Kubadillishwa kwa sarafu

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Hivi sasa wafanyabishara wakubwa wameacha kuagiza mali wakiangalia kwanza hali ya uchumi itakuwaje chini ya serikali ya rais JPM.

Hii ina maana kuwa kuna fedha nyingi sana majumbani mwa watu hao.

Mimi siyo mchumi lakini nadhani namna ya kurudisha hizo fedha kwenye mzunguko ni kubadilisha sarafu haraka ili zitoke huko mafichoni na kurekebisha sheria ya benki kuu ili kuthibiti matumizi ya fedha taslimu.

Hivi sasa mtu unaweza kuchukua hata tzs bilioni moja fedha taslimu kwenye masanduku na masandarusi.!!!!!!!!!!!!!
Kuna haja ya kukataza kabisa benki kulipa fedha taslimu kwa hundi zote. Watu wafungue akaunti ili fedha zote zipitie benki.
 
Back
Top Bottom