Wewe mbona ulipoambiwa una majina kibao hapa JF ukaruka kama kuku? Toa jina lako sahihi na wana JF watapigwa na shock maana unayoandika kwa jina la mwafrika hayaendani na wewe.
JF hailazimishi mtu kujitambulisha kwa majina yake mpaka anapoamua mwenyewe. Hivyo ndivyo walivyofanya watu wengi wakiwemo mwaklinga na Zitto.
Tena naona Mwakalinga kafanya la maana kwa kulikubali na jina analolitumia siku zote za huko nyuma. Sasa kama kuna unafiki wowote nendeni kautafute na tuleteeni hapa ili tu,lime huyo Mtanzania aka Mwakalinga.
Kubenea unafikiri mjinga, kaingia mitini kwasababu hana utetezi juu ya hili. Kwa lugha ya vijana amelikoroga, mwache alinywe.
Gottee,Mwakalinga. Heshima mbele Mkuu. Nichukue nafasi hii kukupongeza kwa nia yako thabiti ya kuwania Ubunge kupitia Jimbo la Uchaguzi la Kyela. Hii ni haki yako ya KIDEMOKRASIA. Full Stop.
Pamoja na pongezi zangu nina machache sana ya kushauri. Unapoingia kwenye siasa mara nyingi unatoa nafasi kubwa kwa jamii ikutazame mbele, nyuma, kulia na kushoto. Pia unapoingia kwenye siasa unakaribisha maadui wengi sana. Yupo jamaa yangu niliyesoma naye shule AMEAPA hataingia kwenye siasa kwa matukio aliyokuwa akiyafanya nyuma hasa tulipokuwa naye 'O' level.
Jina lako sasa hivi si geni tena kwenye masikio ya watanzania. Humu mitandaoni jina lako sasa linatajwa kila mahali, tofauti na nyuma japokuwa umekuwa ni mshirika mzuri tu kuanzia kule TANZANET, Jambo Forums na baadaye Jamii Forums. Utagundua jina lako limepata umaarufu pale tu ilipotangwazwa unakuja Bongo kwa maandalizi ya uchaguzi. Ninachotaka kukushauri hapa kaka ni vizuri sasa hivi yale yote unayoyaongea ukawa unayafikiria mara mbili mbili. Pamoja na 'uzushi' wote wa Kubenea dhidi yako hukustahili 'kushabikia' ile asidi aliyomwagiwa kaka. Wewe unataka kuingia pale 'mjengoni' ili uwe mtunga sheria. Hizo sheria nani atazilinda kama wewe mtunga sheria mtarajiwa unaona 'kudhalilishwa' kwako na Kubenea hakuhitaji tena sheria ya kumlinda zaidi ya kumwagiwa zile 'pili pili manga'? Inshallah Mungu akikujalia ukaja kwenye Kampeni utawakuta akina 'Kubenea' wengi tu huku. Hivi kuna mtu alichafuliwa jina kama Salimu Ahmed Salim? Angekuwa na 'mzuka' kama wako basi angetupa 'Hiroshima' na si Tindikali maana hao 'wachafuzi' walikuwa wengi mno!
Jambo jingine ndugu yangu ni vema ukawa makini sana na timu yako. Kwa maelezo yako mwenyewe ni wazi kuwa uko karibu sana na Mheshimiwa Mwakipesile. Kwa asilimia nyingi unajua kuwa hatagombea uchaguzi. Unajua kuwa kila Ijumaa anatoka Mbeya na kwenda Kyela na kurudi mwisho wa wiki. Unajua kuwa familia yake ipo Kyela tangu amewachaguliwa kuwa RC wa Mbeya. Ningekuwa mimi wewe ningejaribu sana kujipambanua kama sio kujiweka mbali na Mwakipesile. Nina wasiwasi unaweza kuja 'kuzoa' kura za Mwakipesile badala ya za kwako.
Wengi tunaamini kabisa Mwakipesile ni mwanamtandao. Kuwa karibu naye kutaashiria kabisa kwamba na wewe ni mwanamtandao au mwanamtandao mtarajiwa. Hili ndilo limepelekea wewe kuonekana uliamua kwenda Arusha kumuona EL ambaye kimsingi ndiye anaaminika kuwa kinara wa Mtandao Mafisadi hata kama ulikwenda kwa masuala yako binafsi. Ukaribu wako na Mwakipesile unaonekana kabisa kuwa umeletwa kuja 'kumwangamiza' Dk Mwakyembe. Jitengeneze uonekane kama Mwakalinga na si Mwakipesile. Kwa umri ulionao sio lazima mwakani uingie 'Mjengoni'
Wamejitokeza watu wengi sana humu kukutetea na kumwangamiza Kubenea. Ni vema ukajipambanua nao. Waache waseme wao. Wewe wasikilize. Usijiunge nao. Leo wanaweza wakaonekana ni wazuri kwako na wewe ukawasifia lakini watakuja kukugeuka na kuanza kusema 'mijineno' ambayo itaonekana kama wewe ndiye umewatuma waseme. Wale wote ambao ni jamaa zako waambie kabisa wewe hutaingia Bungeni kwa kumchafua Dk Mwakyembe kama ilivyo yeye hataingia bungeni kwa kukuchafua wewe. Waambie kabisa kazi ya kumuondoa Dk Mwakyembe pale Kyela ni ngumu sana inahitaji mkakati mzito na si 'vijineno' tunavyovisikia humu kwa desturi ya watu wa Kyela ninavyoijua.
Mwisho niwaulize wanajamii wenzangu, mbona hili la Kubenea kuja kujieleza 'limevaliwa njuga' sana wakati humu humu kuna 'wazushi' ambao huwa wanakuja na kuja nayo wakibanwa wanapotea halafu unawakuta kwenye thread nyingine wametulia tuliiiiiiii wanapiga miluzi kama sio wao?
Mwishoni nakukaribisha mwanangu tena uje Kyela ila elewa tu Dk Mwakyembe ni 'jiwe' kweli kweli hakikisha unakuja na 'fataki' maridhawa. Utakuwa umesikia matukio yaliyotokea siku za nyuma kwa watu walioingia kichwa kichwa. Njoo na SERA nzuri watu watakuelewa na usisubiri ile ile ILANI isiyotekelezeka ambayo hutungwa na 'vizee' ambavyo hata masikio yamechoka kusikia na yakisikia yanasikia kinyume, vitasikiaje wakati muda wote pale 'mjengoni' vinakuwa vimembonji kwa hiyo usikivu wao uko kindotondoto zaidi!
Mwakalinga. Heshima mbele Mkuu. Nichukue nafasi hii kukupongeza kwa nia yako thabiti ya kuwania Ubunge kupitia Jimbo la Uchaguzi la Kyela. Hii ni haki yako ya KIDEMOKRASIA. Full Stop.

Gottee,
Nashukuru kwa ushauri wako wote. Ila hilo la Mwakipesile naona umekimbilia kwenye conclusion ambayo ni wrong. Mimi ni mdau wa siasa za Kyela kwa muda sasa na nawajua wahusika wote kwa undani hata kwa wale ambao sio marafiki.
Hata ukiniuliza habari za Mwakyembe nitaweza kukuandikia zote zile ambazo ni public hata kama sijaongea na Mwakyembe kama miaka minne sasa.
Habari nilizo nazo za Mwakipesile ni zile ambazo kila anayefuatilia habari za Kyela anajua. Unless hauko Kyela lakini kama uko Kyela ninaamini utakuwa na hizo habari.
Baada ya kusema hayo napenda niweke msimamo wangu wazi. Namfahamu Mwakipesile siku nyingi tokea alipokuwa mbunge wa Kyela. Yeye alikuwa hanifamu na tumeonana uso kwa uso mara moja ambayo ni mwaka huu nilipokuwa TZ. Nimewahi kuongea naye kwa simu mara kadhaa sikumbuki idadi ila haizidi mara tano. Sina ugomvi naye wala sina sababu ya kuficha kwamba namfahamu. Ila sidhani pia ni sahihi kusema niko naye karibu sana. Watu nilio karibu nao, naongea nao karibu kila wiki. Nitaendelea kuwasiliana naye sawa na mwana Kyela mwingine yeyote. Siwezi kumkataa au kumruka mtu kwasababu tu eti ni mwana mtandao, kama ni hivyo bora nikose huo ubunge na nitakuwa happy kufanya shughuli zangu zingine. Ungeniambia Mwakipesile ni jambazi au ni mhalifu, hapo ningeogopa hata kumsogelea, lakini kuniambia ni mwana mtandao, nikae nae mbali naona ni ushauri ambao hautanisaidia mimi, hauisaidii Kyela wala TZ
Ya Mwakyembe nayajua maana tulikuwa kambi moja 2005. Wacha mpambano ufike na ngoma iwekwe kati tayari na kwa mechi kuanza.
...............Jina lako sasa hivi si geni tena kwenye masikio ya watanzania. Humu mitandaoni jina lako sasa linatajwa kila mahali, tofauti na nyuma japokuwa umekuwa ni mshirika mzuri tu kuanzia kule TANZANET, Jambo Forums na baadaye Jamii Forums. Utagundua jina lako limepata umaarufu pale tu ilipotangwazwa unakuja Bongo kwa maandalizi ya uchaguzi. Ninachotaka kukushauri hapa kaka ni vizuri sasa hivi yale yote unayoyaongea ukawa unayafikiria mara mbili mbili. Pamoja na 'uzushi' wote wa Kubenea dhidi yako hukustahili 'kushabikia' ile asidi aliyomwagiwa kaka. Wewe unataka kuingia pale 'mjengoni' ili uwe mtunga sheria. Hizo sheria nani atazilinda kama wewe mtunga sheria mtarajiwa unaona 'kudhalilishwa' kwako na Kubenea hakuhitaji tena sheria ya kumlinda zaidi ya kumwagiwa zile 'pili pili manga'? Inshallah Mungu akikujalia ukaja kwenye Kampeni utawakuta akina 'Kubenea' wengi tu huku. Hivi kuna mtu alichafuliwa jina kama Salimu Ahmed Salim? Angekuwa na 'mzuka' kama wako basi angetupa 'Hiroshima' na si Tindikali maana hao 'wachafuzi' walikuwa wengi mno!
...........................................Mwakipesile ni mwanamtandao. Kuwa karibu naye kutaashiria kabisa kwamba na wewe ni mwanamtandao au mwanamtandao mtarajiwa. Hili ndilo limepelekea wewe kuonekana uliamua kwenda Arusha kumuona EL ambaye kimsingi ndiye anaaminika kuwa kinara wa Mtandao Mafisadi hata kama ulikwenda kwa masuala yako binafsi. Ukaribu wako na Mwakipesile unaonekana kabisa kuwa umeletwa kuja 'kumwangamiza' Dk Mwakyembe. Jitengeneze uonekane kama Mwakalinga na si Mwakipesile. Kwa umri ulionao sio lazima mwakani uingie 'Mjengoni'
.....................!
Kwa vile kuna kundi la watu ambao wanaamini kabisa kuwa hakuna mtu mwingine yoyote (ndani ya CCM au nje yake) ambaye anaweza KUIONGOZA WILAYA YA KYELA (kuliongoza Taifa letu na kuwa Tanzania) bila ngwe ya pili ya Mwakyembe (Kikwete) haiwezekani basi CCM na mashabiki wa utawala bora wa Mwakyembe (Kikwete) waamue kubadilisha Katiba ili waondoe vikomo vya utawala na ikiwezekana wapitishe uamuzi wa kumtangaza Mbunge Mwakyembe kama Mbunge wa Maisha wa Kyela (Rais Kikwete kama Rais wa Maisha wa Tanzania.)
Kwa kufanya hivi angalau tutajua tugombee mambo ya UDIWANI (ubunge) tu kwani Ubunge (Urais) tayari una mwenyewe!
.- Saafi sana mkuu, tupo pamoja sana.
Respect.
FMEs!
Sikonge,Kyela Devcelopment Corporaiton (KDC)
Kuna nyepesi nyepesi zinasema kuwa hii kampuni amenunua Mbunge mmoja wa Wilaya iliyopo Mbeya. Bado niko katika kuwasiliana na mpashaji wangu habari. Mara nikipata habari ni Mbunge gani kanunua na kwa shilingi ngapi basi nitakujulisheni. Jamaa kapania kufungua hata KTV yaani Kyela TV.
Mfanye Subira na nitakujulisheni siku si nyingi.
Shetani ILAANI KYELA kwa watani wangu.
NB: Shalom, habari za siku Rabin. Umepotea kabisa kama makalio ya nyoka. Heri za Mwaka mpya kabisa mkuu maana natimka.
..
Mkuu fmes,
Juhudi za kumpata mtu makini Kubenea zimeshindikana?
.
Mkuu Sam.
1.Yule mjinga anayejiita Mwafrika or Solomon David or Mzee Mwanakijiji amesema hii ya Mwakalinga ni Low level na hivyo Kubenea hawezi kuja kuijibu.
2.Kwamba alijibu ya Zito kutokana na kuwa ilikuwa high Level.Ndiyo msomi huyo na anatumia muda wake mwingi kuikosoa serikali uku kichwani mwake ni mtupu.
