kuelekea digital(Ving'amuzi,TCRA,decode r za mediacom,)

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,339
2,000
habari wandugu,
leo nimekuja na viswali vyangu baada ya kupita website ya tcra na kukosa majibu yakinifu kuhusu huku kuhamia kwa digitali kutoka analojia(digital migration),na maswali yangu ni kama yafuatavyo.
1.je kuhamia digitali kutatunufaishaje sisi watumiaji?
2.kati ya watumiaji na warusha matangazo ni nani anafaidika zaidi?
3.TCRA inafaidikaje kwa kubadili mfumo huu?
4.kuna ulazima sana wa kuhamia digitali?
5.kwa sisi wenye decoder za satellite kama za "mediacom" ina maana ndo mwisho wa kutumia ma dish yetu ya satellite?
6.je ni tofauti gani zipo kwenye hivi ving'amuzi wanavyotaka tununue vinavyozidi satellite dish?
7.je hivi ving'amuzi vinanyakua mawasiliano kutoka kwenye satellite au katika Terrestirial transmission towers(kama za simu),ne je zimeshafungwa kila mkoa/wilaya?

8.Internet Protocol (IP TV–internet) iko supported na hivi ving'amuzi,au miaka kadhaa ijayo watakuja kutuambia tubadilishe tena?


hiyo hapo chini writtten in blue ndo maelezo ya TCRA,nadhani wanaweza wakafanya jambo la maana zaidi zaidi ya jingle yao ya kimafumbo ambayo haieleweki kirahisi na mwananchi wa kawaida,kwa muda huu mfupi uliobaki nawashauri wawe na vipindi maalum ,kama ilivyokuaga ile ya kusajili namba za simu,watu walielewa zaidi.

"JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UZINDUZI WA TANGAZO (JINGLE) NA
WIMBO WA KUHAMASISHA UHAMAJI WA TEKNOLOJIA YA
UTANGAZAJI KUTOKA ANALOJIA KWENDA DIJITALI
1. Wakati Tanzania ikielekea katika ukomo wa kutumia Teknolojia ya
Utangazaji ya Analojia, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania leo
inazindua tangazo (jingle) na wimbo wa kuhamasisha umma
kujiandaa na mabadiliko haya. Tangazo na wimbo unaitwa "Ni
Wakati wa Dijitali Tanzania" vinaanza kutumika rasmi kesho
tarehe 1 Desemba 2012;
2. Tangazo hilo na wimbo vyote vinalenga katika kueleimisha,
kukumbusha na kuhamasisha umma umuhimu na faida za
teknolojia mpya ya dijitali;
3. Tangazo hilo na wimbo vyote vinaelekeza wananchi kutotupa
televisheni zao za zamani kwa kuwa zitaendelea kutumika kwa
kuunganishwa na king'amuzi.
4. Sambamba na kuelimisha na kuhamasisha, tangazo na wimbo
vyote vinasisitiza kuzimwa kwa mitambo ya Analojia tarehe 31
Disemba 2012 kwa mujibu wa kanuni za Mamlaka ya Mawasiliano
kuhusu mifumo ya dijitali za mwaka 2011;
5. Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kusisitiza kuwa wananchi
wanunue ving'amuzi kutoka kwa Mawakala waliosajiliwa na
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na wapate garantii ya
ving'amuzi hivyo;
6. Ni matarajio ya Mamlaka ya Mawasiliano kuwa wananchi na watoa
huduma za dijitali watatoa ushirikiano ili kufanikisha uhamiaji toka
mfumo wa analojia kwenda dijitali.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIAmwisho kabisa,naombeni wenye ujuzi na majibu kwa maswali yangu wanijuze
cc: Young Master MziziMkavu, cielo watu8 Bujibuji Mzee Mwanakijiji Mbuzi Mzee Nicas Mtei Invisible The Boss Mtambuzi Mkuu rombo Boflo
 
Last edited by a moderator:

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,763
2,000
4.kuna ulazima sana wa kuhamia digitali?

