Maneno ya Said Kubenea ndio yaliyomharibia Lowassa

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Shombo za kubenea zimeharibu ndoto ya Lowassa kuharibu ni rahisi kuliko kuunda, kutambua hili haihitaji kurejea nukuu ya mwandishi mkubwa wa vitabu raia wa Czech, Ivan Klima. Ila unachopaswa kuzingatia ni kuwa kuharibu ni kuunda, kuunda ni kuharibu (To create is to destroy, to destroy is to create).

Mantiki; Huwezi kuunda kitu pasipo kuharibu kingine. Tofali haliwi mpaka mchanga, saruji na maji viharibiwe. Na unapoamua kuharibu, vilevile unaunda kingine, ulikuwa na nyumba imevunjwa, kimebaki kiwanja. Hiyo ni kanuni!

Unapomshughulikia mtu kumchafua, huishii kumharibu. Badala yake unajikuta unampa wasifu mwingine. Alionekana mtu mzuri, wewe unavumisha kuwa ni mwizi, ile heshima aliyokuwa nayo inaondoka, sifa yake mpya ni mwizi.

Edward Ngoyai Lowassa ana mengi ya kuumiza. Ndoto za Ikulu hazipo, zimepotea, sizioni zikiwa hai (sizungumzii ubishi wa sasa). Msisitizo wangu upo palepale, inahitaji majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kwa uhai na afya, ipo siku inawezekana Muumba akitaka.

Maisha bila unafiki yanawezekana, yapo mambo inabidi kuyasemea waziwazi. Lazima kumkumbusha Lowassa watu ambao wamesababisha afike alipo. Anawajua ila haonekani kama vile anawakumbuka.

Ni dhambi kuilaumu Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa ilimuonea kumkata. Ni utovu wa fikra sahihi, kumtazama Rais Jakaya Kikwete kwa macho mabaya kwamba ndiye aliyempa paja (kumuwekea kizingiti) Lowassa asiingie Ikulu.

Vema kurejea kule ambako Lowassa alichafuka baada ya kuchafuliwa. Ambako kulisababisha apoteze sifa za kuongoza (legitimacy). Kamati Kuu ya CCM ilitenda kazi yake kwa hofu kubwa. Ni wazi Lowassa alihitajika lakini ilihofia heshima ya chama na mashambulizi ya wapinzani baada ya kupitishwa.

CCM kilihofia kufanya kampeni zake kwa mtindo wa kujibu hoja na kumtetea mgombea. Maana zipo kashfa nyingi kumhusu. Ni uzandiki kukwepa kusema kuwa Lowassa amekuwa alama ya ufisadi nchini kama vyombo vya habari vilivyoripoti na wapinzani kupaza sauti.

Tukumbuke; Lowassa akiwa kwenye kiwango chake bora kabisa, akitetemekewa nchi nzima, akionekana mtendaji bora, waziri mkuu mithili ya hayati Edward Moringe Sokoine, mtu wa kufanya uamuzi mgumu kwa wakati, alidhalilishwa na kudhalilika mno!

Akaporomoka kutoka mtu wa kutetemekewa na watendaji serikalini, mpaka wa kulia-lia: ?Nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana.? Hakufika hapo mwenyewe, kuna watu walimfikisha.

Kama ilivyo somo la mwendo wa kitu (Classical mechanics), Lowassa alikuwa anasubiri muda tu kuingia Ikulu, Magogoni. Hakuna mwingine angeweza kushindana naye katika mbio za kumrithi Rais Kikwete.

Hakuna wa kupinga; Lowassa alikuwa katika mwendo kasi mnyoofu (linear momentum) kwenda Ikulu. Kwa maana uzani wake (mass) kiuongozi na kisiasa, ulishabihiana barabara na kasi (velocity au speed) aliyokuwa nayo.

Wanafizikia wanajua ili kukizuia kitu kilichoshika mwendo wake mzuri ni lazima kigongane na kingine. Mwandishi Saed Kubenea anahusika moja kwa moja kuzipeleka makumbusho, ndoto za Lowassa kwenda Ikulu.

Hakuna namna ya kumzungumzia Kubenea na safari ya Lowassa kwenda Ikulu iliyokwama pasipo kutaja neno ?unafiki?. Ni sikitiko langu kuwa wananchi wa Jimbo la Ubungo wamemchagua mnafiki awe mbunge wao kwa miaka mitano. Ndivyo walivyoamua!

Rejea ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba kati ya Kampuni ya Kufua Umeme (Richmond) na Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya serikali na Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco).

Kati ya ushahidi uliotumiwa na kamati hiyo ya bunge, iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe, lilitajwa Gazeti la Mwanahalisi ambalo bosi wake ni Kubenea.

