Wadau nipeni maujuzi na
utaalamu mwepesi kwa walio weledi katika mambo ya Bima.Nataka kuanzisha
kampuni yangu ya Udalali wa Bima. Tayari ninakmapuni lakini haina line
ya Bima lakini kwa sasa naona kama kuna Opportunities katika eneo hilo
na naweza kucapitalize vya kutosha, ila miye ni mtaalamu wa mambo ya
fedha na uchumi siyo Bima.Kwa kutambua nafasi ya jamii forums naombeni
msaada katika kukidhi haja yangu ya kuwa na kmapuni ya Bima kwa siku
zijazo kwa kuanza na kampuni ya udalali.Msaada kwa wabobezi katika secto
hii iwe ni
- Mtaji unaotakiwa
- staff qualification
- maeneo/ location ya biashara
- mahitaji na masharti ya leseni ya Udalali
- na mengineyo yanaendena na biashara hii
- Vijana waliomaliza au kuwa na elimu ya Bima watapewa kipaumbele
wakati wa ajira
- Tofauti ya Wakala wa Bima na Dalali wa Bima katika mahitaji ya
Usajili.
- Naweza kupata fomu za usajili kwenye mtandao wa Mamlaka ya Bima au ni
non- digital?
- natanguliza shukrani kwa elimu nitakayopata toka kwenu.