Kuchakata Gogo la mbuyu

Tundapori

JF-Expert Member
Aug 12, 2007
649
274
Wakuu salaaaaaam.
Msaada.

Natafuta mtaalam mwenye uwezo na uzoefu wa muda mrefu wa kuweza kuteketeza gogo kubwa la Mbuyu (Baobab).

Mbuyu huu mpaka sasa umeshafikisha miaka miwili tangu umekatwa, ila gogo lake ndo haliozi haraka.
Nimelichoma moto mara kwa mara lakini lipo tu na mimi natamani lioze au lipotee haraka iwezekanavyo machoni pangu. Gogo ni kubwa kama tembo aliyelalia tumbo.

Sina imani na mambo ya kishirikina, na mtu asiniambie mambo ya kutafuta mbuzi au kuku wa kafara, eboo.....

Mwenye uwezo au mbinu salama ya kuliangamiza hili gogo tuwasiliane kwa kuni PM.

Bei ya kulichakata maelewano.

Gogo lipo Dar es salaam kwenye makazi ya watu.
 
Kama bado gogo lipo kwa awamu hii utapata mtaalam ukizingatia vyuma....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom