Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Kubenea: Lowassa ameonesha njia

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Saed Kubenea

HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.

Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.

Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.

Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.

Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.

Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.

Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.

Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.

Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.

Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.

Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.

Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.

Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.

Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.

Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.

Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.

Mwisho
 
Hata mkileta maelezo marefu vipi, Lowassa bado sio mtu sahihi kuwepo cdm. Anaweza kurudi tu ccm na kutoa huo ushauri wake mzuri akiwa huko. Ama anaweza kwenda hata TLP na kuongeza nguvu huko na hizo siasa zake. Watavuna watu wengi tu tunaombiwa walimpa kura mpaka cdm ikapata wabunge wengi.
 
Huyo jamaa anawabipu ukawa kujionesha yeye bado ni hot cake, kifupi anatingisha kibiriti, ili ukawa wamtetemekee, huyu jamaa hafai anataka kuleta siasa za mrema, za kuabudiwa.

Anataka afukuzwe ili agome
Kufukuzika moto uwake Kama NCCR ya Miaka ile
Ulipo tupo vs Bavicha
Wanamtandao wanataka kuteka Chadema baada ya kushindwa huko CCM
 
Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.

Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.

Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.

Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.

Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa Cuf.

Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.

Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.

The remaining part of the story sina interest nayo, mi naangazia hayo maneno yenye rangi nyekundu

Sitaki kuamini kuwa CCM, Usalama wa taifa hadi Jakaya walikuwa hawajui

Kama ni kweli basi hiyo ni hatari kubwa sana
 
Hata mkileta maelezo marefu vipi, Lowassa bado sio mtu sahihi kuwepo cdm. Anaweza kurudi tu ccm na kutoa huo ushauri wake mzuri akiwa huko. Ama anaweza kwenda hata TLP na kuongeza nguvu huko na hizo siasa zake. Watavuna watu wengi tu tunaombiwa walimpa kura mpaka cdm ikapata wabunge wengi.
Mlipeni kwanza pesa zake alizowekeza Chadema. Msilete uhuni wa kumdhulumu mamvi.
 
Mlipeni kwanza pesa zake alizowekeza Chadema. Msilete uhuni wa kumdhulumu mamvi.

Hilo halina shida maana hakuianzisha cdm yeye bali aliikuta tena ikiwa kwenye hali nzuri ile mbaya. Lakini baada ya yeye kuingia hapo ndio chama kikaanza kuingia nuksi. Aonyeshe kiwango cha mauziano aliyofanya tena kwa EFD receipt na terms za hiyo biashara, wanachama na sisi washabiki tuonyeshwe. Kisha tutaamua tulipe kulingana na faida aliyoingiza huku tukipima madhara aliyoiletea cdm. Ila kama alifanya biashara ya kitapeli itabidi aondoke na waliopeana naye hizo hela. Una lingine?
 
Back
Top Bottom