Usipaniki dadangu. Mie sikukutuma ukalambe watu viatu,we endelea tu huko kuuza akili na uhuru wako kwa mwenye akili.
Watu jasiri, wenye akili na wathubutu hawauzi uhuru wao aslani.
Wenye akili hutumia akili yao kuteneneza patterns za maisha yao kadiri waamuvyo wao.
Kuaniriwa ni sawa na kuolewa na mume, maana unamtumikia huyo mume.
Ukiajiriwa maana yake unauza akili yako kwa alie kuajiri. Huyo aliekuajiri ataitumia akili yako atakavyo yeye na sio utakavyo wewe.
Huwa nawadharau sana nyie mlioajiriwa na kuishi kwa kutegemea mshahara unaolipwa mwisho wa mwezi.
Huwa nacheka sana unayona mafanyakazi yanajazana baa meisho wa mwezi

. huo kama sio utumwa wa akili ninini?
Unatumiwa maisha yaki yote nguvu zikiisha unafukuzwa uende kwenu uwapishe wenye nguvu.
Hakuna mwenye akili ndogo amewahi kuniajiri
Unakuta jitu na mikotimikoti mtumbo mbele lakini linaishi kwa kupokea mshahara mwisho wa mwezi.
Mwanaume unavimbavimba tu kumbe mtu mwenyewe nguvu yako iko kwa anaekulipa mshahara, kesho akisema masi litumbo linaporomoka, unakufa kwa msongo wa mawazo.
Heshima kwenu wapambanaji mliojiajiri!
Kuajiriwa ni utumwa wa akili.