Na wakati anajitetea, Lowassa aliliita Mwanahalisi ni gazeti la udaku, ingawa hakutaja hivyo moja kwa moja. Mjumbe wa Kamati ya Mwakyembe, Injinia Stella Manyanya, alisema hawakuchukua ushahidi katika magazeti ya udaku, isipokuwa walilitumia Mwanahalisi.

Unafiki wa Kubenea; Rejea matoleo ya nyuma jinsi Mwanahalisi walivyomshughulikia Lowassa kila toleo na kila makala. Kisha kumbuka jinsi Mwanahalisi walivyogeuka watetezi wa Lowassa kila toleo na kila makala baada ya kuhamia Chadema, kisha kuwa mgombea urais kupitia mwavuli wa Ukawa.

Katika hili la unafiki wa Kubenea, kuna mambo mawili lazima kuyaweka wazi. Mosi; Kama habari na makala alizokuwa anaandika kuhusu Lowassa zilikuwa ni uzushi na alimsingizia, huo ni unafiki wa kiwango cha juu.

Pili; Ikiwa alichokuwa anakifanya kilikuwa sahihi, kwamba Lowassa alifanya uchafu mwingi, kama alivyoandika na kuchapishwa na Mwanahalisi, maana yake aligeuka na kumsifia baada ya kuhamia upande wenye maslahi naye. Hakika huo ni usaliti wa miiko, maadili na taaluma ya uandishi wa habari kwa jumla.

Turejee kwenye mosi; Kama alimsingizia, tuusimamishe ukweli kuwa Kubenea hana ubavu wa kuwa na uhasama na Lowassa. Maana yake alitumiwa na maadui wa Lowassa. Mwandishi anayetumika kuchafua wengine ni mnafiki, ni msaliti wa taaluma, ni kanjanja!

Twende kwenye pili; Tunaposimamia kipengele hicho, maana yake ni mtu maslahi. Kwa namna alivyomgeuza Lowassa kutoka ubaya wa Shetani mpaka kumpamba na kumpa uzuri wa Malaika, maana yake anaweza kuandika chochote kusherehesha kilicho na maslahi yake binafsi.

Tukumbuke; Wakati magazeti mengine yaking?ata na kupuliza kuhusu Lowassa, Mwanahalisi lilijipambanua kuwa gazeti bora la uchunguzi kwa kumchunguza Lowassa na kuanika kile ambacho walikitambulisha kwa wasomaji kuwa ni ?habari za ndani? au ?habari za kiuchunguzi?.

Kubenea na Mwanahalisi yake waligeuka marafiki wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, enzi hizo Nape akiutaka uenyekiti wa UVCCM.

Nape alimshambulia Lowassa kwa msaada wa Mwanahalisi. Iliibuliwa mpaka kashfa eti, Lowassa aliingia mkataba haramu, wa kifisadi wa jengo la UVCCM, Upanga, Dar es Salaam. Ikaelezwa kuwa mkataba wenyewe ulisainiwa usiku.

Mwanahalisi ndilo pekee liliandika habari hiyo. Kipindi hicho kukawa na uswahiba mkubwa tu kati ya Kubenea, Mwakyembe na Nape. Zikawa zinapigwa habari za kumtandika Lowassa bandika-bandua.

Mwanahalisi ndilo lililoandika bila woga kuwa Lowassa ni fisadi. Likamshambulia Rais Kikwete kwa kumlinda. Ni gazeti hilo lililowaonesha Watanzania kuwa hapa nchini hakuna fisadi kama Lowassa.

Baada ya Mwakyembe kusoma Ripoti ya Richmond, kisha Lowassa akajiuzulu, wakati wa majumuisho ya hoja (windup) baada ya michango mbalimbali ya wabunge, Mwakyembe alisema: ?Lowassa aliwajibika kutokana na makosa ya watu wa chini yake.?

Nikiri kuwa Mwakyembe alikosea, maana sehemu ya kwanza alieleza mambo mengi kuonesha jinsi Lowassa alivyokosa maadili ya kiungozi mpaka kutoa maelekezo kwa ?vimemo? kuwa Richmond ipewe zabuni ya kufua umeme wa dharura megawati 100.

Baada ya hapo, Mwakyembe alikaa kimya. Na zipo taarifa kuwa ukimya wake haukuwa na maana ya kujiweka kando, badala yake alifanya kazi ya kumlisha ?nondo? Kubenea ambaye aliendelea kumfanya vibaya Lowassa kupitia Mwanahalisi.

Nyakati hizo ndipo Mwanahalisi lilikuwa kwenye ubora wake. Walimgeuza Lowassa kupitia vichwa vya habari kadiri walivyotaka. Walimpaka masizi, shombo na kila aina ya uchafu mpaka kumsababishia anuke na kuogopwa!

Kubenea kupitia Mwanahalisi lake akaandika kuhusu mpango wa Lowassa, kuwekeza shilingi bilioni 8, kwa ajili ya kujisafisha na kashfa mbalimbali zilizomuandama ili kujitengenezea njia ya Ikulu. Kubenea, Kubenea, Kubenea!

Hebu cheka kidogo; Mwaka 2015, Kubenea akageuka adui wa Nape na Mwakyembe. Alikwenda mpaka Kyela kufanya kampeni za kumwangusha Mwakyembe. Hawakuishia hapo, walimtandika kisawasawa Nape. Mara Mwanahalisi, mara Mawio.

Mwandishi maarufu wa vitabu, mlokole Israel Ayivor, aliwahi kuzungumza: ?Save your skin from the corrosive acids from the mouths of toxic people. Someone who just helped you to speak evil about another person can later help another person to speak evil about you.?

Kiswahili chake: Linda ngozi yako dhidi ya tindikali hatari kutoka kwenye vinywa vya watu sumu. Yule aliyekusaidia kuzungumza mambo mabaya kuhusu mwenzako, ndiye atakayemsaidia mtu mwingine kuzungumza uovu juu yako.

Hapo ni rahisi mno kuelewana, kwani Nape na Mwakyembe walimtumia Kubenea kuzungumza uovu dhidi ya Lowassa, ila baadaye waligeukwa. Wakasemwa vibaya sana, maana mwenzao alishageuka na kuwa upande wa Lowassa.

Hii tunaojua haitupi shida, tunafahamu kwamba Kubenea hushika palipo na maslahi ya bosi Anthony Komu.

Komu ni Mkurugenzi wa Fedha Chadema, vilevile ni Mkurugenzi Hali Halisi (Mwanahalisi).

Ndiyo maana Zitto Kabwe alipotofautiana na viongozi Chadema, Mwanahalisi na Mawio walimshughulikia na wanaendelea kumshughulikia. Zaidi maandishi ya Kubenea yamekuwa yakihusika.

Mtoto wa bilionea Phillemon Ndesamburo, Lucy Owenya alionja ladha ya maandishi shombo, alipogombea na Komu ubunge kura za maoni Chadema. Lucy alishinda lakini alikatwa na Kamati Kuu Chadema, Komu akapitishwa.

Maandishi shombo ya Kubenea yalimrudi hata Dk Willibroad Slaa alipojiengua Chadema, kwa kutomkubali Lowassa. Kabla ya hapo Slaa akiwa Katibu Mkuu Chadema na nguzo muhimu ya chama, hakuguswa na zaidi alisifiwa mno.

Wakati nikiendelea kusherehesha mada hii, inatosha kupiga mstari kuwa ama kwa kutumika au kuipigania nchi yake, Kubenea amehusika kuziharibu ndoto za Lowassa. Maandishi yake makali, yaliingia kwa watu ambao walimuona hafai.

Kubenea alimfanya Lowassa aimbwe ni fisadi. Lowassa akawa na sifa mbaya kwenye jamii. CCM nao walitaka mpaka kumvua uanachama (kujivua gamba), wakasita na kuendelea naye. Ikaja kwenye urais, wakaogopa kumsimamisha agombee.

Binafsi naamini kuwa kama baada ya Richmond, ukimya ungefuata, Lowassa asingeandamwa na kashfa za ufisadi, leo hii ndiye angekuwa anasubiri kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maana CCM ingempitisha kugombea na angeshinda kirahisi kutokana na nguvu kubwa binafsi aliyonayo pamoja na ya chama.

Lowassa siye mjinga, naamini anapotuliza kichwa kukumbuka mahali ambako safari yake iliharibika, moja kwa moja Kubenea lazima atokeze haraka na gazeti lake, Mwanahalisi.

Ni kituko wengine kupiga kelele, kumlalamikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva, kumshambulia Rais Kikwete, au kumtazama kwa kijicho, Rais Mteule, Dk John Magufuli, wakati kwa takriban miaka 10 mfululizo, Kubenea alipandikiza mbegu ya kuharibu ndoto za Lowassa kwenda Ikulu.

Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln ?The Great Emancipator?, alikuwa na maadui wengi ambao waliamini kwa umaskini wake, kamwe asingeweza kuwa Rais wa Marekani. Walimwekea vikwazo vingi kwa kumdharau tu kwamba hawezi. Na kweli alishindwa mara nyingi kabla ya kuzifikia ndoto zake.

Baada ya kuwa rais, wakati akitarajiwa angepambana vilivyo na maadui zake waliomdidimiza huko nyuma, Lincoln alihoji: ?Do I not destroy my enemies when I make them my friends??

