Kuelekea Kumbukizi ya mwaka Mmoja wa Hayati Rais Dkt. Magufuli naomba Kauli zake hizi ziwe zinachezwa kwa Watanzania na Wageni Waalikwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,920
1. Tanzania siyo Shamba la Bib na kamwe Watanzania msidanganywe na yoyote Tanzania inajiweza yenyewe kwa kila Kitu hata kama Sisi Viongozi hatusafiri Kuzurura huko Kwao

2. Tanzania siyo Masikini na nawashangaa wanaosema ni Masikini wakati ina kila Kitu, Rasilimali zote na imebarikiwa sana na Mungu

3. Nachukia sana Rushwa / Ufisadi na pamoja na kwamba tumeanza Kupambana nao ila bado upo hivyo kama Rais nitakuwa Mkali ili niwapambanie Watanzania Masikini

4. Tanzania si ya Kuomba Pesa bali yenyewe ndiyo ya Kuombwa Pesa na Mataifa makubwa

5. Kamwe sitosafiri nje ya nchi bali Wao ndiyo watanifuata hapa hapa Tanzania Kwangu

6. Watanzania tuna Dharau na Unafiki sana na usidhani kila anayekuchekea au uko nae karibu Wanakupenda kwani wapo wengine wanaotamani hata Ufe ili wafanye yao

7. Leo mtanichukia kwa haya niyafanyayo kwa Tanzania na jinsi ninavyotaka kuwaandaa Watanzania Kiuchumi ili waondokane na Maisha magumu lakini nikifa mtanikumbuka na Nikifa nawaomba mnikumbuke tu kwa Mazuri yangu

Nashindwa kuendelea na Kauli ( Nukuu ) zake zingine kwani naona naanza Kulia kwa Uchungu mkubwa nikimkumbuka Rais wangu Kipenzi ambaye huenda ikatuchukua hata miaka 2000 ijayo Watanzania Kubahatika kumpata kama Yeye Hayati Dkt. Joseph Pombe Magufuli ( JPM )

R.I.P Rais Magufuli tunakulilia nno tu.
 
Rais Magufuli Profesa Wa Siasa, Alitumwa na Mwenyenzi Mungu kupitia Rais Kikwete Kutuonyesha Mapungufu Ya Katiba. Kazi ambayo aliiweza Sana. Kwani alifanya kazi Kwa kutumia upande hasi wa Katiba na kutaja vifungu vinavyompa uwezo jumlisha logic ya kutenda aliyotenda.

Ninampenda na Nitaendelea kumpenda Magufuli.

Wako
Katika Ushirika wa Watakatifu.
 
He was great and ataendelea kuwa hivyo japo hayupo no one to compare.

Hii nchi kuna watu wanafanya yao na pasipo mtu kama Magu hakika ni shida.

"Kuna mtu hapa naskia anashikilia kisima cha wananchi na kuzuia watu kuchota maji, huyo mtu dawa yake ni kumchukua na kumtumbukiza kisimani akitoka humo hatorudia tena" Hayati, 2015 Zanzibar, Nilicheka sana!😀😀
 
Ukisema iwe hvyo itawajengea wananchi hali ambayo baadhi ya makundi nchini hayaitaji wananchi wawenayo ili waendelee kutanua vizuri
 
8. Sisi CCM tunataka Ile ya "nikuteue Mimi, nikupe gari Mimi, nikulipe mshahara Mimi halafu utangaze ushindi kwa mpinzani...hiiiiiiii bhagosha"
Kwa wengine hii pia ni moja ya mazuri ya mwendazake, kauli kama hii ilisaidia sana kuleta "umoja, mshikamano na usawa" katika nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa.
 
Back
Top Bottom