kuna jamaa yangu ameanzisha mwaka juzi, mchakato unaanzia pale tcra kwa wewe kuandika barua ya maombi ya leseni ikiambatana na andiko la mradi. hiyo itabidi uwafuate wataalamu wa maandiko ukimaliZa unapeleka pale tcra pamoja na us dola mia tano (sina akika kwa sasa) utasubili ujadiliwe pia utaitwa kwenye mahojiano, kama andiko lako limepita utapewa kibari cha ujenzi cha muda nafikili ni miezi 3 utatangaza kwa majaribio kama hupo vizuri utakabiziwa leseni yako kamili, mtaji nakushauli tenga milion 20, vifaa ni pamoja na transmita, audio mixa, mic mbili, compyuta japo mbili, pia kuna kifaa kinaitwa s.t.l (link)