KUBENEA arejea amesalimu amri?

Status
Not open for further replies.

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Mkurugenzi/Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, Saed Kubenea, amerejea jana jioni akitokea nchini India alikokuwapo kwa takribani mwezi mmoja akipata matibabu ya macho yaliotokana na kuvamiwa na kumwagiwa tindikali, ofisini kwake Januari 05 mwaka huu.

Je, baada ya kufungiwa na baada ya kuendelea kuuguza macho na baada ya kupata kibano cha polisi, Kubenea na MwanaHalisi lake watarudi na kasi ile ile ama wamesalimu amri kwa mafisadi?

Gazeti la MwanaHAlisi litarudi mitamboni Januari 14 Mwaka huu, JF tuna mchango gani kwao? Je, litaibuka na habari nzito ama litaingia kutetea mafisadi?

i210_Kubearrival.jpg
 
najua tumechoka, lakini lazima tujue kutokuwapo MwanaHalisi ni pengo. Na kuna mpango wa kutaka kuongeza kifungo
 
Kubenea usiogope,endelea kuwachachafya mafisadi,Watanzania msikubali kabisa ubakaji wa uhuru wa vyombo vya habari.Tanzania itakombolewa na watu kufuatilia mustakabali wake na kukataa ukandamizaji.Mwanahalisi ina wapenzi wengi kiasi kwamba lilipofungiwa wamefadhaika sana ila kwa vile ni wapole wameendelea kusubiri lakini uonevu ukiendelea uvumilivu utakoma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom