Kuanzishwa kwa chama cha wakulima wa nyanya Tanzania(CHAWANYATA)

fastum

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
337
220
Habari njema kwa wakulima wote wa nyanya Tanzania, kwa muda mrefu sana tumeona wakulima wa nyanya tanzania wakipoteza mitaji yao kwa bei ambazo hazina faida kabisa ila sasa hichi chama kitakuwa kinafanya kazi yake kama EWURA kwa kudhibiti be za nyanya nchi nzima kwa makusudi kabisa ili mkulima wa nyanya aweze kupata haki yake stahiki kwa maendeleo la taifa letu.
Chama kwa kipindi chote kitadhibiti bei za nyanya wakati nyanya zipo nyingi na wakati zipo chache kwa kutoa bei elekezi kwa nchi nzima kwa yoyote atakaetaka kununua na kwa wakulima kujua ili wasipunjue stahiki zao.mfano wakati nyanya ni nyingi mno kutakuwa na bei elekezi mfano shillingi elfu 15000 kwa tenga moja ili mkulima aweze kupata faida na kumudu kulima tena,pia ikiwa nyanya ni chache kwa mfano kunakuwa na bei elekezi ambayo kwa mfano tuseme elfu 45000 kwa tenga kwa nchi nzima ili kumlinda mlaji pia kuepuka tudhulumiwa na hawa madalali katika biashara hii ya zao la nyanya.Naomba kuwakilisha tunakaribisha maoni yenu wadau ili nchi hii iweze kuenda mbeli hii imetokana baada ya kuona wizara ya kilimo ikiwa imelala kabisa kutowasaidia wakulima pamoja na walaji au watumiaji wa zao la nyanya asanteni.
 
Wakulima wa nyanya kama mnataka hicho chama kiwe na meno.mnatakiwa muwe na kiwanda cha kuprocess nyanya.pia maghala ya kuifadhi nyanya wakati wa msimu ili muweze kukontrol bei ya nyanya kwa kipindi cha mwaka mzima kwa kukontrol demand and supply! Mziki wa nyanya unakuwaga pale msimu wa mavuno,mvua kibao
 
Back
Top Bottom