Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,707
- 1,729
Wakuu, moja ya mambo yanayoharibu mazingira ya ulimwengu wetu ni kuchoma majani hasa wakati masika inapoisha na kiangazi kuanza. Tabia hii imezidi hasa mkoa wa Tabora kwani hali ya hewa ni hatari watu wanajichomea majani kama ni mashindano vile! Kama ningekuwa kiongozi wa serikali ningeweka sheria kali kwa atakae fanya kitendo hicho. Lakini labda ni jambo la imani kufanya hivo, kama inaefahamu vema tabia hii atujuze na kwa nini mkoa wa Tabora tuu?