Kuachinana Majimbo ni kuua demokrasia ya ushindani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuachinana Majimbo ni kuua demokrasia ya ushindani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Sep 4, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wapo watu wanasema vyama vya upinzani viwe vinaachiana kwa kupima upepo chama kipi kina nguvu katika kila eneo la uchaguzi ili wakishatambua wakiunge` mkono chama kile. Mimi sikubaliani na sitakaa niunge mkono dhana hii kwa sababu voters want a variety of political tastes, they dont vote solely on personlity they put across a combination of many factors. Watu wanatakiwa kuwapanga wapiga kura katika makundi yafuatayo;
  • Wale ambao piga ua wanapigia vyama, kwa kiwango kikubwa kundi hili lisipoona ushiriki wa chama chao linaweza kuto kwenda kupiga kura
  • Washabiki wa masuala ya kisera hawa wengi hupigia kura mtu kutokana na anavyowagusa kwa sera na kutambua matatizo yao
  • Kundi la tatu ni wale wa bendera hufuata upepo hawa hupigia mtu yeyote wanaeona ana mvuto kwa wat waliowengi na hawa ndio kundi ambalo ni rahisi kulibadilisha
  • kundi lingine ni lile la watu wenye hasira na uongozi wa chama chao hawa hupigia chama kingine kwa kukomesha
  Na kwa hiyo uwepo wa vyama vingi hauna uhusianao mkubwa na uvurugaji wa kura za upinzani, unaweza pia kuvuruga kura za chama tawala kwa sababu kitakuwa na maadui wengi wa kukidhoofisha kwa mashambulizi ya maneno kila kona.

  Ushiriki wa vyama vingi katika mchakato wa uchaguzi ni nguvu badala ya udhaifu tulione hivyo na tukubali liende hivyo

   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mtapeana majibu wapinzani kwa wapinzani. Hii hainihusu
   
 3. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CHADEMA imeachia jimbo la urais kwa miaka 10 ndipo wakamuweka muasisi wa kampeni kwa helikopter.

  Uchaguzi wa serikali za mitaa nako hawajajitoma sana na waliachiwa wengine.

  Mwaka 2010 ulikuwa wa mwisho kwao kuachia majimbo na 2015 usitegemee jimbo likakosa mgombea ubunge wa CHADEMA.

  Kuachia jimbo ni ishara kwamba chama ni kichanga na hakina tishio lolote kwa chama tawala.

  Ukitaka kujua uchanga huo CHADEMA imeshaupa kisogo ingia JF halafu fuatilia thread zinatungua upinzani uone ni chama gani kinalengwa na majina ambayo hata kama hujui kukariri lazima yatakukaa kichwani.

  Kama husomi JF basi nunua gazeti la UHURU na dada zake ujue ukubwa wa CHADEMA kana kwamba havipo vingine.

  Ndiyo sababu rafiki zangu na hata wauza magazeti wenyewe hunishangaa ninaponunua UHURU kila siku , hawajui ninapima upepo kuwa ni chama gani ni tishio kwa CCM hadi kutopuuzwa kwa kukaliwa kimya.

  Hivyo CHADEMA wasiingie mtego wa kuachia majimbo kwa kusikiliza lugha tamutamu kuhusu hili.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  DEMOKRASIA KWA MAANA YAKE HALISIA HAIWALAZIMISHI KITU WAPINZANI
  NCHINI KUFUATA NJIA MOJA TU WAIPENDAYO CCM


  CUF, NCCR-Mageuzi na CHADEMA, msisikilize maneno ya kipuuzi hapo juu; enyi Wah wetu Dr Slaa, Freeman Mbowe, Prof Lipumba, James Mbatia, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Tundu Lissu, Mabere Marando na wengine wengi tu tafute; katafuteni haraka 'MKAKATI WA SIRI' wa kufanya kazi kwa pamoja Igunga na mwisho kutuletea mwakilishi wa wananchi kwa mara ya kwanza katika kipindi chote cha miaka 15 iliyopita.

  Manene ya hapo juu tafsiri yake rasmi ni kwamba CCM imeanza kutetemeka matumbo ENDAPO WAPINZA WATAPATA BUSARA ya kufanya kazi kwa pamoja maana kwa strategy hiyo wanajua wazi maana yake itakua vipi huko Igunga na kwingineko nchini.

  Hakika Demokrasia si lazima iende kwa mtindo mmoja tu bli ukweli ni kwamba kuna njia kibao za watu kufika Igunga pindi unapotokea katika pembe yoyote ya taifa hili. Kwa kuwa maana halisi ya neno demokrasia (ambayo kimsingi hatuifahamu nchini) ni UAMUZI WA WATU WENGI KATIKA NCHI, KWA MASLAHI YA WATU WENGI KATIKA NCHI NA YAKIONGO NA CHGUO LA WATU WENGI HAO ili malengo ya pamoja yaweze kukidhika ipasavyo.

  Hivyo basi, bado inawezekana wapinzani wakafanya mchakato wa kila chama kufanya mchujo binafsi wa wagombe wake kisha wakawapambanisha wale wagombea bora waliobahatika kushinda katika kila chama cha upinzani kimojawapo ili mgombea bora zaidi akapatikane miongoni mwao wale washindi katika kila chama.

  Baada ya hapo, yule atakayeonekana kuwashinda wenzaake wote katika kinyang'anyiro hicho cha kufa mtu mwishowe hukabidhiwa bendera ya vyama vyote vilivyoridhia mkakati huo na sasa mbio za kuwang'oa mafisadi kung'oa nanga rasmi jimbo baada ya jimbo.

  Na wewe Mwita hapo juu, ni bora ukaanza kushiri mawazo kama haya tena bila mzaha wowote ili CCM kisije kikapata ugumu sana baada ya sisi wapiga kura kukigeuza chama cha upinzani miaka si mingi sana toka sasa.

  NB: Na nyinyi Maxence Mello, Invisible pamoja na William Malecela; hili la KUCHOMOA BAADHI YA SHIREDISHI kali ubaoni bila taarifa yoyote kwa wanajamvini ndio tuseme ni demokrasia ya wapi???????

  Tunaomba majibu hapa jukwaani haraka.

   
Loading...