Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Kwani wewe unataka upinzani hapa nchini?Heri ya Muungano wadau.
Nimejiuliza tu,nikaona ni vema pia nipate maoni kutoka kwa werevu wa mambo.Ila mimi kwa upande wangu nimeona ya kuwa KUB,Mbowe amepwaya na abadilishwe ili tupate KUB mbadala mwenye weledi.Na hapa sio jambo la Aibu amwachie Rwakatare Wilfred ambaye alipata kuwa KUB (2000/2005).Japo kulikuwa na ugumu lakini mara kadhaa aliongoza kambi ya upinzani iliyoweza kuwashawawishi wabunge wa CCM kuunga mkono hoja dhidi ya serikali.
Ikumbukwe tu mara kadhaa KUB wa sasa hayupo "consistent" hili linatokana na sababu kwamba yeye kama kiongozi huyumbishwa na mawazo ya wasaidizi wake yaani hana anachosimamia kama kiongozi,ikitokea Lisu,Kubenea,Mnyika wakatoa ushauri(miluzi) hukosa uamuzi.
Kakosa "Focus" na kutengeneza hoja endelevu ili kuleta matokeo na badala yake anajikita na vijihabari na matukio yasiyo na msingi.
Uwezo wake wa kuchimba ripoti na kuwasilisha mada za kitaalam kwenye hadhira ni mdogo..mara nyingi huongea kwa kufoka foka (povu),hana "details" na mambo mengi ya msingi na sio msomaji.
Ni hayo tu,nipo tayari kukosolewa...nimelazimika kuleta haya kwa sababu KUB ni mtumishi wa umma na analipwa kwa kodi zetu.
Ni kweli...Mbowe alikuwa bora chini ya Slaa na Zitto..,ndio maana hata kikao cha bunge kilichopita ilibidi amkibilie ZZK baada ya kutowa hoja yenye mashiko.Sasa ni dhahiri udhaifu wa Mbowe unaonekana wazi......na hii inasababishwa kwa kutokuwepo kwa Dr Slaa
Lazima kunakuwa na Kaimu kiongozi wa shughuli.za serikali,kumbuka Majaliwa ni binadamu huuguwa na hupata dharura.lakini siyo mbowe tu,Hata majaliwa kassim amepwaya sana!....Amekacha kipindi cha maswali ya papo kwa waziri mkuu kila alhamisi
Jikite kwenye hoja mkuu,hasira zinaziba ufahamu.Kwani wewe unataka upinzani hapa nchini?
Huhitaji kuangalia bunge ili ujue udhaifu wake,hata akiongea na waandishi anatowa hoja dhaifu.Hivi hilo bunge mnalifuatiliaje?
Au kuna private channel pale Lumumba?
Mimi naona bora ungekuwa wewe KUBJikite kwenye hoja mkuu,hasira zinaziba ufahamu.
Jikite kwenye mada dogo!Kwani siku za sikukuu huwa mnalipwa Over Time?
Dogo lazima mjifunze kukubali kukosolewa,jikite kwenye mada.Toa boriti kwenye jicho lako ndo utoe kitanzi kwenye jicho na mwenzako. Wapinzan au Mbowe anakuhusu nini? Acha Mawazo mgando leo ni public holiday naona unataka ulipwe 7 x 2 . Tumekustukia
Unajuwa bavicha wanajuwa KUB si mtumishi wa umma.Ukichanganya mambo matatu yafuatayo ndio utaelewa kwa nini amepwaya....
Moja ni aibu ya kumtetea fisadi na kumpa agombee urais ndani ya kipindi kifupi tena bila wanachama wake kuridhia.
Mbili ni kumtosa Think tank wa Chadema Dr Slaa na timu yake.
Tatu ni kiwango chake cha elimu kisichojulikana !