WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 457
RAGE ALISAMBARATISHA TAWI LA SIMBA LA MPIRA PESA
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Rage amelifunga Tawi la wanachama wa timu hiyo linaloitwa Mpira Pesa kwa madai ya kukiuka katiba ya klabu hiyo, pia amevunja kamati zote ndogondogo za timu hiyo.
Rage pia amemfuta uanachama mwenyekiti wa Tawi la Mpira Pesa, Awadhi Masoud pamoja na Ali Bane kwa madai ya kutoa siri za klabu pamoja na kufanya ubabaishaji kwa kutumia risiti feki na kushindwa kulipa ada ya uanachama kwa miaka miwili mfululizo.
Uamuzi huo wa Rage kulifuta uanachama tawi la Mpira Pesa umekuja siku chache baada ya viongozi wa tawi hilo kuomba wanachama 698 wa Simba kujitokeza kusaini fomu ili kuitisha mkutano wa dharura kwa lengo la kujadili matatizo ya klabu hiyo pamoja na kutokuwa na imani na uongozi wa sasa.
Wanachama hao waliunda kamati ya kukusanya saini hizo wakiongozwa na Bane (Mwenyekiti), Masoud (Katibu) na wajumbe Hamis Omar, Chuma Suleiman, Said Kubenea, Mkoma Hamis, Sophia Lubuva na Omari Mnkonje.
Rage alisema,"Kuna baadhi ya wanachama siyo waadilifu na wapo kwa ajili ya kuleta migogoro ndani ya klabu yetu. Nilichoamua na kamati yangu ni kufuta Tawi la Mpira Pesa pamoja na watendaji wake."
Alisema,"Kama wanataka kuwa wanachama tena wanapaswa kujiandikisha upya, lengo hasa ni kumaliza tabia za udanganyifu zinazofanywa na watu wachache."
Source; Rage alisambaratisha Tawi la Mpira Pesa - Michezo - mwananchi.co.tz
My Take:
Kubenea amekata tamaa na kurudi tena kwa Gazeti la Mwanahalisi sasa anataka kusaka uongozi ndani ya Club ya Simba?