Kubambikia Wananchi Kesi, Itungwe Sheria Kuwabana Polisi

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Muda mrefu kimesikika kilio cha wafungwa na mahabusu kadha kulalamika kuwa wamebambikiwa kesi, hali kadhalika, wananchi kote nchini wamesikika hapa na pale wakilalamika kuwa maafisa wa serikali za mitaa, wenyeviti, wakurugenzi na wengineo wengi wakidai kwamba ama wao wenyewe ama jamaa na ndugu zao wamebambikiwa kesi.

Malalamiko haya yamekuwa yakisikika muda mrefu lakini hakuna hatua zozote za makusudi zilizoonekana zikichukuliwa na ama jeshi la polisi ama serikali yenyewe. Kwa sasa ni muda mwafaka wa kuitaka serikali ipeleke muswada bungeni utakao wabana polisi na maofisa wengine wa ngazi mbali mbali kutoweza bambikia kesi wananchi.

Pasipo kuwepo na sharia mahususi inayo wabana wanaobambikia wananchi kesi uonevu na dhuluma hii itaendelezwa na hawa polisi wetu.

Mara nyingi mahakama imekuwa ikiwaachia huru watu hawa waliobambikiwa kesi na polisi; hata hivyo watu hawa kabla ya kuachiwa wanakuwa wameshateseka na kuumizwa kisaikolojia, kimwili kiuchumi na kijamii.

Dawa na suluhisho ni moja tu, bunge litunge sharia ya kuwabana polisi wanaofanya uovu huu kwa watu wasiokuwa na hatia na ambao mara zote hawana uwezo wa kuajili mawakili wa kuwatetea.
 
Ni kweli na inauma Sana...lakini Bunge lenyewe ukitazama waheshimiwa wakufanya komedi zao utachoka!
 
Suala Si sheria hapo,mbona tuna sheria nzuri sana.Hapa issue hapo ni waliopewa dhamana ya kutekeleza hizo sheria ndiyo shida.

Rais Magufuli haangaiki na sheria Bali anahangaika na wanatekeleza sheria

Tatizo ni maadili,attitude, ethics,commitment n.k ktk utekelezaji wa kazi zetu za kila siku.
 
Back
Top Bottom