​Ili kwenda na utandawazi uliopo inabidi dunia nzima ihame katika mfumo wa kutumia anaelojia katika luninga zao na ili mfumo huo ukamilike ni vema jamii ikahakikisha kuwa lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho ndicho kinatumika katika kubadilisha mfumo ili kuweza kufanikiwa katika ubadilishaji huo.
 

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,763
2,000
1.je kuhamia digitali kutatunufaishaje sisi watumiaji?

​Faida ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia bili ya umeme, kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye luninga yako. Pia itasaidia kuongezeka kwa ajira kwa kuongezeka kwa makampuni mengi ya utangazaji.
 

tembeleh2

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
765
195
Mimi sitaki kujibu maswali yako kwa sababu maswali yote yamejibiwa kwenye vipindi mbali mbali vya TV asubuhi kwenye vituo vingi hapa nchini. Mimi nataka kutoa masikitiko yangu kwa wananchi wa mikoa yote ukitoa mikoa saba ambayo huduma za ving'amuzi zimefika hawatapata huduma ya habari mpaka wawe na madishi. Kulikuwa na uharaka gani wa kuzima mitambo ya analigoa wakati huduma ya digitali haijafika mikoa yote? Nafikiri serikali ina lengo fulani ambali haijaliweka wazi.
 

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,339
2,000
Mimi sitaki kujibu maswali yako kwa sababu maswali yote yamejibiwa kwenye vipindi mbali mbali vya TV asubuhi kwenye vituo vingi hapa nchini. Mimi nataka kutoa masikitiko yangu kwa wananchi wa mikoa yote ukitoa mikoa saba ambayo huduma za ving'amuzi zimefika hawatapata huduma ya habari mpaka wawe na madishi. Kulikuwa na uharaka gani wa kuzima mitambo ya analigoa wakati huduma ya digitali haijafika mikoa yote? Nafikiri serikali ina lengo fulani ambali haijaliweka wazi.
Mimi si mtazamaji sana wa TV mida ya asubuhi,so sijafanikiwa kuviona,imekuwa ni vyema kututaarifu abt hiyo mikoa saba,je ni mikoa gani?
 

SIM

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
1,774
2,000
Mimi si mtazamaji sana wa TV mida ya asubuhi,so sijafanikiwa kuviona,imekuwa ni vyema kututaarifu abt hiyo mikoa saba,je ni mikoa gani?

Darisalama Arusha Dodoma Tanga Mwanza Mbeya Moshi
 

SuperImpressor

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
1,492
2,000
Lakini pamoja na hayo habari njema ni kwamba kwa ile mikoa ambayo itakuwa haijawekewa hiyo mitambo wataendelea kutumia analog mpaka hapo watakapowekewa.
 

meidimu sirkon

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
202
195
Ndg,kama ulivyonunua simu mpaka ukamiliki intaneti kefu hivyo pia dijitali kenye runinga ni muhimu ili kupungusa chenga chenga kwenye mawimbi ya picha na sauti.
 

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
1,500
Tcra upuuzi mtupu utawekaje deadline wakati haujasambaa nchi nzima tena inarudi unaanza kusema ile mikoa ambayo haijafikiwa na digitali itaendelea kutumia analojia huo si upuuzi umeahidiwa nini tarehe 31 dec kuweka deadline wakati bado haujakamilisha.Hamuoni hawa watu wapo kibiashara zaidi na ndio maana wamekimbia kusimika viminara vyao kwenye hiyo mikoa tajwa maana wameona wangelikwenda kwenye mikoa wanayotumia satellite dish wasingalipata wateja kwa wingi.na baada ya hapo 31 mtaona hakuna spidi hiyo tena wataanza kusuasua.
 

tusichoke

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
1,312
1,250
Darisalama Arusha Dodoma Tanga Mwanza Mbeya Moshi

Kwa kuongezea ktk baadhi ya mikoa hiyo saba iliyotajwa wanaorusha matangazo hayo ni wababaishaji wetu TBC wakishirikiana na WACHINA ni full comedy mara no signal mara channel kuhamishwa bila taarifa. Kwa ujumla hawa jamaa ni weupe ktk hii biashara. Iwapo ITV NA STARTV watakuja na ving'amuzi vya aina hii bac hata km itakuwa kulipia ni sh.5000 itakuwa ni wizi mtupu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom