KUACHWA /KUTENDWA SIYO MWISHO WA KUKOSA KUONA KILICHO SAHIHI KWAKO

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Unapoyaanza maisha yako baada ya kutendwa/kuachwa, huwa ni wewe utayebeba matokeo yoyote yale ya kiakili, kimwili, kiuchumi na kijamii.
Unapokuwa peke yako unapambana na upweke, unapambana na mazoea na unapambana na majuto.
Ni maamuzi ya kihisia, mtu unapokuwa mgumu kuukubali ukweli, kwamba wewe siyo wake tena au siyo wako tena.
Uhalisia, hupaswi kummisi hata punje mtu aliyefanya uteseke na kuanza ukurasa mpya wa maisha ambayo ukuwahi kuyawaza.
Inapaswa kutendwa/kuachwa, iwe ni mbegu ya wewe kujithamini na kujiboresha kiakili, kihisia,hadhi na mfuko wako.
Hata kama siyo rahisi, unapaswa kupambana na ujitambue wewe ni bora sana na yeyoto anayekupenda ni kwasababu amekuona wewe ni bora.
Unapompa thamani, ni sahihi ila anapogeuka na kuwa maumivu kwako, usione tabu, kukubali kuyaanza upya maisha yako.
Mapenzi hayaishi yapo, uzuri wa mtu upo kwenye macho ya mtu na kupoteza ni mwanzo wa kutafuta na kujua ulipokosea.
Unapoendelea kulazimisha mapenzi na asiyeona chozi lako, maumivu yako na namna umpendavyo ni kuzidi kujiumiza, kijidhoofisha kiakili, kimwili , kiuchumi, kufungua watu waone kichaa chako na kujidhalilisha.
Mwenye kuamua kukutenda ubaya hata siku moja hawezi taka wewe ufanikiwe, uimarike, uboresheke, upendeze wala uwe mwenye furaha. Furaha yake ni wewe kuzidi kudhoofika, apate mengi ya kusema juu yako, usikubali.
Jitenge na wasiojua thamani yako
#imarika
#Ukomo wa maisha hautabiriki, chukua fursa ya kujali afya na muda na siyo kubadilisha uongo kuwa ukweli utakusumbua.
Na mwandishi "mmmuhumba".
20230124_070320.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom