Kuchapa watoto

ila mtoto ukimchapa kila wakati mwisho anazowea, anakua haogopi tena

EXACTLY!,....I think the best way ni kutumia akili zaidi badala ya nguvu to come up with effective, non violent ways kuwaelimisha, to me any kind of hitting is violent!, and they're so tiny!, kuwapiga ni kuwaonea tu kusema ukweli.
 
Bila ya kuchapwa nsingefika hapa nilipo, wenzako wengi walikua hawachapwi saivi maisha sio mazuri kwa upande wao

Mkuu you're one of those who, spanking worked!, and you ended up to be a good kid, mbona hata kuna wanaochapwa mpaka kuumizwa and still!, hawakusikia!
 

Kuna watoto ni very manipulative...na very tricky....akijua hakuna kuchapwa..ni usumbufu 24/7....nina relative ambao hawachapi watoto...hawawezi hata kuongea na wageni kwa kitulia...watoto wanataka attention all time...
 
Last edited by a moderator:
ukweli nikua watoto wetu tusipowachapa pale wafapo makosa yanayostahli kuchapwa tunawaharibu.wazazi wetu ni mifano tosha kwetu kwa walivyotulea.ukimwangalia mtoto wa leo na enzi zile tunakua sisi ni tofauti sana kitabia na uwezo wa kiakili.mimi nakumbuka zamani ilikua ukitenda kosa hata huko kwenye kwenye michezo ambapo mzazi pia hakuoni unachapwa na mtu mzima yeyote aliyekuona bila kujali anakujua au hakujui umetumwa na mzazi ukapitia michezo utachapwa na mtu yeyote atakayekuona huko na ukifika hom huthubutu kusema coz utaongezewa kichapo.na kweli tulinyooka na tulikua na uwezo wa kuish maisha.ya aina yoyote nailikua ngumu kumkuta mtoto mtukutu vijijini enz hizo.leo weng wetu tumeyaacha malez hayo tunawalea kwa kuwadekeza eti.ndo kileo sijui tunategemea wakue na tabia njema?hiyo ni ndoto kwakweli tusijidanganye ukweli tunatengeneza kizazi cha nyoka huko mbeleni.zamani biint wa miaka kumi na tano hamjui mwanaume tena ukimtongoza ujipange vizur coz kwanza anaogopa akionekana itakua bonge la.tatizo hom.leo bint wa umr huo ameshatoa mimba kama tano au zaid vipi watoto wake watakuaje vipi wajukuu zake?kwakweli ndug zangu mtoto ni mtoto lazima pale anapofanya kosa umpe adhabu stahki na pia lazima uwe mtu wa kubadilika ucheke nao na kuwafundisha nalezi kwa upendo lakini akienda kinyume mpe adhabu hata badae akikaa aikumbuke ili asirudie makosa pia akuheshimu na kukuogopa pia kua nikifanya hili baba au mama akijua ni balaa.
 
Mkuu you're one of those who, spanking worked!, and you ended up to be a good kid, mbona hata kuna wanaochapwa mpaka kuumizwa and still!, hawakusikia!

Sina maana kwamba utampiga kila siku, ila kila siku ukimgomba kwa mdomo inafika hatua kwwmba anaakuzowea wewe ni msemaji. Ndio maana kuna watoto wengine ukiwatishia paka tu wanalia, ila kuna wengine wanacheza nae. Mtoto ukimfanya aogope kitu gani basi atakua ivo ivo, kucheka cheka na mtoto mpaka hata akiharibu laptop yako bila ya adhabu yoyote kunasababisha tabia mbaya kwa mtoto. Ndio maana unamkuta mtoto hata akienda kwa jirani utaletewa taarifa mara ameharibu hiki mara kile. Na jirani akimgomba kidogo anakuja nyumbani kusema amepigwa na wewe unagombana nao
 

mankachara sio kwamba sikubaliani na adhabu kabisa, I don't agree with physical punishment kwa watoto, na nilisema kitu muhimu ni bora kutafuta njia nyingine ambazo ni non physical kuadhibu watoto kama vile kumpunguzia uhuru wa kucheza au kufanya kitu alichozoea kwa muda fulani, na watoto walivo akiona wenzie au wanacheza au wana enjoy kufanya something they're not allowed to kwa sababu wamekosea, they'll learn from their mistakes. Wanazo akili pia za kufikiria.
 
Last edited by a moderator:
Kuna watoto ni very manipulative...na very tricky....akijua hakuna kuchapwa..ni usumbufu 24/7....nina relative ambao hawachapi watoto...hawawezi hata kuongea na wageni kwa kitulia...watoto wanataka attention all time...

...and if you don't give them the attention they deserve ndo wanakuwa vichwa ngumu, but if you spend enough time to teach them what 'YOU', want them to be?!,they'll definitely turn out the way 'YOU', want them to be!
 
Igeni tu wazungu, watoto wenu msiwachape mtaona tu huko mbele.

Si swala la kuiga au kutokuiga, mfano watoto wanavochapwa mashuleni is daylight abuse
 
Kumchapa mtoto ni LAZIMA na WAJIBU kwangu..! Mtoto lazima achapwe lakini kumuadhibu huko kuwe kwa kumfundisha na kumuomyesha wapi amefanya kosa na alitakiwa afanye nini. Hata hivyo, sio vizuri kumchapa wakati una hasira coz hutafundisha bali utamuumiza, kabla ya kumchapa ni lazima ukae nae umueleze kwa nini unafanya hivyo ili aelewe kosa na sababu za kuchapwa. Pia usimchale mtoto kila anapofanya kosa kwa vile unamfanya awe sugu na asielewe maana ya kuchapwa, most of the time anapokosa tunatakiwa kutumia busara za kuongea na hivyo unaongeza kuwa karibu nao.

Sijutii kuchapwa na wazazi wangu coz they taught me. Na system hiyo nitaitumia kwa wanangu..!!
 
Reactions: kui
....sikumbuki kuchapwa mkuu!, nakumbuka kugombezwa sana but si kuchapwa, and I came out pretty good...lol!
bora kuchapwa kuliko kugombezwa, kwasababu kugombezwa ni psychological torture mbaya sana. viboko vinasaidia na ukiona mtu anasema viboko ni child abuse ujue umagaribi umemharibu.
 
binti yako atakuwa mojawapo ya mambulula wakubwa baadaye, na itamgarimu. acha kuiga mambo ya wazungu, ndio maana watoto wa kizungu wanafikia miaka 18 analeba boyfriend/girlfriend home na anajitangaza bwabwa na wazazi hawala la kumfanya kwasababu uhuru umepitiliza, mwanadamu kwa asili kama asipobanwa na kufinywa kidogo lazima atapotea tu au dunia itamfunza na ni bora afunzwe na mzazi kuliko kufunzwa na dunia kwasababu kufunzwa na dunia atakuja kustuka shuka kumekucha na yeye ameshapata madhara makubwa kabisa. hata wewe unayejiona uko bora, pengine ni kwasababu umefinywafinywa sana na dunia/walimwengu/maisha hadi ukawa experienced. acha kuishi katika nadharia, mlee mtoto katika njia impasayo naye hataisahau hata akiwa mzee, na imeandikwa usimnyima mapigo...fimbo hata vitabu vitakatifu vimeruhusu. you are a duty to raise your child well, otherwise if they get lost you will be the one to blame.
 
binti yako atakuwa mojawapo ya mambulula wakubwa baadaye, na itamgarimu.

Kama sasa hayuko mburula (karushwa madarasa mara mbili na hajawahi kukosa kuwa kwenye dean's list) sidhani baadaye anaweza kuwa mburula.

Shuleni wala nyumbani hana matatizo ya tabia. As a dad I couldn't be any prouder than that.

acha kuiga mambo ya wazungu, ndio maana watoto wa kizungu wanafikia miaka 18 analeba boyfriend/girlfriend home na anajitangaza bwabwa na wazazi hawala la kumfanya kwasababu uhuru umepitiliza,

Oh yeah? Mbona kuna vibaka na majambazi wengi tu huko mavumbini ambao hata hawajafikisha umri wa miaka 18?

Mbona kuna malaya wengi tu huko mavumbini ambao hawajafikisha umri wa miaka 18? Au wewe hujawahi kukutana nao?

mwanadamu kwa asili kama asipobanwa na kufinywa kidogo lazima atapotea tu

Hapana, si kweli muda wote na mara zote. Mbona mimi nilianza kuishi mwenye nikiwa na na miaka 18 na sikupotea? Na kwetu wala sikuwahi kupigwa na wazazi hata siku moja.

au dunia itamfunza na ni bora afunzwe na mzazi kuliko kufunzwa na dunia kwasababu kufunzwa na dunia atakuja kustuka shuka kumekucha na yeye ameshapata madhara makubwa kabisa.

Madhali mtu bado yuko hai ataendelea kufunzwa na dunia. Kila siku mimi najifunza mapya yakiwemo mahusiano yangu na watu wengine. Au wewe ushajifunza yote ya kujifunza na huna tena cha kujifunza?

hata wewe unayejiona uko bora, pengine ni kwasababu umefinywafinywa sana na dunia/walimwengu/maisha hadi ukawa experienced.

Kila aliye hai ana la kujifunza. Kujifunza hakuna mwisho.

acha kuishi katika nadharia,

Kwa taarifa yako mi ndo mayor wa Realville.

mlee mtoto katika njia impasayo naye hataisahau hata akiwa mzee,

Binti yangu ni mwenye tabia njema kabisa na mpaka sasa najivunia kazi niliyoifanya katika kumlea hadi akafikia hapo alipo. Hana tatizo lolote. She is class, grace, and brains personified. I love her more than life itself.

na imeandikwa usimnyima mapigo

Imeandikwa na nani?

...fimbo hata vitabu vitakatifu vimeruhusu.

Sifuati hayo mavitabu ya riwaya za dini mimi.

you are a duty to raise your child well, otherwise if they get lost you will be the one to blame.

Say what....?
 
bora kuchapwa kuliko kugombezwa, kwasababu kugombezwa ni psychological torture mbaya sana. viboko vinasaidia na ukiona mtu anasema viboko ni child abuse ujue umagaribi umemharibu.

Kugombezwa ni psychological torture?!, na si kupigwa?!, mkuu naona kama vile imekaa the other way around, unavomchapa mtoto in your mind you're thinking you're punishing them so that they learn not to do the same thing next time, in their mind with their immature brain they're thinking, this GIANT is trying to hurt me!, unafikiri watajifunza kitu kweli hapo zaidi ya kuumia na kufikiria zaidi maumivu waliyopata?!
And now they're hurt both physically and emotionally!
 

Unampunguzia uhuru kivipi, mtoto unamwambia kalale yeye anang'ang'ania hataki. Sasa utamfanya nini. Unampa kofi moja hajanyamaza ameshalala
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…