Kubana misuli

waits

Member
Sep 2, 2014
38
16
Wakuu heshima yenu na itifaki izingatiwe!!!!!

Ninalo tatizo ambalo limekuwa likinisumbua kwa muda mrefu, zaidi ya miaka mitano sasa. Nimetafuta namna ya kulidhibiti bila mafanikio. Naomba nililete kwenu wataalam wa jukwaa hili kwa msaada wenu wa mawazo na ushauri kwani linanipa shida sana mpaka nashindwa kufanya shughuli zangu kiufanisi.

TATIZO: Misuli ya kiunoni kuja mpaka matakoni inavuta/inakaza, nikikaa napata shida kunyenyuka, nikitembea natembea kwa shida kwa kuchechemea, na wakati mwingine inafikia hatua nikilala kujigeuza inakuwa kwa shida sana. Zamani kidogo ilikuwa inatokea mara moja baada ya miezi minne mpaka sita lakini siku hizi ni almost kila mwezi inajirudia kwa kubadilishana/kupokezana kwa maana kwamba kama mwezi huu ni misuli na tako la kushoto awamu nyingine itakuwa kwa tako la kulia. Nimeishawahi kwenda hospt nikaambiwa kwamba huenda ni tatizo la pingili hazijakaa vizuri wakanishauri kupiga x-ray, matokea yakaonyesha pingili zangu hazina shida yeyote.

Naamini ushauri wako wa kitabibu utakuwa na nafasi kubwa kunisaidia kupata ahueni.
Natanguliza shukrani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom