Damy Scotty
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 717
- 453
Lowassa.
Hivi kwenye siasa kuna consistency?
Lowassa akishinda hawi Mwenyekiti wa chama,chama na dola haitokuwa kama CCM,Chama kitaisimamia serikali na kuiwajibisha wakati maCCM serikali inakitia chama mfukoni na hakina sauti wala mlio wa huzuni!!!
Lowassa akishinda,Mawaziri baathi yao ni Mbowe,Mbatia,Tundu Lissu,Mnyika,Halima Mdee,Kafulila,Silinde,Habib Mnyaa,Mbarouk etc
Kwenye orodha tajwa hapo,wabunge gani wa maCCM wanawazidi hao tajwa hapo kwa uchapa kazi na uadilifu??!! Utasema January Makamba,Ridhiwani,Ummy Mwalimu,Angela KairukinChenge na kina Mama Sita?!!
Lowassa atarudisha katiba ya Warioba,Magufuli ataweza?! Lowassa atavunja mkataba wa bandari ya Msoga/Bagamoyo na kupeleka mradi Tanga au Mtwara,Magufuli atathubutu?!
Serikali ya UKAWA itatunga upya sheria ya mafuta na gesi na kufuta ile ya CCM ambayo imepitishwa na wabunge 80 tu wa maCCM kati wabunge 400,Magufuli atathubutu au ataishia kuleta ukasuku tu?!!
CCM (idea, deeper kuliko chama) ni lazima ishinde mwaka huu.
Ama kwa mgombea wake Magufuli, ama kwa mgombea wake Lowassa.
Upinzani hauna mgombea.
Kwa hivyo, CCM haiwezi kuanguka mwaka huu.
Huwezi kuleta mabadiliko ya kweli kwa kutumia makapi ya CCM ambayo hata hayajapata muda wa kuangaliwa ndani ya upunzani.
CHADEMA hamjajifunza kwa Shibuda tu?
Mimi namuelewa Mwanakijiji.
Unabii huu ulitabiriwa Na Mzee mwanakijiji, na sasa ni wazi kabisa unatimia. .
Kwa vile unabii utatimia ulivyo, nawasihi wale wote waliofunguliwa kuwa tayari kwa lolote kwani vichaa wamepewa sime sokoni! Tutakiona cha moto! Kama walivyowahi kusema wengine ni bora kufa kwa heshima kuliko kuishi kwa aibu! Tuendelee kuwaamsha watu wengi zaidi ili kuhakikisha kuwa pigo la kwanza takatifu, pigo lisilo na huruma, pigo lisilo na onyo liangukie CCM kwenye chaguzi zote zinazokuja kuanzia sasa.
Kwani unabii utatimia; ndivyo ilivyopaswa kuwa, nayo itakuwa kwani hivyo ndivyo ilitakiwa iwe. NA ITAKUWA.
Nitafute Facebook: Mimi Mwanakijiji
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Kama wewe ni mfuatiliaji utagundua kuwa katika ile list of shame haikuwa na Lowasa peke yake.. pamoja na wengine Mkapa alikuwemo, Kikwete pia alikuwemo, licha ya Lowasa mwenyewe kukiri kuwa ile dili ilikuwa na ya Mamlaka ya juu, na juzi Lisu kuthibitisha hadharani kuwa Richmond ni ya Kikwete kwa nini sasa anaandamwa Lowasa peke yake?
Tatizo lilikuwa uwaziri mkuu au Richmond? Kama tatizo lilikuwa Richmond kwa nini kamati ya Mwakyembe haikumhoji? TAFAKARI
Tatizo unaongelea siasa wakati mimi naongelea principled leadership.
Consistency gani unayoiongelea hapa. Kuwa specific.
Mimi naongelea consistency ya kumpinga Lowassa kama fisadi.
Mwanakijiji alimsema Lowassa fisadi kitambo sana. Kaandika mengi sana kuanzia vibahasha walivyokuwa wakipewa waandishi wa habari mpaka Richmond. CHADEMA walipenda kusikia hilo kwa sababu Lowassa alikuwa CCM. CHADEMA wakamuita Lowassa fisadi mkubwa. Na list of shame akawekwa.
Leo Lowassa kaenda CHADEMA. Mwanakijiji anaendelea kusema Lowassa fisadi. Na mimi sioni Lowassa kaacha vipi au lini kuwa fisadi. Kwa hiyo katika hili Mwanakijiji yupo consistent.
Huko CHADEMA sio tu mmemkaribisha, mmempa na nafasi ya kugimbea urais bula ya kutueleza Lowassa kaacha ufisadi lini?
CHADEMA is not consistent in this.
Kweli Kiranga? Labda utakuwa hukumsoma Mzee Mwanakijiji mwaka 2010 na harakati zake katika kuinadi CCJ ya Nape, Sitta na Mwakyembe waliodaiwa kuwa wapiganaji ndani ya CCM. Hawa Mzee Mwanakijiji aliwapenda sana tu na hata siku moja hakuwaponda. Ikumbukwe kwamba kabla ya kashfa ya Richmond zilikuwepo pia kashfa zingine kama za CDA, TIC na zinginezo ambazo zote zilimhusisha mtu moja naye ni Samwel Sitta....Mimi namuelewa Mwanakijiji.
Kweli Kiranga? Labda utakuwa hukumsoma Mzee Mwanakijiji mwaka 2010 na harakati zake katika kuinadi CCJ ya Nape, Sitta na Mwakyembe waliodaiwa kuwa wapiganaji ndani ya CCM. Hawa Mzee Mwanakijiji aliwapenda sana tu na hata siku moja hakuwaponda. Ikumbukwe kwamba kabla ya kashfa ya Richmond zilikuwepo pia kashfa zingine kama za CDA, TIC na zinginezo ambazo zote zilimhusisha mtu moja naye ni Samwel Sitta.
Kinachonishangaza ni kwamba wote waliowahi kuwa na tuhuma katika nchi hii tukianza na Kikwete, mkataba wa IPTL akiwa Waziri wa Nishati, hadi Mwakyembe, Umeme wa Upepo, wanafumbiwa macho lakini si Lowassa. Bahati nzuri tuko wengi, on record, tuliosema na tunazidi kusema, adui wa taifa hili ni CCM na si individuals, ni mfumo. Kinachomsukuma Mzee Mwanakijiji ni chuki abayo imekomaa na kugeuka obsession dhidi ya Lowassa.
kashaeleza kwamba mwenye Richmond ni rais. maelezo gani ya kueleweka unataka?Mie sijawatetea hao wengine.
Na wala sijasema kwamba nakubaliana na Mwanakijiji katika yooote.
Ila katika la kumsema Lowassa, siwezi kushangaa Mwanakijiji akishindwa kumpa support Lowassa leo, kwa sababu hajawahi kumpa support.
Ninachoshangaa ni CHADEMA kumpa nafasi ya kugombea urais bila maelezo ya kueleweka kuhusu ufisadi wake.
Lowassa anapata prominence sasa kwa sababu anagombea urais.
kashaeleza kwamba mwenye Richmond ni rais. maelezo gani ya kueleweka unataka?
Just like that? Na rais naye kasema mwenye Richmond anatembea na Tundu Lissu.
Kwa nini hajatoa documents siku zote hizo?
ni rais huyo alisema hamjui mwenye richmond na hajawahi muona, ni huyo alimleta muoman aliyejieleza kwamba ndiye mmiliki wa richmond, ni huyo leo anasema mwizi yuko na na lissu. lazima tukubali kuwa kwenye richmond tulitakke sides kwa mapenzi tu siyo facts. facts zinapoanza kujionyesha kuna watu kama mwanakijiji wanaona aibu kubadilika kwasababu kipindi kile waliongea kana kwamba wanaujua ukweli wote.Just like that? Na rais naye kasema mwenye Richmond anatembea na Tundu Lissu.
Kwa nini hajatoa documents siku zote hizo?
And to Lowassa just like that!?
Unataka mpaka aje kutoa hata minutes za baraza la mawaziri ambaye mwenyekiti wake ni Rais mkuu?
Jamaa anaposema waende mahakamani ana maanisha kweli kuwa serikali ilipeleke hilo mahakamani ili kila kitu kikaagizwe kiende huko!!
ni rais huyo alisema hamjui mwenye richmond na hajawahi muona, ni huyo alimleta muoman aliyejieleza kwamba ndiye mmiliki wa richmond, ni huyo leo anasema mwizi yuko na na lissu. lazima tukubali kuwa kwenye richmond tulitakke sides kwa mapenzi tu siyo facts. facts zinapoanza kujionyesha kuna watu kama mwanakijiji wanaona aibu kubadilika kwasababu kipindi kile waliongea kana kwamba wanaujua ukweli wote.
hakutoa documents zote kama tu mwakyembe alivyosema serikali ingeanguka. bado hatujui ukweli wote wa richmond hivyo tusione aibu kubadilika mara mambo yanavyojifunua.