Kuapishwa Uwaziri Wasio Wabunge

edsonda

Member
Mar 17, 2009
5
0
Hivi kile kiapo wabunge wateule wanachofanya bungeni mbele ya spika si kina maana baada ya hapo wanakuwa wabunge kamili na si wateule tena ili waweze kikatiba kufanya kazi zao.
SASA inakuwaje akina Shamsi Nahodha ambao ni wateule tu na hawajala kiapo bungeni wanaapa kuwa mawaziri wakati ILI uwe waziri ni lazima uwe mbunge kwanza!!!

Kama hivyo ndivyo, je kile kiapo Rais anachokula uwanja wa Taifa ni kulinda katiba kwa baadhi tu ya mambo, hasa makubwa na si ku-observe each and every thing in constitution?
Je, mwanasheria mkuu na wanasheria washauri wa Rais wanamtakia mema kwa hilo?

kuvunja vipengele vidogo kunapelekea kutokuwa na uwoga tena wa kuvunja vipengere hata vikubwa. Ni mtizamo wangu tu na naomba tukemee na ku-highlight hili ili katiba isinyanyaswe this much.

Asanteni!

Mkuu labda umepitiwa kidogo, hawa mawaziri wote ni wabunge walioapishwa kwa mujibu wa katiba

Hivi kile kiapo wabunge wateule wanachofanya bungeni mbele ya spika si kina maana baada ya hapo wanakuwa wabunge kamili na si wateule tena ili waweze kikatiba kufanya kazi zao.

SASA inakuwaje akina Shamsi Nahodha ambao ni wateule tu na hawajala kiapo bungeni wanaapa kuwa mawaziri wakati ILI uwe waziri ni lazima uwe mbunge kwanza!!!

Kama hivyo ndivyo, je kile kiapo Rais anachokula uwanja wa Taifa ni kulinda katiba kwa baadhi tu ya mambo, hasa makubwa na si ku-observe each and every thing in constitution?

Je, mwanasheria mkuu na wanasheria washauri wa Rais wanamtakia mema kwa hilo?

kuvunja vipengele vidogo kunapelekea kutokuwa na uwoga tena wa kuvunja vipengere hata vikubwa. Ni mtizamo wangu tu na naomba tukemee na ku-highlight hili ili katiba isinyanyaswe this much.

Asanteni!
Edisconda, unaiaibisha JF!. Hukusoma chochote humu wakati kila kitu muhimu kwa taifa hili lazima kipandishwe hapa jf, lets assume jf hukupata muda, hata magazeti?, yote yako online na picha waliweka. Anyway, pia hii ni haki yako under the freedom of expression.

Najua mnadhani sipo makini na ufuatiliaji wa HABARI, lakini mkumbuke mfano nilioutoa ni Shamsi Vuai Nahodha AMBAYE ni MBUNGE wa KUTEULIWA na aliteuliwa wakati Bunge session imeisha Dodoma. Hivyo pia Prof. na Mengji kama angepewa UWAZIRI nae ingekuwa TABU.

Unless walipata MUDA wa kuapishwa ubunge hawa watatu. Kitu ambacho SIKUMBUKI kutokea.

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom