Kuelekea Mei Mosi: Kumwongezea mshahara mwalimu na athari zake

Supervision

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
265
203
Faida ya kuwaongezea walimu mishahara mizuri!Habarini ndugu zangu wa JF.Nimeamua kuleta bandiko langu baada ya tathimini niliyoifanya kwa hawa ndugu zetu walimu.

Bila kupoteza muda naomba nirudi kwenye hoja,faida za kuongezea mishahara waalimu ambazo ni kama ifuatavyo:

01.Kuinua mtu wa chini.Ikumbukwe kuwa walimu wapo kila kijiji hivyo unapoongeza mshahara kwa walimu unaongeza kitu kikubwa.Ujue kama kijiji kina waalimu kumi au ishirini na ukawapa shilingi milioni moja na kuendelea ujue kuna milioni zaidi ya kumi zipo kijijini hapo.Walimu hawa watapeleka pesa zao kwa wafanya biashara wadogowadogo watanunua mafuta ya kupikia,soda,sukari na vingine vingi.Lakini kama haitoshi waalimu wengi hujihusisha na kilimo hivyo wale watu wanaowalimia kupanda na kuvuna watajipatia pesa,na kadiri anavyoongezewa pesa ndivyo atakavyo lima zaidi.

Hapa mtu wa chini atakuwa anajipatia kipato na kuongeza mzunguko wa pesa mjini na kijijini kwani hata mjini waalimu ni wengi zaidi.Watu wanaotegemea ajira kutokana na mishahara ya walimu wataongezeka kwani sasa mwalimu anapata zaidi hivyo anapofanya zaidi katika kilimo au kazi nyingineyo ujue vibarua wake wanaomfanyia huongezeka na kujipatia pesa ama wanaomuuzia vitu watapata zaidi na kupelekea kuongeza mzunguko wa pesa.

02.Kuwaongezea walimu mishahara mizuri kutafanya wengi kusomea ualimu na kufanya walimu wawe kila mahali.Yaani siku zote waalimu hukubali kuwa kinachowafanya wawe chini siyo kazi mbaya,bali hudharaulika kwasababu ya maslahi madogo.Uchumi mdogo huwafanya wadharaulike.

03.Itaongeza hamu ya kazi.Siku zote maslahi humfanya mtu awe tayari kufanya kazi usiku na mchana.Naukitaka kuamini tazama walimu wa private hupenda kazi zao na kufanya kwa mashindano lakini mwalimu huyohuyo wa private aliyekuwa akafaukusha saba ukimpeleka shule za serikali hufanya kazi chini ya kiwango tatizo ni maslahi.


04.Kuongeza pato la taifa kupitia kodi kwani mwalimu anapolima mazao na kuuza ataongeza pato kupitia kodi na akianzisha mradi endapo ataweza kupata pesa nzuri kutokana na mshahara wake ataajiri watu katika mradi wake na kulipa kodi.Kama kila kijiji kati ya waaalimu kumi,watano watafungua biashara basi ajira nyingi zitatengenezwa na kodi kuongezeka.

Jamani hata posho kila katikati ya mwezi kama kada zingine hakuna!Ngoja niendelee;

05.Kuongeza ufaulu.Jamani kuna watu wengi waliingia kazini kwa kuupenda ualimu yaani tulikuwa na mwalimu anafurahia kufundisha hadi raha na anaeleweka ila baadaye akaonekana kukatishwa tamaa.Sasa watu hawa wapo wengi kama mwalimu wa shule ya msingi angekuwa na uhakika wa kupata milioni nina uhakika kunawalimu wangelala darasani wanakesha wakifundisha.<br />SALAMU KWA mama yetu Profesa Ndalichako.<br /><br />

06.Kusaidia mapinduzi ya viwanda nchini.Pale anapopata mshahara mzuri atalima sana yaani kama hupenda kulima pamba atalima mara dufu,kahawa,korosho,miti,na vingine Vingi.Kumbe basi hata malighafi za viwanda zitaongezeka na kuifanya nchi iharakishe katika mapinduzi ya viwanda.Chamsingi ni kufanya kilimo na biashara bila kukiuka sheria za Utumishi wao.


SAIDIA MWALIMU,USAIDIE TAIFA
 
Yaani unapoangalia wingi wa nyumbu then wanaweza kutishwa kwa mngurumo mmoja tu wa simba, dah inashangaza sana.

Kumbe nyumbu wale wangeungana na kuwa kitu kimoja chenye nguvu hata simba hawasogei karibu. Umoja ni nguvu.
 
Kwa maoni Yangu wangebakiza na mishahara hyo hyo ila wapewe incentives kama za majeshi the main reason ni kuwa inflation haishuki reasonably so hakuna faida na kuongezeka kwa mshahara
 
Najua ww pia ni mwalimu ndio maana unajitetea kwa jasho,rejea no1:je yule mwanakijiji asiye na biashara wala chochote yy ni mkulima tu ataipataje hiyo pesa ya mwalimu iliyopo mfukoni mwa mwalimu?
 
Mtoa mada upo good sana ila umekosea haya mambo mazuri mkuu wa nchi hataki kupangiwa yeye anataka yakwake tu tena yale ya hovyohovyo . mkishauri hivi anasema mnampangia so hafanyi. Walimu acheni kusubiri huruma ya huyu jamaa kumbukeni kuongezwa mshahara nihaki yenu na lipo kwenye mikataba mlio sain wakati mnaajiriwa chamsingi fuatilieni hatua za kuchukua mwajiri wenu anapo kiuka makubaliano ya mkataba.
 
Mleta mada hiyo faida ya wengi kusomea ualimu naomba uifute. .Kwasasa wapo walimu mtaani tangu 2015,2016 hawana ajira.Labda useme vinginevyo
 
Acha kuota mchana...mwalimu ni daraja la kuvukia,ataendelea kua alivyo sasa mpaka daima
 
Hahaha hawasikilizwi sababu viongozi wao hawadai nyongeza za mshahara WAP hudai madai halafu hata mwl akigoma waliambiwa hata wagome miaka nane wakirudi watazikuta chaki hahaha bado unadhan watagoma we subiri zero ukiona zimeongezeka ndio mgomo huo maana wakiandamana watapigwa tu kama MTU mmoja kiongozi alivyosema zis means zidumu fikira sahihi za mwenyekiti
 
Walimu walipwe mishahara kwa kadili ya ufahulu wa shule zao hiyo ndo italeta ufanisi wa kweli na kuinua ubora wa elimu Tanzania kwa asilimia 100

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Walimu wanahali ngumu sana, lakini ukiwaona wako smart sana kimavazi

Hongera Waalim
 
Walimu ndo kizazi cha hovyo kabisa katika jamii ya watumishi wa umma. Wao kila siku ni kulialia tu. Hawachukui hatua hata kwa kuandamana tu. Mtakufa na ujinga wenu.
 
Walimu wanaumizwa sn na chama chao kiitwacho CWT. Hakina mwelekeo wala dira na hakijui misingi ya kuanzishwa kwake. Wanakalia kula pesa za walimu tuuuu. Imefikia hatua kila mwalimu anapgia nia maslah yake kivyake. Mfano, Kenya kuna chama cha walimu imara sn na wanaumoja thabiti sn na walimu wanalipwa vzur sn. Huku kwetu n uozo mtupu naomba cag awakague walimu watalilia makato yao.
 
Hawa walimu acha wazidi kusota tena ikiwezekana wapunguziwe mishahara coz wao ndo viherehere kwa kuichagua rangi pendwa ya kijani. Yaani wanasaidia mpaka kuiba matokeo ilimradi kijani ishinde uchaguzi. ACHA WAZIDI KUISOMA NAMBA. Labda wanaweza kushtuka 2020!!!
 
Back
Top Bottom