Kubana Matumizi: Ofisi ya Waziri Mkuu kutumia bajaji, pikipiki

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutenga fedha ya kununulia bajaji na pikipiki zitakazotumiwa na watumishi kwa mwaka huu wa fedha, ikiwa ni mkakati wa kubana matumizi.

Wizara iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2016/17, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa amesema uamuzi wa namna hiyo unaendana na dhana ya kubana matumizi ya fedha ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Hata hivyo, hotuba ya bajeti iliyosomwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana, haionyeshi pikipiki na bajaji hizo zinanuliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa kada gani.
 
Ziliwahi kununuliwa bajaj ili zitumike kama ambulance wakati wa awamu ya nne. Leo hii hakuna hata moja inayofanya kazi hiyo. Tuachane na mawazo mgando- yanaweza yakanunuliwa magari ya gharama ndogo yakawekewa utaratibu mzuri wa matumizi. Gharama za uendeshaji wa magari ya serikali zinatokana na unrealistic fuel allocation inayotolewa kwa magari hayo pamoja na unrealistic repair & maintenance cost. Serikali ikiweza kubana maeneo hayo mawili itaweza kuendesha magari yake kwa gharama ambazo ni affortable.
 
Huko si kubana bali kuongezwa, mataumizi mengi ni ya kimagumashi mafuta ya elfu 20 inaandikwa laki2,repairing ya laki inaandikwa mil10 hapo ndio wizi ulipo.
 
Serikali ina maajabu hii, mpaka yanafikia ukomo wa kushangaza! kwa nini wasiondoe mashangingi? Awamu iliyopita walikuja na hoja ya bajaji kuwa ambulance mahospitalini lakini hatujafanikiwa kuziona hata moja zikifanya hizo kazi, ifike mahali waweke bajeti yenye manufaa kwa wote na sio kwa kupumbaza watanzania.
 
Waongeze na bajeti ya matibabu ya majeruhi wa ajali barabarani na burial assistance maana usafiri huo una tabia ya ajali za mara kwa mara
 
Gari jipya linaandikiwa linatumia lita 1 kwa Km 8 na bei ya mafuta hayo inakuwa doubled...

Gari la serikali lililopo pool linatumika kuhudumia small house ya boss...kumtoa nyumbani kwenda saloon, toka saloon...kumsalimu shost...toka hapo kwenye burudani ya taarab...

Kwa mwendo huo tutafika? Kubana matumizi kuende pamoja na kuwapa raia na vyombo vya dola mamlaka ya kukamata magari ya umma yanayotumika vibaya...pia iwekwe sheria ya muda wa mwisho wa magari hayo kuwa mitaani kama ilivyokuwa enzi za Ruxa
 
Ziliwahi kununuliwa bajaj ili zitumike kama ambulance wakati wa awamu ya nne. Leo hii hakuna hata moja inayofanya kazi hiyo. Tuachane na mawazo mgando- yanaweza yakanunuliwa magari ya gharama ndogo yakawekewa utaratibu mzuri wa matumizi. Gharama za uendeshaji wa magari ya serikali zinatokana na unrealistic fuel allocation inayotolewa kwa magari hayo pamoja na unrealistic repair & maintenance cost. Serikali ikiweza kubana maeneo hayo mawili itaweza kuendesha magari yake kwa gharama ambazo ni affortable.
Kabisa mkuu ikiwa watu binafsi wanayamiliki bila kuwa na gharama kubwa kama serekalini.
 
Ziliwahi kununuliwa bajaj ili zitumike kama ambulance wakati wa awamu ya nne. Leo hii hakuna hata moja inayofanya kazi hiyo. Tuachane na mawazo mgando- yanaweza yakanunuliwa magari ya gharama ndogo yakawekewa utaratibu mzuri wa matumizi. Gharama za uendeshaji wa magari ya serikali zinatokana na unrealistic fuel allocation inayotolewa kwa magari hayo pamoja na unrealistic repair & maintenance cost. Serikali ikiweza kubana maeneo hayo mawili itaweza kuendesha magari yake kwa gharama ambazo ni affortable.
Ni kweli mkuu.... life time ya bajaji ni 3 yrs hivo ni kujidanganya kufikiri kununua bajaji ni rahisi.... na wakati huo haziwez fanya kazi nyingi....
 
Wafanyakazi wakopeshwe magari ya kawaida Suzuki,Starlet wapewe fedha ya mafuta tu
Mkuu nimeona hii kwenye makampuni ya kimarekani..... kwa kweli ni very effective na gharama ni ndogo kwa kampuni.... serikani inaweza fanya hv kwa baadhi ya taasisi na vyeo fulani maana mwisho wa siku mambo ya repair hayahusu kampuni/ serikali...
 
Back
Top Bottom