Kiukweli ni moja kati ya matukio yenye kuumiza moyo na kuleta huzuni isiyomithirika hebu vuta picha ni maumivu makali kiasi gani utayapata pale unapogundua kuwa yule uliyeamini kuwa ni malikia wa moyo wako yule ambaye kila siku anakuimbia nyimbo nzuri za mapenzi huku mkiwa watupu kitandani yule ambaye kila siku analalama kuwa maisha yake hayawezi kukamilika bila ya uwepo wako hapa duniani.
Yule ambaye mlikula nae viapo kuwa ni kifo tu ndio chenye haki ya kuwatenganisha kwani muunganiko wenu MUNGU pekee ndiye aliyeuunganisha yule ambaye ulijitoa na kumpigania kwa kila hali kwa ajili yake ili ajae tabasamu usoni mwake,yule ambaye ulimkuta hana mbele wala nyuma na ukaamua kumuinua ili na yeye aonekane mtu kati ya watu, hadi ukafikia hatua ukagombana na ndugu zako au watu wa karibu kwa ajili yake alafu unakuja kugundua kuwa kumbe yale yoote uliyokuwa ukiyapigania kwake hayana maana tena.
Hayana thamani hata chembe ndani ya moyo wake, yale yote uliyokuwa ukiyafanya juu yake ni kama ulikuwa unajipendekeza tu kwake kumbe kuna mtu mwingine anamthamini kuliko wewe uliyekuwa unajitoa kwa ajili yake ukiangalia nyuma umbali uliotoka, muda uliopoteza na hasara ulizopata juu yake unajawa na hasira ambayo inaweza ikakufanya ufanye jambo lolote baya ukifikiria magumu.
Uliyopitia kwa ajili yake unatamani umkate kichwa kwa hasira,ukitazama jinsi alivyokutenganisha na ndugu na marafiki katika kumfanya yeye afuarahi.. unabaki ukimuangalia anavyokucheki kwa dharau huku wewe ukibubujikwa na machozi mengi ya hasira kali, kabla hujaamua adhabu umpe inamfaa ambayo itamfanya na yeye ayapitie maumivu makali unayohisi wewe kwa ajili yake.Ni matukio ambayo usiombe yakukute maishani mwaka.kwani yanaweza yakabadilisha kabisa maisha yako na kuonekana kituko kama sio mwendawazimu mbele ya jamii.LOVE HURTS