Tunapokubali kuwa kazi ya kuimarisha upinzani bado ni kubwa, tukubali pia kuwa usalama wa Taifa hili, unaopaswa kusimamia maslahi ya wananchi bado nao unahitaji kuimarishwa kwa kuongezewa ari ya uzalendo. Katika Mchakato huu tulikosea katika kutunga sheria. Laiti sheria ingetamka kuwa Mwenyekiti wa Bunge awe ni mtu asiyetokana na chama cha siasa na awe Jaji wa Makahama Kuu au ya Rufaa, ni dhahiri tungepata Katiba nzuri maana maadili ya Jaji yanafahamika kama kweli akiamua kutenda haki kwa mjibu wa maadali ya nafasi yake. Katiba iliyotawaliwa na ushabiki wa kisiasa, tutapata katiba ya wanasiasa!
Hili la Jaji kuwa mwenyekitii ndoo kabisaaa uozoo...wajua majaji wote ni wateule wa Raisi huku wengi wao wakipewa kama fadhila, ukada na urafikii??
Kosa kubwa hata Rasimi hii imekosa sana misingi ya utawala na maadili yake. Yahitajikaa Katiba itakayojalii sana Maadili na Uongozi hasa upatikanaji wa viongozi kama Majaji, mawaziri, wakuu wa taasisi za umma, usimamizi wa mapato na matumizi ya umma, na rasilimali zetu.