3. Kwa hiyo inawezekana hata Fmes naye anataarifa hizo kuwa huyu Kubenea hawezi kujibu shutuma zidi ya Mwakalinga.
4.Fmes, alikuja kwa kumuomba sana Kubenea kujitokeza na sasa Fmes amebaki kuwashukuru tu wachangiaji bila kutujulisha juhudi zake za kumtafuta Kubenea zimeishia wapi.
5.Ufisadi uko kila pahali,kuanzia kwenye serikalini Media za akina kubenea na mpaka hapa JF.
Kyela Devcelopment Corporaiton (KDC)

Yule dogo ameowa juzijuzi kwenye familia ya Mwakyembe.
Sasa huwezi kuwashitaki Wakwe zako. Unafahamu tena kama penzi limekukolea.
Aliomba mwenyewe kufuta kesi ya utekaji. Sijui ni Binti alimghiribu??
.
Mkuu Sam.
1.Yule mjinga anayejiita Mwafrika or Solomon David or Mzee Mwanakijiji amesema hii ya Mwakalinga ni Low level na hivyo Kubenea hawezi kuja kuijibu.
2.Kwamba alijibu ya Zito kutokana na kuwa ilikuwa high Level.Ndiyo msomi huyo na anatumia muda wake mwingi kuikosoa serikali uku kichwani mwake ni mtupu.
3. Kwa hiyo inawezekana hata Fmes naye anataarifa hizo kuwa huyu Kubenea hawezi kujibu shutuma zidi ya Mwakalinga.
4.Fmes, alikuja kwa kumuomba sana Kubenea kujitokeza na sasa Fmes amebaki kuwashukuru tu wachangiaji bila kutujulisha juhudi zake za kumtafuta Kubenea zimeishia wapi.
5.Ufisadi uko kila pahali,kuanzia kwenye serikalini Media za akina kubenea na mpaka hapa JF.
Kubenea,
RC Mwakipesile anasema alikupigia simu na umeomba msamaha kwa kumchafua, je ni kweli? Kama ni kweli si njoo uandike hapa JF badala ya kuomba msamaha kwa chini chini?
Alikuwa anahutubia baraza la madiwani la halmashauri ya Kyela.
Pia aliongelea madai ya kwamba yeye anajiandaa kugombea ubunge. Amekanusha vikali na kusema alikuwa mbunge miaka 10 na sasa kapewa cheo kikubwa zaidi, atakuwa mjinga kurudi kung'ang'ania ubunge wenye matusi kibao.
Lingine alifanya utani kwa kuwaambia wajumbe hakujua kumbe ana mtandao mkubwa sana ambao umefika mpaka London? Kama ana uwezo wa kumchomoa mtu London na kumleta Kyela, hayo ni mafanikio makubwa sana.
Lingine aliongelea kuhusu kufukuzwa kazi kwa mwenyekiti wa halmashauri. Alisema yeye na Tamisemi wameridhia, hivyo mzee Kisugujila ndio hivyo kitumbua kimeota mchanga.
Habari ndiyo hiyo, nimewaambia waandishi waliokuwepo wanipatie copy na kama wataleta nitawatumieni.
Mkuu Kubenea,
Najua ni mwana JF; hata kama una mapenzi na mtu mmoja kwenye siasa za Kyela lakini magazeti yako hayana haki kuingia kuchafua watu wengine bila sababu zozote. Ulichoandika kwenye makala hii hasa kuhusu Mwakalinga ni majungu na uongo mtupu. Nitafafanua zaidi hapo chini.
.
Mkuu fmes,
Juhudi za kumpata mtu makini Kubenea zimeshindikana?
- Zikishindikana nitakuwa mtu wa kwanza kusema, nenda tena utizame maneno yangu huu ni msimu wa Holidays, watu wako bussy na hakuna haraka anyways, asipopatikana kabisa nitasema mwenyewe.3. Kwa hiyo inawezekana hata Fmes naye anataarifa hizo kuwa huyu Kubenea hawezi kujibu shutuma zidi ya Mwakalinga.
4.Fmes, alikuja kwa kumuomba sana Kubenea kujitokeza na sasa Fmes amebaki kuwashukuru tu wachangiaji bila kutujulisha juhudi zake za kumtafuta Kubenea zimeishia wapi.
Unataka kusema kuwa Mwakalinga na Rostam Azizi wana ushirika wa mapenzi ya ndoa?