binafsi nimeingiza gari baada ya kuinunua z'bar mara ya kwanza ilikuwa dec 2010 wakat huo ilikuwa naafuu sana kwan ushuru ulikuwa unakadiriwa.
kunachofanyika ni kwamba, gari ikiingia zanzibar inalipiwa ushuru ambao kwa hesabu za bongo ni mdogo so kama ukiinunua na kuileta huku wanakadiria ushuru na kukuambia ulipe balance baada ya kutoa ule uliokwisha lipwa zanzibar. i saved a million shs
kwa sasa TRA wana njia mpya ya kulipa ushuru. ushuru haupigiwi kwenye bei uliyonunulia gari badala yake wanapigia kwenye depreciated price
kwa hiyo hata kama utanunua gari kule na ikawa imelipiwa ushuru kidogo, ukija nayo huku unalipa ushuru to the point that ni bora ununue huku huku
jun this year nmenunua tena gari kule na kilichotokea ni kwamba imenigharimu laki sita zaidi ya kama ningenunua hapa.
this difference is due to the fact that the dealer had his profit in the selling price and i have to pay for transporting the car to dar and pay the argent for clearance