Kuagiza subaru forester

I think for long journeys inabidi nichkue subaru coz wa2 wanasema hata ukikanyaga vipi haziyumbi hata ukipishana na semi spid haitikisiki ukizingatia mimi nataka kuitumia long journeys...
 
Kama unataka presha na ugonjwa wa moyo nunua hiyo gari .kama hutaki achana nayo kuna jirani yangu kaamua kuuza yake sasa anatembelea IST unafikiri mchezo ilimfilisi
 
mkuu kwa hio auto inakufa gia box mara moja kushinda manual?

Yangu Manual haijasumbua gia box wala engine,imeingia bongo 2011.Ni imara sana,ila sehemu nyingi inatumia umeme.kwa Daresalaam spare zipo maduka special ya Subaru.Dar vile vile fundi nadhani fundi ni mmoja aliiyemtaja mdau,yuko mitaa ya Mwenge karibu na TRA.
 
wakuu nimeona niunganishe swali langu hapa mfano umenunua gari kwa dolla 6000 ukiifikisha bandarini unalipia gharama kiasi gani hadi kuitoa na kuanza kuitumia
 
kaka kama ni gari ya kwanza achana nayo kama ishu ni 4wheel nunua rav4 hiyo gari ni ya mashindano na wazoefu wenye magari mengi,kwanza mafuta pili spare cylinder head yake inauzwa milioni moja sawa na engine nzima ya gx100,mafundi ndio hao wanahesabika ,pata picha inakufia singida on the way to mwanza utalivuta mpaka dar
 


Subaru ni gari ya vijana wa Arusha.We mtu wa Dar huiwezi!!!

Nenda kwenye GX 110
 
Mimi ndio gari yangu mkuu nimeitumia kwa miaka mnne sasa sina shida nayo nasafiri nayo mafuta kawaida tu kwani nimegundua gari zinazokula mafuta kidogo life span yake ni ndogo sana subaru injini yake ni imara sana.Kitu utunzaji tu
 
Mimi nilianza kujipanga kuagiza subaru imprezza, vp yenyewe inaunafuu, au ni vilevile kama forester
 
Habari wanajamii .....nnampango wa kuvuta forester naomba msaada nitumie kampuni gani kuagiza toka japan ambayo iko cheap na haina usumbufu au ujanjaujanja.Pia hizi gari hazna matatizo??? Nsaidien

...wala usiende mbali, kuna forester inataka kuuzwa hapa, iko poa sana, kama unaihitaji ni pm
 
Habari wanajamii .....nnampango wa kuvuta forester naomba msaada nitumie kampuni gani kuagiza toka japan ambayo iko cheap na haina usumbufu au ujanjaujanja.Pia hizi gari hazna matatizo??? Nsaidien

...kesho nitaipiga picha then ntakutumia, ni nyeusi
 
Me ninanyo iyo subaru forester for 4 good years now ni ya 1998 turbo cc 2000 nilinunua tradecarview ,kiukweli ukiwa na hii ndinga huwezi jutia maamuzi yako kwa nini uminunua,me nadhani ikitoka land cruiser mkonga inafuata subaru coz sina historia ya kukwama sehemu korofi, ni AWD ni mashine amabyo ukifunga spare yake ni mkataba ingawa spare zinapatikana kwa mbinde na ni bei juu. Hii mashine kwa kutoka nduki unaweza ata ukamkingia kifua mwenye V8 mafuta ni 1 ltr kwa 7.5 kms kwa yakwangu mimi. Safari za mza- dar yani ukiwa na hii mashine huwezi pata stress ndugu.
Try one brother.
 
Nunua subaru forester aka 'confidence in motion''
hii ndio gari yangu ya kwanza ,,so far haijawahi nisumbua.vuta kitu cha 2004 ,km kama 60000 hivi utaipenda.andaa dola 4500 kuingiza dar halafu kama milioni 6 hivi kuiweka barabarani.
Gari iliyonisumbua njiani ilikuwa prado..nahisi dereva wake alikuwa kichaa flani hivi kwa sababu nilitembea kwa 160 sikumkuta.
Nunua subaru...uenjoy safari!
 


Kama Prado ilikupita basi wewe ni mwoga.Mimi nina Prado na Subaru.Nikitaka kuweka heshima kwenye safari ndefu huwa natumia Subaru.Huwa natembelea 180 km /hr karibu nusu ya safari.

Gari zilizowahi nisumbua ni Kilimo Kwanza na Mercedes Benz.

Namuomba Mungu anibariki nivute Mercedes Benz. Hapo ntakuwa natembea 240km/hr.

Kilimo kwanza nitawakomesha
 
Subaru ya 2014.

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 

Kiukweli sijawahi zidisha 120 na nina Benz c class!! sasa wewe baba unawatoto Kweli hizo vurugu za 160 au 240 unawahi nini?! Hizi barabara za bongo Kweli ukakimbie 240?!rami ya mchina?! Acheni kuchezea uhai mtaacha watoto wanageuzwa house girl
 
Habari wanajamii .....nnampango wa kuvuta forester naomba msaada nitumie kampuni gani kuagiza toka japan ambayo iko cheap na haina usumbufu au ujanjaujanja.Pia hizi gari hazna matatizo??? Nsaidien

be forward unapata nzuri cif usd 2200 mpaka dar ushuru 2.7m ..dingi liko barabarani unakula miziki tu ...
 
be forward unapata nzuri cif usd 2200 mpaka dar ushuru 2.7m ..dingi liko barabarani unakula miziki tu ...

kwa hio total mpaka barabaran inasmama ngap?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…