Kubenea awaonya wanaopiga ramli kuhusu hatima yake CHADEMA, azungumzia Virusi vya Corona

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,222
15,073
"Nataka wananchi wenzangu wa Ubungo na Dar es Salaam pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi zinapaswa kuungwa mkono na jamii ili wananchi wajue madhara ya ugonjwa huu wa Corona tufuate ushauri wa wataalam.
EUlgKtTUUAAc-Ic.jpg


Kuna hatari za kiafya kutoka nchi tajiri duniani juu ya gonjwa hili la Corona sembuse sisi?, Mungu atunusuru na haya mambo ya kufanya mzaha.

Nimshukuru Spika Ndugai kwa kupunguza idadi ya wabunge Bungeni ametumia mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba kulinda afya za wabunge lakini haitoshi, ni vizuri bunge likafungwa kama maambukizi yataendelea, kuokoa maisha ya watu.

Mapato ya serikali yanategemea kodi na mapato makubwa ni ya utalii, tutegemee uwepo wa mdororo wa uchumi duniani kwa sababu ya gonjwa hili.

Huu sio wakati wa kurushiana vijembe na kuonyeshana ubabe, hii vita vi yetu sote, wakati wa vita ya Kagera, Taifa lilikuwa pamoja na huu ugonjwa ni lazima tushikamane pamoja kuhamasisha jamii inaelimika na Serikali isaidie.

Inawezekana taarifa zinazotolewa sasa sio za kweli kwa sababu kuna shida pia ya utambuzi ambayo ni jambo serious kabisa, serikali iwekeze katika maeneo ya kuhudumia wagonjwa.

Ni jambo jema shule zilivyofungwa kwa sababu mzazi unakuwa karibu na mwanao lakini kwa misongamano iliyopo kwenye madaladala unaona bora huyo mtoto angebaki shuleni.

Baada ya Anthony Komu kutangaza kuondoka Chadema yamekuwepo maneno mengi nikitajwa na mimi nitamfuata Komu, Komu ni ndugu yangu kabisa, lakini urafiki wangu na Komu haunifanyi kila anachofanya nami nifanye, mimi bado mbunge wa Chadema.

Mimi nimeshaenda mahakamani mara nyingi sana, lakini inategemea na nafasi yangu na mimi naamini sio lazima watu wote kukusanyika katika tukio moja, mimi nashiriki kwenye shughuli za Chadema, sina shida na chama na nipo pamoja na viongozi wangu," Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
 
Ningeshauri kuweza kupambana na Corona kukatwa kwa wabunge, wakatwe asilimia 80% ya mishahara yao wakiwamo mawaziri, makatibu na wakurugenzi wa mashirika kuweza kupatikana fedha za ku saidia corona,country lock down kama ikitokea na misaada mingine.

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh Kubenea amekiri urafiki, ukaribu na undugu wake na Komu, lakini amesema kwamba si kila alifanyalo Komu na yeye aweza kufanya.Ameonya kwa Msisitizo mkubwa sana kwa watu kuacha kupiga ramli.

Amedai kwamba hana mpango wa kuhama Chadema wala hana sababu ya kufanya hivyo.
 
Mh Kubenea amekiri urafiki , ukaribu na undugu wake na Komu , lakini amesema kwamba si kila alifanyalo Komu na yeye aweza kufanya . ameonya kwa Msisitizo mkubwa sana kwa watu kuacha kupiga ramli .

Amedai kwamba hana mpango wa kuhama Chadema wala hana sababu ya kufanya hivyo .
Ni jambo jema!
 
Haya sasa nyumbu waliokuwa wanatukana baada ya kusikia jamaa ataongea na waandishi wa habari wanajisikiaje sasa hivi?
 
Kubenea anapitia wakati mgumu sana kisaikolojia, kwa sisi tuliokuwa viongozi ndani ya Chadema tunajua, Hapa niseme ukweli kwa kubenea anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa za kisiasa, kiuchumi na kijamii pia.

Kiukweli ndani ya chama chake hayupo vizuri kabisa lakini kwenda upinzani kama rafiki yake Komu anaona hapana na kuingia CCM inamuhuuma kwani alikuwa na mahusiano mbabaya na watu wa kule kama ugonvi wake na Makonda na wengine, Kubenea kupiga goti kwa Makonda kwake ni kitu kigumusana na hii kutokana na tabia yake.

Ndani ya chadema kuna Redbregedi Nyekundu hii uwa inachapa sana, sasa Kubenea anaogopa hayo pia kwani hana ujasiri hivyo anapooza rejeta iliyopasuka.

Pia nilazima afanye hivyo kwani anajua fika kuwa chama chake kina mtu anayekimiliki hivyo hapendi akutane na maswaibu yoyote. Mmiliki ni mmiliki tu hivyo anajua anaweza kuhukumiwa nje ya katiba kama wengine kwani anajua hilo.

Lamwisho ni kuwa Kubenea alijipambanua kama mtu wa misimamo na jasiri asiye yumbishwa wala kushindwa na alipania sana kuwa msemaji wa tofauti pindi atakapokuwa mbunge lakini akakutana na vitu vingine tofauti zaidi kuona kumbe hata chama chake kinamziba mdomo sasa aelewi afanye nini.

Mimi namshauri Kubenea kuwa tunamkaribisha CCM na kama anaona haya kuonana na Makonda na wengine anitafute mimi nita simama kumuombea msamaha kwa yote aliyotukana kwani sisi tunaitaji wanachama kilasiku ntampeleka kwa Bashiru na kumwita Makonda mgonvi wake wasameheane hili tujenge nchi asiogope.

Upande aliopo si salama kabisa kwani ametumika kama mpira wa kiume tu, njoo kamanda nchi inakuitaji si Chadema inakuitaji mzee.
Is me man Daza karibu.
 
Ningeshauri kuweza kupambana na Corona kukatwa kwa wabunge,wakatwe asilimia 80% ya mishahara yao wakiwamo mawaziri, makatibu na wakurugenzi wa mashirika kuweza kupatikana fedha za ku saidia corona,country lock down kama ikitokea na misaada mingine.... Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika maslahi yao CCM na upinzani wanaungana tena wanakuwa na hasira za kufwa mtu. Wakatwe 80% thubutuuu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom