Kuelekea miaka mitatu ya Rais Magufuli: Mafanikio ya bandari yaleta matumaini

Ulipo linukuu tu hilo gazeti, tayari umeondoa credibility ya habari nzima.
Huwezi kuvunja credibility ya habari sababu wewe una personal grievance na gazeti. Kama waandishi wamekwenda na kumuhoji mkurugenzi na akawapa hizo data misioni tatizo hapo.
 
Minafikiri ni hatua kubwa inapigwa ukilinganisha na huko tulipotoka na hii inatokana na Rais wetu kuwa firm kwenye suala la bandari na kuchukua hatua mbalimbali. Tukijipanga kwenye bandari tu hii nchi inafika lengo lake la kuwafikia uchumi wa kati na nnaposema bandari simaanishi ile ya Dar es salaam tu na maanisha zote za baharini na maziwa makuu with reference na Reli yetu ya kati na SGR. Naiona TANZANIA MPYA kwa kweli.
 
Ndio msingi wa nadharia ya utoaji huduma, lazima ukae na wadau ili usikilize changamoto zao. Wasingekaa na wadau wangejuaje kama kumbe uwezo wa kufikia mapato ya trilioni 1 siyo ndoto kama wataendelea kuborosha utendaji wao na namna ya utoaji huduma ili waendelee kuwavutia hao waliokimbilia Mombasa na kama hujui mkakati wao jamaa utatimia na wateja wote watarudi sababu jamaa wanatumia mabilioni mengi kweli kwenye kuboresha miundombinu ili bandari iwe ya kisasa.
Naogopa kusema sana nisijejulikana. Ila nawaambieni mimi najua kuliko hilo gazeti. Kitu walichofanikiwa hawa watawala wa sasa ni kupunguza idadi ya wakwepa kodi na watu huwa wanachanganya sana mapato wanayokusanya TRA bandarini na mapato ya TPA.Katika yoote aliyoyasema ni moja tu yuko sahihi sasa hivi ni wao kwa wao tu ndo wanaoinngiza mizigo bila kodi kama yale makontena ya naniliu. Lakini mengine yote wameyakuta yanazidi kuzorota siku hadi siku. Nafikiri katika viongozi wabovu waliowahi kutokea TPA huyo anashika namba mbili akimfuatia Kipande. Na kama wataendelea hivi Mungu atunusuru huko mbele nitakuja tena hapa kuelezea
 
Nimefungua tu kunangalia kama umeweka no. ya simu. Kumbe umesahau... nakukumbushia basi!!!! Hahahaha....
 
Nakumbuka wapigaji na machangu wao walilia sana kisa eti walikuwa hawataki serikali kuleta maendeleo nchini, wao walitaka waachiwe huru ili waendelee kuliibia taifa kama enzi za Kikwete.
 
Mkuu na timu yake wanastahili pongezi sana,nakumbuka wakati ana sweep kelele za wapigaji zilikua nyingi mno

Mkuu ni jambo zuri kwa maendeleo hayo. Je tunaweza kuambiwa deni la taifa limekuwa kwa kiasi gani katika kipindi hicho? Hapa tunaweza pia kupima uwiano wa haya maendeleo na deni letu.
 
Inakuaje mbunge aliyejiuzuru kwa kutaka mwenyewe apewe nafasi ya kugombea upande wa pili?
Kama hujui kusoma, hata picha huioni?
Hakuna mbunge/diwani anayejiuzulu uwakilishi bali hujitoa kwenye vyama vyao tu,uwakilishi unachukuliwa na katiba kwa sab haitambui muwakilishi binafsi,hivyo hana budi kutetea nafasi yake.
 
Mkuu ni jambo zuri kwa maendeleo hayo. Je tunaweza kuambiwa deni la taifa limekuwa kwa kiasi gani katika kipindi hicho? Hapa tunaweza pia kupima uwiano wa haya maendeleo na deni letu.
Anzisha uzi kuhusu deni la taifa,hapa ni kuhusu mapato ya bandari kuongezeka baada ya maboresho
 
tindo said:
Mkuu ni jambo zuri kwa maendeleo hayo. Je tunaweza kuambiwa deni la taifa limekuwa kwa kiasi gani katika kipindi hicho? Hapa tunaweza pia kupima uwiano wa haya maendeleo na deni letu.
Nasubiri jibu la swali hili
 
Nasubiri jibu la swali hili

Hili huwa haliongelewi na wala hawataki liongelewe kabisa. Inajengwa picha kwamba tunafanya mambo haya kwa hela zetu. Mfano mzuri angalia uzinduzi wa hiyo flyover ya Tazara. Wajapani wametoa 92% ya huo ujenzi sisi ni 8% tu, lakini Magufuli anavyotajwa kwenye hilo daraja unaweza kudhani katoa 100% kutoka kwenye mshahara wake.
 
Nyinyi ni waongo sana wakati wiki iliyopita wafanyabiashara walikaa na mawaziri watatu; waziri wa fedha, uchukuzi na viwanda. Wafanyabiashara wanapitishia bidhaa zao kenya, Mombasa leo nawashanga eti mapato yamepaa huu ni uwongo mtakatifu endeleeeni na ujinga wenu
Huna hata aibu hebu pitia takwimu za bandari ya mombasa uone ilivyoporomoka kwenye idadi ya wateja wake,acha uongo

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom