Kuboresha elimu Kigoma Ujiji

Mayor Ruhava

New Member
Dec 28, 2016
1
0
4 Jan 2017

Baada ya kutembelea chuo cha VETA na kukagua miundombinu ya chuo, nimewasiliana na waziri wa ELIMU Prof. NDALICHAKO katika ziara yake fupi ndani ya manispaa ya kigoma ujiji, Amenihakikishia kuwa wakati tukizungumza nae kuwa wizara imeshaingiza kiasi cha Fedha Tsh 160 milioni kwaajili ya ujenzi wa madarasa 8 na Tsh 10 ukarabati wa miundombinu ya shule ya msingi Karuta.
Aidha hazina imeshatoa bilioni 1 kwaajili ya ukarabati wa shule ya kigoma secondary ambayo ilikua ni ahadi ya serikali kuboresha shule kongwe nchini aliyoitoa mnamo mwezi wa 8/2016 katika ziara yake shuleni hapo, Nimatarajio yangu na yawengi kuwa ubora wa miundombinu ya shule hizi itaboreshwa ipasavyo ili kuwa rafiki zaidi kwa kujifunzia kwa watoto wetu.
Sambamba na hilo wizara pia imetoa Bilioni 1 ujenzi wa Grand high school iliyopo KASULU hii nihatua nzuri kwa maendeleo ya ELIMU.

Hussein Ruhava
Mayor Kigoma Ujiji.
 
Back
Top Bottom