Kiswahili: Je, siwaangamizi maadui zangu pale nitakapowageuza kuwa marafiki zangu?

Lowassa kwa kutumia falsafa hiyo ya Lincoln, aliamua kuwageuza wale waliokuwa na viherehere, kumsema vibaya, akawafanya kuwa marafiki zake. Kubenea huyo, akasema hata Richmond alionewa!

Mwandishi wa habari, uliandika habari ya uchunguzi kuwa Lowassa ni fisadi, miaka michache baadaye unasema Lowassa alisingiziwa kuitwa fisadi. Sasa hapo aliyemsingizia ni nani? Kama siyo wewe na kalamu yako!

Pengine Kubenea alikuwa na ndoto ya kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, baada ya Lowassa kushinda urais. Au labda aliota kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu. Hayo mambo yameshindikana, hiyo ni kwa sababu ya shamba la chuki dhidi ya Lowassa alilolilima kwa Watanzania.

Kubenea asifikiri Lowassa amesahau, mwanamashairi, hayati Maya Angelou aliwahi kuandika: ?I've learned that people will forget what you said, people will forget what you did, but people will never forget how you made them feel.?

Kiswahili: Watu watasahau kile ulichosema, watasahau kile ulichofanya, ila hawatasahau ulivyowafanya wajisikie.? Lowassa hatamsahau Kubenea. Na hivi urais umekwama, hasira zake lazima zipae juu zaidi.

Chuki ya Lowassa kwa Kubenea na Mwanahalisi; Mwaka 2010, Lowassa akiwa vizuri hasa, imara kama chuma cha pua, nilikutana naye bungeni, nikampiga picha, alikuwa amezungukwa na watu, akanishika mkono (siyo kwa shari), akaniambia: ?Kuna magazeti hayaruhusiwi kunipiga picha.?

Nikamuuliza ni yapi hayo, hakutaka kujibu, akaniambia tu ?yapo na yenyewe yanajijua?, katika wale watu waliokuwa na Lowassa, mmoja wao aliamua kutoa sentensi nyoofu: ?Mojawapo ni Mwanahalisi!?

Unaweza kuwaza mbona Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu na wengine nao waliwahi kumshambulia Lowassa na sijawaandika. Itakuja makala kuhusu majina ya watu waliomnyima urais Lowassa mwaka 2015.

Imeandikwa na Luqman Maloto,
Maandishi Genius..
 
Kubenea ni miongoni mwa waandishi wahuni tu hana lolote akihongwa pesa kidogo tu anakusafisha kweli
 
Shombo za kubenea zimeharibu ndoto ya LowassaKUHARIBU ni rahisi kuliko kuunda, kutambua hili haihitaji kurejea nukuu ya mwandishi mkubwa wa vitabu raia wa Czech, Ivan Klima. Ila unachopaswa kuzingatia ni kuwa kuharibu ni kuunda, kuunda ni kuharibu (To create is to destroy, to destroy is to create).

Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
U Genius uko wapi hapo.

Ni ukweli usio pingika hata ivo ya kuwa hao mazandiki ya Chadema ndio yalituaminisha milolongo ya kashfa za ufisadi hadi Lowassa akapigwa chini, CCM wakaamua kujivua magamba na Chadema wakaanzisha Magwanda.

Chadema tangu kinunuliwe kimekosa Dira. Kubenea kamchafua sana Lowassa akifuatiwa na hao Chadema.

Wayanywe wakati sisi tunapeta na JPM
 
'Lowassa hasafishiki '- Mwanahalisi!

Hakuna Akili Kubwa Duniani kwny Siasa Kama Kumtumia Adui yako kusilibia Mgombea wao wa Urais wakidhani wanakukomoa Wewe!

Mbowe na Kubenea na Nyumbu wote wametumika sana bila ya kujijua!

Mapumziko mema Mwalimu wa Siasa Jeshini (JWTZ) na Uraiani Luteni Kanali Mstaafu Jakaya Kikwete

Jakaya Kikwete na Edward Lowassa ndio Wanasiasa waliotukanwa Zaid na Nyumbu wa Chadema 2005-2015 lakini cha ajabu;

Baada ya 2015 Kipenzi cha Roho cha Nyumbu kwa sasa ni Lowassa!

Mtu wanae mmiss zaid kwa sasa kwny Uongozi ni Jakaya Kikwete!

Nyumbu sio Watu wa Mchezo mchezo!
 
Sijui Niite Hotuba,au Makala Au Vyovyote Vile,ila kiukweli sijui ni kwa nini lowassa hanaga muda wa kujibu haya mavitu,kitu nachohisi ndicho kinampa chati kuliko
 
Back
Top Bottom