DEMOKRASIA KWA MAANA YAKE HALISIA HAIWALAZIMISHI KITU WAPINZANI
NCHINI KUFUATA NJIA MOJA TU WAIPENDAYO CCM
CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA, msisikilize maneno ya kipuuzi hapo juu; enyi Wah wetu Dr Slaa, Freeman Mbowe, Prof Lipumba, James Mbatia, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Tundu Lissu, Mabere Marando na wengine wengi tu tafute; katafuteni haraka 'MKAKATI WA SIRI' wa kufanya kazi kwa pamoja Igunga na mwisho kutuletea mwakilishi wa wananchi kwa mara ya kwanza katika kipindi chote cha miaka 15 iliyopita.
Manene ya hapo juu tafsiri yake rasmi ni kwamba CCM imeanza kutetemeka matumbo ENDAPO WAPINZA WATAPATA BUSARA ya kufanya kazi kwa pamoja maana kwa strategy hiyo wanajua wazi maana yake itakua vipi huko Igunga na kwingineko nchini.
Hakika Demokrasia si lazima iende kwa mtindo mmoja tu bli ukweli ni kwamba kuna njia kibao za watu kufika Igunga pindi unapotokea katika pembe yoyote ya taifa hili. Kwa kuwa maana halisi ya neno demokrasia (ambayo kimsingi hatuifahamu nchini) ni UAMUZI WA WATU WENGI KATIKA NCHI, KWA MASLAHI YA WATU WENGI KATIKA NCHI NA YAKIONGO NA CHGUO LA WATU WENGI HAO ili malengo ya pamoja yaweze kukidhika ipasavyo.
Hivyo basi, bado inawezekana wapinzani wakafanya mchakato wa kila chama kufanya mchujo binafsi wa wagombe wake kisha wakawapambanisha wale wagombea bora waliobahatika kushinda katika kila chama cha upinzani kimojawapo ili mgombea bora zaidi akapatikane miongoni mwao wale washindi katika kila chama.
Baada ya hapo, yule atakayeonekana kuwashinda wenzaake wote katika kinyang'anyiro hicho cha kufa mtu mwishowe hukabidhiwa bendera ya vyama vyote vilivyoridhia mkakati huo na sasa mbio za kuwang'oa mafisadi kung'oa nanga rasmi jimbo baada ya jimbo.
Na wewe Mwita hapo juu, ni bora ukaanza kushiri mawazo kama haya tena bila mzaha wowote ili CCM kisije kikapata ugumu sana baada ya sisi wapiga kura kukigeuza chama cha upinzani miaka si mingi sana toka sasa.
NB: Na nyinyi Maxence Mello, Invisible pamoja na William Malecela; hili la KUCHOMOA BAADHI YA SHIREDISHI kali ubaoni bila taarifa yoyote kwa wanajamvini ndio tuseme ni demokrasia ya wapi???????
Tunaomba majibu hapa jukwaani haraka.