Kuandamwa kwa Makonda

Kuandamwa kwa Makonda

Kumekuwa na kelele nyingi walipoitwa wasanii kituo cha polisi na wengi wakapaza sauti kuwa wanaonelewa tu, wakadai wakamatwe mapapa wa biashara hiyo na si mateja.

Wametajwa watu 'wakubwa' katika nchi hii ila cha ajabu kulalamika kumezidi! Nini hamaki yenu?

Makonda anaandamwa kuanzia ndani ya bunge na hadi katika vyama vya siasa, wafuasi wa waliotajwa nao mishipa ya shingo inawatoka!

Watu wa madawa ya kulevya ni kama wachawi, ukiambiwa bibi yako ni mchawi unaweza kudhani anaonelewa lakini hujui kuwa mambo hayo hufanyika kwa siri sana.

Hata akitajwa baba yako mzazi kuwa mpole maana huzijui harakati zake, na aliyetajwa hapaswi kuhamaki na kuanza kubwabwaja bali aache sheria ifanye kazi yake na kama ahusiki atakuwa huru na itakuwa ndiyo mwisho wa uvumi.

Matusi, kejeli na kashfa za kila aina anatupiwa makonda, huenda mmemchukia au kumdharau lakini kumbukeni kuwa anachojaribu kufanya kimewashinda wengi na pia kumbukeni anaposema yeye inasema kamati ya usalama ya mkoa wa Dar es salaam, hivyo ana mamlaka hayo ya kumuita yeyote katika swala la usalama bila kupingwa kwa malumbano.

Kikwete aliwahi kusema tu madawa ya kulevya yanaingizwa na baadhi ya viongozi wa dini na akaandamwa sana mpaka akaamua kutulia, je Nchi hii ni ya watakatifu hakuna wanaoingiza unga? Mbona kila anaetajwa ni mkali na wafuasi wake wanamtetea?

WANANCHI WENZANGU TUSICHEZE NGOMA TUSIYOIJUA, UNAPOONA WAKUBWA WANAPAMBANA UJUE MASLAHI YAMEGUSWA.
NI MUDA WA MAPAMBANO NA KUMUUNGA MKONO MAKONDA NA ALIYE MCHAFU AJISAFISHE MWENYEWE.

Ndimi Mvumbo Kivugo.
Makonda hatupiwi kashfa, style yake ya kuongea na kufanya kazi ndo inamponza.
Fuatilia ile ziara yake ya Dar mpya afu uone kama ule ndo utawala bora.
Fuatilia vita yake ya sasa ya madawa ya kulevya. Vita tunaipenda ila watu wanalamikia "Makonda Style".
Ngoja nikuulize swali. Ingekuwa hii vita imefanywa na tuseme Waziri wa Mambo ya Ndani...
Akawataja watu kwa style hiyo hiyo na katika orodha akamtaja Makonda kwa style aliyowataja Mbowe, Manji na Gwajima.
Hapo ndo ungekisikia kilio na ulalamishi wa Makonda. Na zile video zake dua zingeongezeka mara dufu.
 
Hapo mwanzo si ndio nyie mlokua mkitaka watu watajwe na Kitwanga kwasababu kulikua na maslai yenu mlotegemea sasa imegeukia kwenu mnaona Makonda afai asinge mtaja mbowe yote malalamiko yasinge kuwepo.
Kwani hao wengine walotajwa hawana jamii inayo wategemea?mpaka nao wasichafuliwe? Acheni zoezi lifanyike akuna mtakatifu chini ya jua
Umehitimisha vyema HAKUNA MTAKATIFU HATA MMOJA
 
Back
Top Bottom