetu utakua bora kwa kila mtu.... Duniani kote dereva bora hupimwa kwa kuendesha uchumi vyema.. kwamba afya ya uchumi ndiyo afya ya abiria....
Hali za watu zinazidi kuwa mbaya na purchasing power ktk nchi inashuka sana je hivyo viwanda na bidhaa zake nani atanunua?
Bei za vyakula bado zipo juu, gharama za umee na nishati ya mafuta bado juu, sukari haishikiki na vitu vingine vya msingi kwa watu pia havishikiki Je? dereva aliyekiri awali kuwa kazi ni ngumu amepata tena uwezo wa kuendesha gurudumu hili au ndo basi tena ameamua bora liende? kama ndivyo vipi wanaosubiri kufika? waendelee kuwa na hamu au washuke tu watafute gari lenye dereva mwingine?

2. AJIRA; Mpaka leo ajira imekua kizungumkuti... hakuna ajira mpya... hakuna nyongeza ya mishahara wala madaraja!! Ajira ni moja ya eneo la kuinua hali za watu... mpaka sasa tumeona sarakasi zisizokwisha na hakuna tena mwenye jibu la uhakika wapi tutamaliza hili suala! Je dereva aliyekiri kazi ni ngumu kwake bado ana nguvu ya kutufikisha kule au ndo basi anafanya bora liende? Abiria waendelee na matumaini ya kufika kwa dereva aliyekiri wazi kuwa kazi kwake ngumu?

3. DEMOKRASIA; Hali ya denokrasia imekuwa mbaya zaidi kuliko vipindi vyote je dereva aliyekiri kushinwa bado ana nguvu ya kutufikisha kule kwenye neema ya demokrasia?
4.ELIMU; Kwa upande wa elimu hali ni mbaya sana hakuna tena matumaini ya kuinuka... tukumbuke duniani kote elimu ndiyo ilikua nyenzo ya kuinua maendeleo katika jamii, elimu inayokuza vipaji, ibua ubunifu na kutengeneza jamii iliyostaarabika... najiuliza Tanzania ya viwanda itakujaje bila elimu itakayobeba lengo la viwanda? au hivyo viwanda vitabebwa na jamii hizi ambazo wengine wangali bado na ustaarabu wa kunya maporini wasiojua vyoo ni nini? zaidi ya matamko tu hakuna jitihada zozote zakuinua elimu yenye vichochezi vya fikra mpya na ubunifu!!! Je dereva aliyekiri hali ni ngumu kwake bado tumtarajie kutufikisha kule ambako wenzetu wako leo?

Basi baada ya hayo machache kila mmoja wetu atafakari kwa kina je atafika anakokwenda? Bado ana matumaini? kama anayo ajiulize yatafikiwaje ikiwa dereva alishakiri kazi kwake ni ngumu? Je tuendelee kutumainia kufika ilhali dereva ameshakiri anajuta kuwa dereva?
NAWATAKIA HERI NA FANAKA KATIKA MWAKA MPYA 2017.
 
Umati wa watu utakaojitokeza kesho utapeleka kilio kwa mafisadi.

Wananchi wako tayari kubadili katiba na kumruhusu magufuli awe rais wa milele ili kuyaangamiza kabisa mafisadi wa ufipa.
Ndugu dereva alishakiri kazi ni ngumu kwake. tena kwa kinywa chake na viashiria vya ugumu wa kazi kwake vimeshaonekana je? tutafika vipi mkuu? kuhusu mafisadi tayari waziri wa sheria amekiri mahakama kukosa kesi na hao unaowaita mafisadi wa ufipa hawajafikishwa huko.....
 
Hilo kwa ccm linawezekana kama fisadi mramba kapewa adhabu ya kupiga deki hospitali na kibaka wa techo kafungwa maisha unategemea nini?
Mkuu kama mahakama ya mafisadi imekosa kesi na waziri kukiri hadharani ina maana ajenda ya ufisadi kwa sasa ni furahisha genge.... kama Magufuli anataka kukomesha mafisadi awafikishe mahakamani kuliko kuiacha mahakama hiyo kuwa makazi ya popo!!!
 
Ndugu dereva alishakiri kazi ni ngumu kwake. tena kwa kinywa chake na viashiria vya ugumu wa kazi kwake vimeshaonekana je? tutafika vipi mkuu? kuhusu mafisadi tayari waziri wa sheria amekiri mahakama kukosa kesi na hao unaowaita mafisadi wa ufipa hawajafikishwa huko.....
Akijibu hili namwaga Heineken yangu , nimepiga funda moja tu !
 
Ukazikazini huu sasa ni kero kila kitu ni kupinga tu na kuiombea mabaya serikali mnakera sana. Kwani ilikuwa lazima Rais atoke kazikazini? Tumeshaanza kuwashitukia na agenda zenu za kuligawa taifa.
 
Na kuomba ushauri wa kisiasa kwa kiongizi wa kidini ni dhihirisho tosha kwamba washauri hana huko chamani.

Ni Suala la kanuni: Political problems needs political solutions. Lkn Sizonje yeye anaunda kanuni zake.

Ndio muelewe athari za ugonjwa wa ZIKA uliotangazwa huko Geita namna ulivyo athiri vizazi vya mkoa huo.

 
Ulalamishi tu mwanzo mwisho. Get off your butt and do something useful!
 
Ukazikazini huu sasa ni kero kila kitu ni kupinga tu na kuiombea mabaya serikali mnakera sana. Kwani ilikuwa lazima Rais atoke kazikazini? Tumeshaanza kuwashitukia na agenda zenu za kuligawa taifa.
Ndugu naona unajitahidi sana kupandikiza chuki.... Nasikia ndo plan yenu ya ushindi 2020!! Kujificha kwenye dini na ukabila huwa ndo silaha ya mwisho kwa walioshindwa!!!
 
Na kuomba ushauri wa kisiasa kwa kiongizi wa kidini ni dhihirisho tosha kwamba washauri hana huko chamani.

Ni Suala la kanuni: Political problems needs political solutions. Lkn Sizonje yeye anaunda kanuni zake.

Ndio muelewe athari za ugonjwa wa ZIKA uliotangazwa huko Geita namna ulivyo athiri vizazi vya mkoa huo.

Kazi IPO.... MTU amekiri mwenyewe pasi na kulazimishwa bado wadanganyika wanamtumaini....
 
Back
Top Bottom