Hivi kile kiapo wabunge wateule wanachofanya bungeni mbele ya spika si kina maana baada ya hapo wanakuwa wabunge kamili na si wateule tena ili waweze kikatiba kufanya kazi zao.

SASA inakuwaje akina Shamsi Nahodha ambao ni wateule tu na hawajala kiapo bungeni wanaapa kuwa mawaziri wakati ILI uwe waziri ni lazima uwe mbunge kwanza!!!

Kama hivyo ndivyo, je kile kiapo Rais anachokula uwanja wa Taifa ni kulinda katiba kwa baadhi tu ya mambo, hasa makubwa na si ku-observe each and every thing in constitution?

Je, mwanasheria mkuu na wanasheria washauri wa Rais wanamtakia mema kwa hilo?

kuvunja vipengele vidogo kunapelekea kutokuwa na uwoga tena wa kuvunja vipengere hata vikubwa. Ni mtizamo wangu tu na naomba tukemee na ku-highlight hili ili katiba isinyanyaswe this much.

Asanteni!